Kipindi Roy yupo G Record alikua anafanya kazi na G Square, G Square alikua anajifunza mambo mengi toka kwa Roy, nilitegemea G Square atakuja Ku hit bongo, ila kwa sasa sijui yuko wapi.
Kipindi G Record imeanza Gulu akiwa DJ na mtu anayejua Music lakini alikua hawezi kufanya Audio Production, na Roy akiwa Mtaalam wa Computer tu, aliyekua anaijua Computer nje ndani ila a hajui kitu kuhusu Codes, Beat na chochote kuhusu Audio Production, wakakubaliana kufanya kazi pamoja.
Gulu kwa uzoefu wake kuhusu Music anatoa idea, na Roy mtaalam wa Computer anafanya ionekana kupitia Computer, wakaanza kutengeneza Beat zenye makosa mengi, na kadri walivyokua wakifanya wakaanza Ku improve.
Mfano nyimbo ya Blue ilirudiwa zaidi ya Mara 3, yani inakamilika mixing, majaribio yao ilikua Bilicanas Club, wakiona ina sound mbovu wanarudi tena Studio kufanya Upya....
Namkumbuka Roy kama mtu poa sana, tatizo alipenda sana Pombe, ni mtu alikua anakesha anakunywa, kwake kulala ilikua Mchana, usiku kazi na Pombe....
Siku moja ananambia miaka michache ijayo Tanzania tutasimamisha aina moja ya Music ambapo popote ikisikika tu Beat watu watasema huu ni Music wa Tanzania, ila alikufa bila kushuhudia hilo....
Kipindi hicho Mr. Nice ndo Msanii mkubwa, hamadi Blue akatoka, akamtoa Roy, akaitoa G Record, kula Msanii akawa anataka kufanya kazi kwa Roy, kabla hawajaanza kula matunda yao, mdudu akaingia G Record, kukaanza kuwa na Wasanii wa Roy, na Wasanii wa Gulu, G Record ikavunjika, Roy akaanzisha G2......!
Dah!
Namkumbuka sana Mwana...
R.I.P Producer wangu!