Mfamo wa wakati huu wa mawasiliano hutegemea sana electronics. Huko kuna vitu vinne tu ambavyo ni😀iode ,capacitor,inductor na rsistor. Diode ndiyo bwana na wengine ni wasaidizi. Mchezo wote huchezwa kwenye diode ambayo huweza kupata derivatives nyingi kama transistors,thyristors nk hivyo kupelekea application tofauti. Muunganiko wa hivi hutoa chochote,mfano:radar,tv,radio,dvd,memory cards,computer nk,chumba kitakachowekwa humruhusu mtu wa IT kutumia maarifa kidogo aliyopewa kutumia chumba alichopewa kufanya programing na yafananayo. Naomba kuuliza wadau,hivi designer akitaka mtambo wake kutuchunguza kisha akatuuzia ama kutupa msaada kama ilivyozoeleka akaweka sehemu moja chumba tuwezachokukiona na kukitumia kwa mfano kama data center yetu na chumba cha pili kisionekane kwetu lakini kimsaidie designer kumpa taarifa yoyote ipitayo kwa chombo hicho je tutakuwa na jinsi ipi ya kujilinda?
Ni bahati mbaya sana kwamba elimu yetu imetugawa sana,mfano mtu wa umeme hujifunza kuzalisha umeme lakini hafundishwi umeme ni nini na unaenda kufanya kazi gani,mtu wa electronics anajifunza vifaa hivi lakini hafundishwi vitatumikaje kupitisha taarifa na mtu wa IT anafundishwa kupitisha taarifa kwa vifaa ambavyo hajui siri za uundaji wake,na bahati mbaya zaidi wote hawa sehemu kubwa wamejifunza kukidhi vigezo vya mitihani na siyo uelewa.