Marangu Coach imefikia hatua hii

Marangu Coach imefikia hatua hii

Tuliposema mabasi ya kichina ni hovyo tulishambuliwa tukaambiwa hatuendi na wakati, huo upuuzi hutausikia Kilimanjaro Express, wale gari zao nyingi kama siyo zote ni toughened and trusted Scania
Kilimanjaro Express nao ni hao hao mwezi wa nne mwaka huu tumetoka Shekilango saa kumi na mbili asubuhi kufikia Mwenge ikapata break down tukafaulishwa,kifupi Kilimanjaro Express ilikuwa zamani sasa ni zamu ya BM
 
Hebu tujikumbushe kwa wale waliowahi kusafiri na mabasi ya shirika la reli kabla ya EAC kuvunjika, basi linafanyiwa sevisi Dar likifika Iringa linafanyiwa sevisi na likifika Mbeya linafanyiwa sevisi, yalikuwa hayaharibiki njiani. EAC ilipovunjika uzembe na upigaji ukaanza, sevisi zikafa kwa kutekwa na sevisi bandia za wizi wa spea magari kila siku mabovu mpaka shirika likashindwa kuendelea , na si mabasi tu hata treni nayo ikakumbwa na tatizo hilo treni zikakata pumzi.
 
Kuna zarura, kuwa mwelewa. Kuna wakati hata kunguru anafia kwenye engine ya ndege.
Dharura ya kuacha kuagiza spea kutoka umbali wa km 60 na kuiagiza kutoka umbali wa 400+ kilometers huo siyo ujinga tu ni uwendawazimu.

Labda kama gari imekodiwa lakini unajua kabisa waliopanda humo wengine wana watoto,wengine wazee ni wagonjwa wengine wanawahi mambo yao mbalimbali halafu kweli gari iharibike ufanye jambo kama hilo?je umejipanga kuwapa chochote baada ya uvumilivu watakaokupa?
 
ABC upper class inabidi achangamkie fursa na kuwaletea ruti huko Moshi, maana migari mingi inaonekana mingarangara
 
Wahindi na waarabu mtoto akizaliwa tu anaingizwa kwenye biashara na atakulia ndani ya biashara japo anaenda shule, akikua staendeleza biashara hiyo kwani amekulia ndani yake na ndicho kinafanya biashara zao ziendelee kuendeshwa na vitukuu na vilembwe kwa jina lilelile la mwaka 1920!
 
Dharura ya kuacha kuagiza spea kutoka umbali wa km 60 na kuiagiza kutoka umbali wa 400+ kilometers huo siyo ujinga tu ni uwendawazimu.

Labda kama gari imekodiwa lakini unajua kabisa waliopanda humo wengine wana watoto,wengine wazee ni wagonjwa wengine wanawahi mambo yao mbalimbali halafu kweli gari iharibike ufanye jambo kama hilo?je umejipanga kuwapa chochote baada ya uvumilivu watakaokupa?
Tena kama limekodiwa inabidi ukodi gari nyingine iwapeleke.
 
Wahindi na waarabu mtoto akizaliwa tu anaingizwa kwenye biashara na atakulia ndani ya biashara japo anaenda shule, akikua staendeleza biashara hiyo kwani amekulia ndani yake na ndicho kinafanya biashara zao ziendelee kuendeshwa na vitukuu na vilembwe kwa jina lilelile la mwaka 1920!
Wenzetu wanafundisha watoto wao kusimamia mali, sisi tukipata mali tunataka watoto wetu waishi kimayaimayai hata kujifulia nguo zao tu hawawezi, unakuta mzazi anamiliki gereji kubwa yenye mashine za maana lakin mtoto akiwa likizo anatumia huo muda kula bata kwenda anapotaka na kuangalia TV

Siku baba ukifa ujue na mali zinaondoka hizo wale mafundi lazima wagawane mali zako maana kwenye familia yako hamna mwenye idea na hizo mashine
 
Back
Top Bottom