mkulungwa03
JF-Expert Member
- Apr 1, 2021
- 317
- 243
Nilizushiwa naendana na kademu kamoja hvi kila kona skuli wanatutania mimi na yule demu, nikajisemea apa acha niitumie hii chance ishu ikaja naanzaje???Namwambia nini?Nakumbuka nikiwa darasa la nne kulikuwa na wadada wawili marafiki sana walioshibana sasa kila mmoja akawa ananitaka ki mpango wake, na shule nilijulikana kwa vitu viwili, 1.Kuchelewa 2. na kushika namba moja kwa kila mtihani mpaka namaliza darasa la 7,
Basi wale wadada walikuwa wamenizidi madarasa mawili ila kiumri nilikuwa nimewazidi maana nilichelewa kuanza shule kisa kamali za karata (chafu tatu)
So siku moja kila mmoja akanifuata ki mpango wake kwa kuniambia anatamani tuwe wapenzi tena kwa kunipa vijisent
Me kutokana na ushamba harafu ndio mara yangu ya kwanza nikawa naogopa nikawa nawakwepa, wakiandika barua wakizituma sijibu, ikatokea siku moja mwanafunzi wa shuleni akafariki basi tukatawanyishwa mapema na njia ya kwenda home ilikuwa lazima upitie msitu wa secondary furani hivi, mmoja wa wale mademu akanifuata nyuma nyuma nilipofika kwa ule msitu nilikuwa peke yangu akanishika mkono akaanza kunikumbatia mara busu za lazima akanivuta mstuni ndani akavua nguo ile namuona uchi wake aisee nilikimbia mbio naogopa,
Rafiki yake alipofahamu kilicho tokea walizibuana wakawa maadui mpaka kwa wazazi maana waliishi karibu karibu.
Mpaka leo hii ukubwani tukikutana wananisimanga kuwa me domo zege,
mmoja amesha olewa, mwezake ndo kahaba wa kujiuza kwenye majiji makubwa huko
Nikawazaaa nikaona huyu acha nitumie njia yetu ile nikachukua daftari langu nikachana katikati nikawa na karatasi kubwaaa ..... Sasa hapo naandika nini likawa swali jingine gumu kichwani mwangu nikaona nikimshirikisha mtu yeyote nitachekwa na ukikumbuka miaka hyo sio mchezo.
Naanza kuandika "Mimi nakupenda Sana nimevutiwa na wewe siku nyingi naomba uwe wa maisha yangu " hapo swaga zikawa zimeisha ile karatasi haijafka hata robo nikaona isiwe kesi ile space yote iliyobaki kwenye karatasi nikachora luv(kopa) kubwaaa kujaza karatasi yote halafu nikachora na mshale katikati.
Nikampa mwamba mmoja apeleke hyo tupo form nyoya apo basi nimekaa nasklizia majibu mara naona anakuja demu na marafiki zake kama 8 hvi nikasema leo kweli Mkulungwa03 nimepatikana wakafika nilipo huku wakicheka hatar kuwa eti ndo huyu kaandika kile kibarua cha kunitongoza DUUUH nilichekwa Hadi nikaichukia shule nikawa mtu wa kujificha Hadi clas kuzama naogopa ila nikajitaidi kujikaza likaisha hilo swala na mtoto hata sikumpata😂😁