Nilikua namfukuziaga kimoyo moyo mtoto mmoja hivi alikua kanizidi kidato, ye form 2 mi form 1
Alikua machine ya hatari kwa sasa wanaita pisi
Dada alikua mzuri balaaa halafu hakuwa na dharau yaani MTU wa watu, wengi walimchukulia kama anaringa kwa sababu ya uzuri wake, wengi walikua wanaogopa hata kupiga nae story,
Kwahyo mi nikawa namsubiria barabarani akipita kutoka tuition namsindikiza kwao huku tukipiga story za hapa na pale,
Washikaji wakawa wananiuliza vipi ushatupa ndoano?
Nikawajibu nishakula tunda kitambooo,
Walinisifia sana kwani demu alikua Chuma kweli kweli yaani mpaka Leo yule Dada hua hachuji,
Aisee ilipita mda mrefu sana nikifanya hii tabia ya kumsindikiza na kuwadanganya washikaji zangu kua namla yule mtoto,
Roho ilikuja kuniuma baada ya kusikia yule demu kaliwa na boya mmoja hivi ambae nilikua na bifu nae pale mtaani,
Nilikua na bifu nae kuanzia Kwenye micjezo yetu mpaka wazazi wetu pia kifupi bifu La kurithi,
Nikaona nijitutumue namimi nifanye kweli sasa,
Nakumbuka nilikuatana nae kama kawaida nikaanza kumsindikiza, nikaanza kujiuma uma na voko za kishamba akawa hanielewi akaniuliza kuna tatizo gani?
Nikamuuliza et Anna unanipenda, akajibu ndio, basi niliachana nae nikiwa na furaha kinyama,
Kesho yake nilipoonana nae nikawa namkomalia sasa anipe jibu langu,
Akiuliza lipi nikawa namwambia we jana. So tushakubaliana jamani tuwe wapenzi,
Alishamgaa sana et Haaaaaaaaah!
Aisee nilijiskia aibu sana maana tulikua tunaheshimiana,
Nikawa namkwepa sitaki hata kuonana nae daah bahati nzuri alihama shule ndio nikawa afadhari kwangu, loooh ile aibu sintokuja kuisahau