Marehemu Grace Mapunda ni nani? Mbona Msiba wake umekuwa mkubwa sana

Huba ni habari ya mjini ndo maana msiba wake umekuzwa sana. Amefariki akiwa msanii active na October alikua kideoni kama kawa akitoa burudani ya sanaa
 
Kuna namna labda aliishi na watu vizuri na kuwagusa either in positve.

Tuupe Muda nafasi .

Rip
 
Ameanza kuigiza tangu miaka ya 90, ila zaidi amefahamika mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati ambapo kituo cha habari za ITV kuanza kurusha tamthiliya zao.

Alikuwa anajua kubeba uhusika kwenye maigizo yake.

She will real be missed 😭
Waigizaji wa aina hii ni wale tunaowaita ma-super star wa madada wa kazi. Hakuna watu wanaojitambua wanaongalia huo upuuzi wao.
 
Itakuwa wewe ni wa juzi au sio mtu wa Bongo Entertainment
 
Hawa ni waigizaji wa aian hii ni wale tunaowaita ma-super star wa madada wa kazi. Hakuna watu wanaojitambua wanaongalia huo upuuzi wao.
Wanaume wengi tumechagua kuwa wapenzi wa kuangalia Mpira wakati huo wenzetu wa kike wamechagua kuangalia hizo tamthiliya.

Japo Siku hizi, imeanza kuwa kawaida Wanaume pia kuwa wapenzi wa tamthiliya za Azam
 
Misiba Mingi ya Wasanii inakuzwa kwa sababu walio hai hilo ndilo Eneo la kutafuta Kiki.

Hasa kuelekea Msimu wa Uchaguzi kama huu hata wasiomjua kama Chalamila na Shigongo nao watajitokeza kujizolea Umaarufu
Shigongo kasema alikuwa mwenza wake, wameishi wote mpaka mauti yanamkuta jukumu la wanae atalibeba yeye siku zote
 
Hizo ni hearsays tu

Yanaweza kuzungumzwa mengi kwenye huu Msiba, ila Idara ya Usalama imeingia Kila mahali kuanzia michezo/burudani/vyuoni/hospitali n.k

Lakini pia msisahau kwamba tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Chama tawala lazima kioneshe mshikamano na hilo kundi la Wasanii maana wamekuwa wakiwatumia Kila Mwaka wa Uchaguzi

Wanatumia ule usemi kwamba "akufaaye Kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…