Mpira umemalizika dakika zilizopita na matokeo ni sare ya goli 1-1 kwa wenyeji Coastal Union na Singida Big Stars.
.
kilichofanya niandike ni namna maamuzi ya ajabu ya Refarii aliyokuwa anayatoa kwa kuwapendelea zaidi wenyeji Coastal.
.
Dakika ya 88 Singida walipata bao la wazi lisilo na kosa lolote lakini bila ya aibu Refa kalikataa bao lao, kiasi cha kuleta mtafaruku baada ya kipyenga cha mwisho.
TFF wawe wanafatilia kwa karibu sana mechi ambazo hazihusishi timu kubwa za Simba na Yanga.
Hizi zinakuwa na maamuzi ya ajabu sana kama mechi za ligi daraja la kwanza aliyeko nyumbani lazima ashinde na akizidiwa sana basi sare ipatikane.
Soka letu linachangamoto nyingi sana