Marafiki hawadumu wanakuja na kuondoka tofauti na ndugu wa damu, Mnapoamua kupata mtoto moja wakati uwezo upo ni kumtesa mtoto, idadi nzuri ni 3+

Marafiki hawadumu wanakuja na kuondoka tofauti na ndugu wa damu, Mnapoamua kupata mtoto moja wakati uwezo upo ni kumtesa mtoto, idadi nzuri ni 3+

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Siku zote kaka na dada yako ndiyo ndugu zako wa kweli na marafiki zako wa kweli. Uhusiano wako na wao ndiyo unaokuelezea uhusiano wako na binadamu wengine.

Baba na mama hawatakuwepo uzeeni mwako na watoto wako hawatakuwepo utotoni na ujanani.

Kaka na dada zako watakuwepo karibu maisha yako yote na vice versa.

Unashauriwa kama una uwezo uzae watoto wengi, mtoto awe na mwenzake lakini ikipendeza zaidi awe na wenzake.


Hata kama kuna changamoto na ugomvi wa hapa na pale, udugu una nguvu ya kipekee inayowaunganisha katika nyakati zote za furaha na huzuni.

marafiki wa nje wanaweza kubadilika kutokana na mazingira au hali za maisha, ndugu wa damu wanabaki kuwa sehemu ya historia yako milele.

mnaweza kuwa watatu kwenye familia, wote bado mnajitafuta lakini kuna namna mnashikana mikono katika namna ambayo marafiki hawawezi, rafiki akijitahidi basi ni muda mfupi

Hata kama kuna changamoto na ugomvi wa hapa na pale, udugu una nguvu ya kipekee inayowaunganisha katika nyakati zote za furaha na huzuni. kuna tukio niliwahi kuliona kaka na mdogo wake hawapatani vizuri lakini kwenye shida wanaendelea kusaidiana, kaka mtu alikamatwa, kilihitajika kiasi kikubwa cha pesa kumnasua, mdogo mtu alipambana usiku na mchana kuuza mali zake za thamani kwa bei ya kutupa ili amtoe kaka yake, wale wa kuitwa marafiki walimkimbia matatizoni.

Ni kosa kubwa sana ikiwa mna uwezo wa kupata watoto wa ziada muamue kupata mtoto moja, ni kumnyanyasa mtoto kwenye future yake
 
ni kweli, uzeeni ndo unajuta kwanini una mtoto mmoja tu au wawili... na hana hata wa kusaidiana naye malezi ya wazee, tutafute hela na tusiogope kuzaa, angalau 3-5 ni namba utayojivunia sana ukiwa uzeeni
 
ni kweli, uzeeni ndo unajuta kwanini una mtoto mmoja tu au wawili... na hana hata wa kusaidiana naye malezi ya wazee, tutafute hela na tusiogope kuzaa, angalau 3-5 ni namba utayojivunia sana ukiwa uzeeni
Hii ipo sana kwa wezetu wa Ulaya na Mrekani, mtu anaamua kupata mtoto moja tu, akifika uzeeni anapelekwa vituo vya kulelea wazee kwasababu mtoto hana wa kusaidiana naye
 
You have a point.

Sisi Tumezaliwa wa3. Wote bado tunajitafuta lkn kuna namna tunashikana mikono in the ways, Mtu baki asinge weza kutushika
 
Watoto watatu ni wengi wakiwa wadogo ila wakishakuwa wakubwa kila mtu anajitafutia utaona ni wachache sana kipindi hicho wewe ukiwa mzee l.
 
Tafuta pesa Ukiwa na pesa utalelewa vizuri hata kama Una Mtoto mmoja. Tatizo umezeeka na pesa huna ,huyo Mtoto akamtafute pesa ya kuleta familia yake na pesa ya kukulea wewe at the same time awe jirani na wewe...Ukiwa na pesa na mazingira mazuri ya kuishi hata wajukuu hawakauki kwako.Mchawi mpunga
 
Aysee mimi sitokuwa na idadi ya watoto, nikiwa na uwezo mkubwa ndio nitakuwa na team kubwa zaidi....mali nyingi watoto wengi atleast 10
 
You have a point.

Sisi Tumezaliwa wa3. Wote bado tunajitafuta lkn kuna namna tunashikana mikono in the ways, Mtu baki asinge weza kutushika
Ndugu mta stick pamoja lakini marafiki hali zikianza kutofautiana ndio mwanzo wa mpasuko,
 
Back
Top Bottom