Marehemu Roy alikuwa anajua sana

Marehemu Roy alikuwa anajua sana

Yah kaka na kuna ngoma kibao za mensen zina quality mbovu.
Kuna ile ngoma ya country boy ft linah ngoma nzuri ila production mbovu saaana yani saana nikitaka isikiliza uwa naipenda, inabidi niiskilize kwa sauti ya chini
Ndo hivyo ila ndo hivyo jamaa ametengeneza pesa sana
 
hawajapotea kwa kupenda.. enzi hizo visual lab tulikuwa tunamuona quality sababu watu walikuwa hawaendi god father au usa...

sasa diamond katufungua macho kwa kuona video quality na hii ikasababisha kina visual lab wakose wateja...

maana leo visual lab hata akaze vipi hana mtaji wa god father au capital dreams.. ambapo diamond anawatumia..

Game imechange sana kuanzia aina ya unaji studio za mziki mpaka videos.
Visual lab kapotea, nisher naye chalii, akina epidu walishawapoteza empty soulz, 2eyes, mwananchi production, benchmark production tayari
 
YH vivian tilya.
Unakumbuka ngoma kama siamini macho yangu ya matonya.
Nilikuwa naikubari mpaka basi
Chungwa ya sumalee
Mwache aende zake ya sumalee
Mimi wewe abby skills na mr blu. Hii ngoma blu alimpa abby skills baada ya kutaka mpa mapozi akaghairi akaimba yeye ndipo akampa mimi wewe.
+ Icecream ya Noorah.
 
tatizo hawakujiandaa na mabadiliko.. singeli nyimbo zinarekodiwa studio za sebuleni kwa mama zao.. ila wanapiga hela balaa... huku p funk au master jay anaumiza kichwa ila nyimbo haibambi wala kuleta faida

Kweli afadhali kajiongeza.
Toka pc ziwe bei chee na kudownload fl studio cubase na new handle basi vikaanza ibuka vistudio vya magheton kiasi kwamba kurekodi kukawa rahisi nyimbo za quality ndogo zikafunika za quality kubwa
 
tatizo hawakujiandaa na mabadiliko.. singeli nyimbo zinarekodiwa studio za sebuleni kwa mama zao.. ila wanapiga hela balaa... huku p funk au master jay anaumiza kichwa ila nyimbo haibambi wala kuleta faida
Pfink kuna kipindi alishindqa sima alama za nyakati akawa anatumia nguvu nyingu kurekodi ngoma lakini zilikuwa na mahadhi sana ya mbele nikajua haziwezi fika popote.
Kipindi kamleta q the don, yupo yeye alikuwepo na jamaa flani kama mmexico sijui
 
Hivi nini kilimtoa uhai Roy?
The man was talented na alipofariki naona mdogo wake enika naye mziki aliupa kisogo.
Yule dada anajua sana nikikumbuka ngoma yake ya baridi kama hii, nimekubamba sijakubamba, wimbo wa makamoa aliomshirikiaha enika wa baby please, nako2nako- hawatuwezi
Enzi hizo radio free iko on fire.. Yaani ikifika ijumaa unakaaa attention kusikia hizi ngoma kwenye top ten
 
hawajapotea kwa kupenda.. enzi hizo visual lab tulikuwa tunamuona quality sababu watu walikuwa hawaendi god father au usa...

sasa diamond katufungua macho kwa kuona video quality na hii ikasababisha kina visual lab wakose wateja...

maana leo visual lab hata akaze vipi hana mtaji wa god father au capital dreams.. ambapo diamond anawatumia..
Sina imani na ww,haya ni mahaba yako binafsi kwa huyo domo
 
Kuna ngoma moja ilikua inaitwa kizizi ya bablee,ule mdundo ni Kama mkono wa roy
 
Kuna ngoma moja ilikua inaitwa kizizi ya bablee,ule mdundo ni Kama mkono wa roy
 
tatizo hawakujiandaa na mabadiliko.. singeli nyimbo zinarekodiwa studio za sebuleni kwa mama zao.. ila wanapiga hela balaa... huku p funk au master jay anaumiza kichwa ila nyimbo haibambi wala kuleta faida
Jay na P ni kujitambua kulikowafanya waachane na bongoflava unamrekodia mtu single kwa laki 5 beat inakua yake then anapigia show moja million moja so wakawa wanataka mikataba ya kula asilimia kwenye shows na endorsements zingine iwapo nyimbo zitatumika
 
Kipindi Roy yupo G Record alikua anafanya kazi na G Square, G Square alikua anajifunza mambo mengi toka kwa Roy, nilitegemea G Square atakuja Ku hit bongo, ila kwa sasa sijui yuko wapi.

Kipindi G Record imeanza Gulu akiwa DJ na mtu anayejua Music lakini alikua hawezi kufanya Audio Production, na Roy akiwa Mtaalam wa Computer tu, aliyekua anaijua Computer nje ndani ila a hajui kitu kuhusu Codes, Beat na chochote kuhusu Audio Production, wakakubaliana kufanya kazi pamoja.

Gulu kwa uzoefu wake kuhusu Music anatoa idea, na Roy mtaalam wa Computer anafanya ionekana kupitia Computer, wakaanza kutengeneza Beat zenye makosa mengi, na kadri walivyokua wakifanya wakaanza Ku improve.

Mfano nyimbo ya Blue ilirudiwa zaidi ya Mara 3, yani inakamilika mixing, majaribio yao ilikua Bilicanas Club, wakiona ina sound mbovu wanarudi tena Studio kufanya Upya....

Namkumbuka Roy kama mtu poa sana, tatizo alipenda sana Pombe, ni mtu alikua anakesha anakunywa, kwake kulala ilikua Mchana, usiku kazi na Pombe....

Siku moja ananambia miaka michache ijayo Tanzania tutasimamisha aina moja ya Music ambapo popote ikisikika tu Beat watu watasema huu ni Music wa Tanzania, ila alikufa bila kushuhudia hilo....

Kipindi hicho Mr. Nice ndo Msanii mkubwa, hamadi Blue akatoka, akamtoa Roy, akaitoa G Record, kula Msanii akawa anataka kufanya kazi kwa Roy, kabla hawajaanza kula matunda yao, mdudu akaingia G Record, kukaanza kuwa na Wasanii wa Roy, na Wasanii wa Gulu, G Record ikavunjika, Roy akaanzisha G2......!

Dah!
Namkumbuka sana Mwana...
R.I.P Producer wangu!
 
Back
Top Bottom