Marekani anatoa misaada kiduchu hataki Ukraine ashindwe wala kushinda sana, anataka vita iwe ndefu ili kumfanyia utafiti Urusi na Ukraine awe mdaiwa



Mwisho wa yote zitatumika Nuclear.
 
Wengi sana tunaoitetea Ukraine humu ndani tunaonekana tunasapoti Ushoga, Tunaiona US ndo kila kitu n.k

Mimi nipo JF kitambo saana, ID hii nimeanza itumia toka 2011. Humu ndani kipindi cha nyuma nilikuwa nakandia saana US kuvunja amani mataifa mengine hasa hasa LIBYA.

Lakini hii haikunifanya nisapoti Russia kwa kuvamia Ukraine, ninaona ni kama Ukraine ananyimwa haki yake ya kuchagua kile anachokitaka. Hata US angevamia nchi yoyote bado nsingeunga mkono.

Kuwa neutral ni jambo zuri mno.

Ongera sana mkuu.
 
Nikiweza nitafuatilia hoja zako za huko nyuma mkuu maana hapa kwa namna ulivyojibu tu nimeona wewe sio mbuyu kuwa ukishasimikwa ardhini unakaa hapo hapo na kukubaliana na jua mvua vumbi n.k Inaonekana Upo huru haufungwi na uchawa.
 
Nikiweza nitafuatilia hoja zako za huko nyuma mkuu maana hapa kwa namna ulivyojibu tu nimeona wewe sio mbuyu kuwa ukishasimikwa ardhini unakaa hapo hapo na kukubaliana na jua mvua vumbi n.k Inaonekana Upo huru haufungwi na uchawa.
Miaka ya nyuma kuna thread humu ilikuwa inahusu silaha ya s300 defenc system, kuna s18 balistic missiles, tulichangia mno na kuisifia Russia, tukasema ndio mbabe wa magharibi.

Kuna special thread inayohusu hiyo s300 ila jina silikumbuka, ina posts zaidi ya 2,000. Kipindi hiko Jukwaa hili kuna jamaa anaitwa Elungata, naona sasa hivi atakuwa amebadili ID. Huyu Bukyanagandi alikuwepo kipindi hiko. Anaweza akaja akathibitisha hili, jamaa huyu ni pro russia toka kipindi hiko JF. Huu mpambano wa vita wa sasa yeye kuwa Pro Russia hata sio kitu cha ajabu.
 
Reactions: Tsh
Unaweza kua sahihi. West wanaakili sana

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mambo mengine huwa atuyasemi - FYI,mimi ni mwandisi(Engineer) niliyesoma vyuo vikuu vya Ulaya magharibi,nimefanya kazi na kuishi huko,masomo yangu na fedha za kujikimu pamoja na nauli ya ndege kwenda na kurudi nyumbani wakati wa likizo nikiwa masomoni nilikiwa nalipiwa na Serikali yao kutoka kwa fedha za walipa kodi wa taifa husika,nakumbuka vizuri walicho nishauri in privacy nifanye iwapo ntarudi nyumbani nikihitimu masomo - so I know these people modus operandi like back of my hand - si watu wema hata kidogo.

Msione si support matakwa yao ya kutaka kuitawala Dunia kinguvu kwa kutumia mbinu mbali mbali zikiwemo overt and covert tactics mkafikiri labda nasukumwa na chuki binafsi, hii si kweli hata kidogo.

Watu hawajui tu, hata mgogoro huu wa Ukraine ulisukwa vizuri siku nyingi tu na mataifa hayo hayo ya magharibi specifically US, walicho kuwa wanasubiri ni opportune time ya kuitumia Ukraine ipigane a proxy war kwa niaba ya US, lengo hasa ni kutaka kuisambaratisha Urusi in totality making sure she will never rise again to challenge the US militarily and Global influence, nikiona Biden ana shed crocodile tears namshangaa sana sana kwa kujitia ni mtetezi mkubwa wa Taifa la Ukraine na Raia wake - ulaghai mtupu, interest zake na wapambe wake zimejikita kwenye kuzitafutia soko kampuni za Merikani zinazo unda silaha, pili battlefield ya kufanyia majaribio ya silaha mpya za Merikani dhiidi ya defense systems za Urusi ili kukitokea vita baina ya Urusi na NATO wajue lipi la kufanya, la tatu ni kutumia kisingizio cha vita ya Ukraine kushiniki Bunge liidhinishe fedha fasta lakini kiasi alisi cha fedha zinazo kwenda Ukraine ni kidogo fedha nyingine zinaishia mifukoni mwa Biden,rafiki zake na wamiliki wa viwanda vya kuunda silaha (MIC)-kumbukeni mwanae wa Kiume wa Rais Biden aliwahi uajiriwa kwenye Serikali ya Ukraine kama mshauri mkuu wa Rais, vile vile alimilikishwa makumpuni ya mafuta na gesi ya huko Ukraine wakati baba yake akiwa ni makamu wa Rais Obama -hii inadhilisha wazi wazi kwamba familia ya Biden ina vested interest kwenye Taifa la Ukraine si ajabu ndio maana saula la Ukraine amelivalia njuga kweli kweli!!

Back to the main point - ushindani baina ya US na Russia, si ushindani tu bali na uadui hivyo vyote vipo deep seated kabisa, actually as far as western leaders specifically the US are concern cold war did not end in 1990s it is still on going in other words still alive and kicking!!! Next time ntaeleza kwa kina sababu zangu za kui-support Urusi.
 
Siyo tumekatwa vichwa tunaangalia kwa ukaribu saaana kinachoendelea huko!!!NATO ni bingwa wa propaganda km mjuavyo hii nayo ni siraha kali sana ya kumshinda adui!

ni ngumu kumuua jenerali wa kirusi!! NATO hata wakifa woote wataonyesha kuwa hao ni warusi! ndo tabia yao!...unadhania NATO wao watasemaje zaidi ya huo uongo!
 
Putin alijazwa akajaa sasa ndio anaanza kugundua mtego alioingia kibaya ni kujitoa anaona aibu.
China walijua hilo wakakwepa mtego
Ziara ya spika wa bunge la Marekani aliyeingia kimabavu Taiwani kutembelea wachina wakaweka mkwara lakini wakashtuka kuanzisha vita wakajua ya Urusi yatawakuta!! Mali zote za wachina nje kutaifisha nk wakaamua kuwa wapole sababu uchumi wa China kwa sasa unategemea dola zaidi na wao ndio wakopeshaji wakubwa wa Serikali ya Marekani!! Wakaona pesa itayeyuka hewani mchana kweupe!! Wakarudisha majeshi nyuma kutoshambulia Taiwani

Humu mmojawapo mimi nilitamka wazi kuwa Putin Bwege hadi ma moderators humu walifuta nyuzi zangu zilizokuwa na comment mwanzo kabisa wa vita za kusema kuwa Putin ,Hopeless na bwege hakufanya analysis ya kutosha kabla kujitosa hiyo vita na Ukraine!! Sasa hivi ushahidi kuwa.Putin hakuwa na akili kuanzisha hiyo vita uko wazi
 
Kwa taarifa yako Ukraine hakopi kupigana vita nafikiri hufuatilii pesa na misaada ya kivita bunge la Marekani linapoindhinisha linatamka wazi kuwa ni msaada

Uwe unafuatililia wanatoa nini.na wanachotoa ni msaada au mkopo? Mleta mada umeandika utoto
 
Huwezi kusema marekani inatoa msaada kiduchu!! Mpaka sasa marekani imeshatoa zaidi ya dola bilioni 60!! Huo ni msaada kiduchu!!! Ni zaidi ya bajeti ya Tanzania kwa miaka mitatu!! Halafu bila aibu unasema ni msaada kiduchu!!!
Hizo pesa silaha bado halafu mtu anaita kiduchu

Kombora moja la Himars la masafa marefu na Laucher yake ni dola milioni sita na laki tano sawa na shilingi bilioni 13 za Tanzania

Marekani imewapa Ukraine makombora ya Himars kibao ukichukulia kombora moja gharama yake sawa na shilingi za kitanzania bilioni 13 bado mtu ataita msaada kiduchu? Akili anakuwa hana
 
Ni kweli kulikuwa hamna dalili zozote zile Putin kushinda Ukraine ili hali mataifa ya Magharibi G7, Canada pamoja na US wapo na Ukraine. Sasa tayari wameshaanza kuijenga Ukraine kwa mabillion ya dola yanayomiminika kila siku.

Silaha za watu wa Magharibi na US ni balaa, itoshe kusema tu kwamba Ukraine anapimiwa silaha, zile ambazo wanaona zinaweza kumsabaratisha kwa haraka hawazitumii ili kwanza kumdhoofisha na kumsogeza kwenye meza ya mazungumzo ya amani akiwa hoi.

Technologia na Silaha za viwango vya juu duniani inamilikiwa na US pamoja na mshirika wake wa karibu Israel.

Pole kwa Putin, maana wanakwenda kuichukua na CRIMEA - recording maneno yangu leo tarehe 12/09/22
 
Hii nakubali mkuu, moja ya watu mliojitokeza hadharani kutamka wazi wazi ni wewe pamoja na nyamizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…