Habari za jumapili Wakuu!
Miaka hiyo bhana! Niko zako mwaka wa Kwanza nikiwa Likizo. Nimerudi zangu Moshi. Sasa mtaa tuliokuwa tunakaa ni karibu na Kota za Polisi pale Moshi Mjini. Kwa wanaojua Moshi Mjini Basi karibu na Club kubwa inayoitwa HUGO Club. Kutoka Hugo Club na uwanja wa mashujaa sio mbali kivile.
Kipindi hicho Nina wenge balaa. Kila demu mzuri anayepita barabarani namtaka.
Kwa wale ambao hamjawahi kufika Moshi niwaelezee Hali ya Moshi na Arusha Mjini kwa upande wa wanawake.
Hii miji ndio miji pekee ambayo kila demu utakayemuona barabarani lazima awe na sura nzuri. Asilimia themanini ni light skin, asilimia 19% ni maji ya kunde mtelezo. Hiyo 1% iliyobaki ndio utakuta wenye rangi nyeusi.
Ninaposema sura nzuri namaanisha sura nzuri. Sio zile za mkorogo au makeup.
Watoto warefu na wenye urefu wa Kati.
Mazingira ya Moshi barabara zake zimezingirwa na miti upande na upande hivyo kuna kuwa na vivuli na Hali ya hewa inakuwa imepoa hasa nyakati za baridi au nyakati za mvua.
Ukitaka uufurahie mji wa Moshi kama kijana mwenye umri Kati ya Miaka 15-25 basi Muda WA kutoka kutembea uwe kuanzia saa Tisa mchana Mpaka kumi na mbili.
Muda wangu wa kutoka kutembea kama kijana asiye na Kazi, asiyejishughulisha, mwanachuo aliyelikizo, aliyemapumzikoni akijaribu kuifurahisha akili na macho yake ilikuwa saa kumi unusu hivi.
Mimi ni wale watu ambao sipendi kutembea kimakundi, ukiniita Tiger kitabia hutokuwa unakosea. Hivyo mara nyingi Sana ungenikuta pekee yangu. Na hiyo usiihesabu kuwa siongeagi na watu au sina washkaji nope!
Naendelea;
Eneo jingine nyeti kwa uwindaji wa warembo ni katika soko la Memorial ambalo ndio soko kubwa Mjini Moshi.
Hapo utakutana na watoto warembo wa kila namna.
Watoto kutokea Arusha, Moshi na wakati mwingine kutokea Kenya.
Bahati nzuri kutokea nilipokuwa naishi hadi sokoni, memorial sio mbali ni mwendo wa dakika thelasini kwa mguu unakuwa ushafika.
Nikaenda zangu sokoni sio kwaajili ya kununua bidhaa Bali kuosha macho na kutafuta vitoweo. Ujana ulikuwa umeniwakia kama Jua la utosi.
Nikiwa nipo sokoni sasa, nikiwa makini kuangalia watoto wazuri huku kelele za wauzaji nikizidhibiti zisiondoe umakini wangu. Natazama nikaona mwanamke mweupe hivi, mwenye umbo thabiti na urefu wa Kati, macho yake makali kiasi lakini sura isiyo na mashaka.
Mwanamke yule alikuwa amevaa suruali ya jeans ya kuvutika iliyochora umbo lake kikamilifu, ni Yale maumbo ambayo sio mwembamba Sana Wala sio mnene. Yupo Kati, Kibindo chake kilikuwa cha Kati labda kimahesabu ni Ratili Tatu kwa nusu Ratili.
Juu alivaa blauzi sikumbuki ilikuwa rangi gani lakini mkufu mdogo ulikuwa ukining'inia shingoni.
Juu kichwani alikuwa kavaa Cap(kofia) ambapo kwa miaka Ile kule Moshi mabinti wengi walikuwa wanatabia hiyo.
Kiumri alikuwa ni Mkubwa mbele yangu kwa miaka isiyozidi mitano. Alikuwa Kati ya Miaka 23-25 hapo.
Pepo mchafu akaniingia kwa nguvu zote na kunipa maelekezo nimkabili Yule Mrembo
Sasa nikawa natafuta nafasi ya kumkabili.
Nilikuwa namfuata nyumanyuma kama kimelea cha mkia wa bakteria.
Tulianzia kwenye soko la nguo yeye Akiwa za kike, suruali akachagua wee akatoka Mimi nikiwa banda la nyuma yake nami nikichagua kana kwamba ni mteja. Maskini muuzaji alikuwa akihangaika Sana tolea nguo akidhani nilikuwa na pesa kumbe hata Mia mbovu sikuwa nayo.
Yule mwanamke alipohama nami nikawa nahama hivyohivyo kinyemela nyuma yake tadhani Mtekaji wa watu.
Ni nusu saa sasa imepita tangu nijipe Kazi ya kumfuatilia huyu Mrembo. Sasa akatokea upande wanapouzia Samaki huku, hapo nikagundua amejua kuna mtu anamfuatilia.
Huku kwenye Samaki kelele sio nyingi na watu sio wengi kivile. Akanitazama akataka kama kuongea Jambo lakini akaishia kutabasamu.
Hiyo ikanipa mjadala kichwani mwangu. Atakuwa anamaanisha nini?
Huyo tukatokea uwanjani huku kwa sababu Hilo soko la Memorial kulitakiwa kujengwe uwanja wa Mpira wa Jamhuri. Lakini wameishia kujenga kasehemu kadogo kakukaa watazamaji na Kama jukwaa hivi.
Nikajisogeza tukawa sambamba tunatembea kwa pamoja kanakwamba unatoka sehemu Moja na tunaenda sehemu Moja. Au kana kwamba ni watu tunaojuana kwa Kipindi kirefu.
Tukasalimiana kisha mazungumzo yakawa yanaendelea nami nikihakikisha najiweka kwenye nafasi nzuri.
Tukatokea upande mwingine WA soko ambapo kulikuwa na mahema ya Mwamposa kwani Kipindi hicho kabla hajaja Dar alikuwa anafanya shughuli zake hapo.
Nikashangaa Yule Mwanamke anaenda upande wa mahema ya Mwamposa ambao mhubiri ambaye ni Mwamposa alikuwa anandelea na huduma yake.
Nikamuuliza kulikoni akaniambia anaenda kusikiliza mahubiri, alafu yupo na Dadaake, kweli kwa mbele nikamwona mdada mwingine Akiwa amekaa kwenye kiti anatutazama.
Ikabidi nimwombe namba za simu.
Akanitazama machoni alafu akatabasamu huku akisema Mimi ni mdogo wake namba za simu za nini? Lakini nikafanikiwa kumshawishi. Akanipa namba tukaagana.
Nikatoka zangu kurudi nyumbani siku ikiwa imeisha.
Basi mawasiliano yakawa yamechachamaa baina yangu Mimi na yeye. Hasa majira ya usiku mnene. Nikimpigia mchana alikuwa hapokei simu. Ikawa sio Kesi kwa sababu walikuwepo warembo wengine. Ujana mbaya nyie!
Alikuwa akinitafuta usiku Sana majira ya tano saa sita hivi. Hapo tutaongea weeee Mpaka saa tisa hivi. Kumbuka Kipindi hicho kulikuwa na of Fulani za kupiga usiku ukifikisha kuanzia dakika Fulani unaweza kuongea usiku mzima.
Tukapanga tutoke out kwaajili ya kujuana vizuri. Kumbuka nimemdanganya vya kutosha na kuuteka Moyo wake. Kumbe naye kanidanganya vilevile. Kiufupi tumepigana kamba za kutosha. Ila haitaondoa ukweli kuwa Joanna alikuwa amenielewa kwa sababu hakuwa na sababu ya kupoteza Muda wake mwingi kwaajili yangu ukizingatia yeye ni Mkubwa na simpi Pesa.
Tukachagua Twende Club Moja IPO maeneo ya Majengo. Ilikuwa siku ya jumapili jioni hivi kama saa moja kwenda.
Siku hiyo Joanna alipendeza Sana na ndio ilikuwa mara yangu ya pili kumwona zikiwa zimepita siku kama tisa hivi tangu tuachane kule sokoni.
Hakuvaa tena suruali. Alikuwa amevaa kigauni kifupi cha Moja kwa Moja kutoka juu Mpaka katikati ya mapaja. Chenye rangi nyeusi. Nywele zake alikuwa amezinyoa vizuri Mno na maskioni kulikuwa na vihereni vilivyo uweka mwonekano wake kijikeshupa.
Aliuliwaza moyo wangu.
Aliyapumbaza macho yangu.
Mimi wakati huo simu yangu nilishazipiga pin namba zote za mademu ili zisiniharibie mitego yangu.
Kwa jinsi alivyopendeza Joanna nilitamani ule uongo niliokuwa namdanganya uwe Kweli. Nilitamani mipango ya harusi Kati yangu na yake ianze maramoja. Kamati ya harusi iundwe na vikao vianze mapema.
Lakini hayo yote yalikuwa ni mawenge yangu yalitoyokana na uzuri na urembo wa Joanna.
Yale macho yake yasiyo na mashaka Leo hii yalipakwa sijui vitu gani, yalikuwa yanarembua mara kwa mara na kufanya mapigo yangu yapigepige kinyume na kanuni za kisayansi.
Sikutaka kupepesa hata macho nisije kukosa hata nukta Moja ya uzuri wake. Uhondo ulinikaba Mpaka rohoni
Unajua hapo tupo Club hapo. Mtoto akaagiza bia kadhaa Mimi kama mjuavyo sio mnywaji. Hii kidogo ikaleta mushkeli lakini nikaiweka Sawa.
Siku hiyo nililipia hiyo bills roho ikiwa nyeupe peeee kama theluji. Ule ubahili wangu wa kipare sijui ulikimbia wapi. Nafikiri uzuri wa Joanna ulikuwa na upako mkali wa ku-cast all demons wa ubahili moyoni mwangu.
Sasa sijui ilikuwaje hela ikaisha. Tayari ni saa tano hivi. Joanna amelewa vibaya lakini bado anakaufahamu. Mimi sina nauli ya kurudi home.
Joanna akachukua simu akapiga kwa dereva taksi kutoka pale stendi Mjini hazikupita dakika kumi tax ikaingia.
Mara Yule dereva kufika akamuita Afande, ila Joanna ni kama akamkazia macho na dereva akazuga kama anajikosha. Akasema tunaenda kwa Afande Maliki.
Mimi sikutilia Maanani.
Tukiwa nyuma ya gari mambo mengine yakawa yanaendelea dunia yote tukawa tumeizingira na kuiteka. Majeshi yetu yalikuwa imara kuimarisha Doria katika maeneo korofi.
Ilikuwa usiku lakini nafsi zetu ziliogelea katika bwala lenye Nuru ya huba.
Ningesema nini pale?
Ningefanya nini Muda ule?
Mimi hata sijui! Gari ikasikamama tukazama kwenye Geti.
Nyumbani kwa Joanna.
Mimi nikajua nampeleka tuu home kwake kisha Mimi nisepe. Yeye alikuwa anakaa mtaa Soweto. Mimi mtaa wa Karanga.
Huko Joanna akagoma nisiondoke. Hapo Dadaake tulimkuta anaangalia sijui tamthilia gani.
Nilishtuka kuona picha ya Joanna ikiwa ukutani Akiwa kavaa kipolisi. Na haikuwa picha Moja zilikuwa kama Tatu hivi.
Hapo moyo kudung! kadang! Kudung! Kadang ukawa unadunda kwa mshtuko wa taarifa Ile. Aiseeh kwa umri wangu ule wakati ule sikujua kuwa kuna wanawake warembo ambao ni maafande.
Chumbani nikakuta gwanda limening'inia kwenye henka.
Kukatisha Stori.
Siku tumekuja kupigana ni baada ya kufumania meseji kwenye simu yangu.
Aiseeh! Tulipasuana kwelikweli! Anarusha mateke Yule mtoto sijapata kuona. Anarusha ngumi Yule mtoto. Alipoona namzidi ujanja, chupa za pombe na stuli yaani ilikuwa mbilinge mbilinge.
Nawatakia wikiendi Njema.
Mtibeli katika Moja na mbili.