Marehemu Grace Mapunda ni nani? Mbona Msiba wake umekuwa mkubwa sana

Marehemu Grace Mapunda ni nani? Mbona Msiba wake umekuwa mkubwa sana

Huba ni habari ya mjini ndo maana msiba wake umekuzwa sana. Amefariki akiwa msanii active na October alikua kideoni kama kawa akitoa burudani ya sanaa
 
Kuna namna labda aliishi na watu vizuri na kuwagusa either in positve.

Tuupe Muda nafasi .

Rip
 
Ameanza kuigiza tangu miaka ya 90, ila zaidi amefahamika mwanzoni mwa miaka ya 2000 wakati ambapo kituo cha habari za ITV kuanza kurusha tamthiliya zao.

Alikuwa anajua kubeba uhusika kwenye maigizo yake.

She will real be missed 😭
Waigizaji wa aina hii ni wale tunaowaita ma-super star wa madada wa kazi. Hakuna watu wanaojitambua wanaongalia huo upuuzi wao.
 
Sote tunafaham ni Muigizaji (Msanii) lakini sio big fish kama Kanumba katika sanaa ya maigizo. Samata katika sanaa ya mpira. Diamond katika sanaa ya mziki. Mbowe katika siasa

Msanii Grace Mapunda ni msanii mkongwe asiejulikana yaani kitaalam tunaita famous unkown lakin msiba wake umekuwa mkubwa kama wa msanii mkubwa Tanzania.

Pia, soma: TANZIA - Muigizaji Grace Mapunda (Tessa) amefariki dunia

Mara ya kwanza naiona picha yake nikajiuliza nani huyu baada ya kuvuta picha ikaja picha yake.

Je, naye alikua anavaa suti nyeusi kwa siri kama mtangazaji wa Wasafi Mau Kikanga.

Maana wamekufa wasanii wengi lakini hakuna aliepewa nguvu kubwa na masikitiko mengi kama huyu

Pia soma: Chalamila ahimiza mfuko wa kwa ajili ya wasanii wa maigizo, Ofisi yake kutoa milioni 15
Itakuwa wewe ni wa juzi au sio mtu wa Bongo Entertainment
 
Hawa ni waigizaji wa aian hii ni wale tunaowaita ma-super star wa madada wa kazi. Hakuna watu wanaojitambua wanaongalia huo upuuzi wao.
Wanaume wengi tumechagua kuwa wapenzi wa kuangalia Mpira wakati huo wenzetu wa kike wamechagua kuangalia hizo tamthiliya.

Japo Siku hizi, imeanza kuwa kawaida Wanaume pia kuwa wapenzi wa tamthiliya za Azam
 
Misiba Mingi ya Wasanii inakuzwa kwa sababu walio hai hilo ndilo Eneo la kutafuta Kiki.

Hasa kuelekea Msimu wa Uchaguzi kama huu hata wasiomjua kama Chalamila na Shigongo nao watajitokeza kujizolea Umaarufu
Shigongo kasema alikuwa mwenza wake, wameishi wote mpaka mauti yanamkuta jukumu la wanae atalibeba yeye siku zote
 
Nimezaliwa na kuish kabla ya tv hazijaanza tv ya kwanza ilikua tvt na tvz

Ni kweli sijakataa lakin sio kwa ukubwa huo aliupata kwenye msiba wake kuna nini nyuma ya pazia maana kapata treatment kama kanumba mpaka rais wa nch anamlilia

Hapana nilianza mwaka 1990 enz za nba itv maiko jordan miziki ya rkelly tamthilia za ua jekundu tausi
Hizo ni hearsays tu

Yanaweza kuzungumzwa mengi kwenye huu Msiba, ila Idara ya Usalama imeingia Kila mahali kuanzia michezo/burudani/vyuoni/hospitali n.k

Lakini pia msisahau kwamba tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Chama tawala lazima kioneshe mshikamano na hilo kundi la Wasanii maana wamekuwa wakiwatumia Kila Mwaka wa Uchaguzi

Wanatumia ule usemi kwamba "akufaaye Kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli"
 
Back
Top Bottom