Marekani: Apigwa risasi baada ya kugonga mlango usio sahihi

Marekani: Apigwa risasi baada ya kugonga mlango usio sahihi

Bila huu ushenzi wa kupigana risasi ovyo, Marekani ni nchi nzuri sana kuishi
Serikali yao inapaswa kuifanyia kazi sheria inayoruhusu raia kumiliki risasi. Mzee mwenye msongo wa mawazo kama huyu, hapaswi kuruhusiwa kumiliki pistol
 

Maandamano yalizuka katika Jiji la Kansas, Missouri, mwishoni mwa juma baada ya mwenye nyumba kumpiga risasi mbili kijana mweusi ambaye aligonga kengele ya mlango wao kimakosa.

Ralph Yarl mwenye umri wa miaka 16, alitumwa na wazazi wake kuwachukua kaka zake kutoka katika nyumba ya rafiki yao mnamo tarehe 13 Aprili, lakini akaenda kwa anwani isiyo sahihi.

Mshukiwa alimpiga risasi Bw. Yarl akiwa katika mlango wake.

Kijana huyo alipiga risasi moja kichwani, imesema familia yake na mawakili wao.

Polisi imemwachia huru mtu aliyefyatua risasi kutoka kizuizini lakini hawajawatambua. Bw Yarl aliruhusiwa kutoka hospitalini Jumapili na anaendelea kupata nafuu akiwa nyumbani na familia yake, baba yake Paul Yarl aliliambia gazeti la Kansas City Star.

"Anaendelea kuimarika," baba yake aliliambia gazeti."

Mawakili mashuhuri wa haki za kiraia Ben Crump na Lee Merritt wanawakilisha familia ya Bw Yarl katika kesi hiyo. Waliwakosoa maafisa kwa kumwachilia huru mshukiwa, ambaye wanasema ni mwanaume mzungu.

"Huwezi tu kuwapiga watu risasi bila sababu kisa mtu anapokuja kugonga mlango wako - na kugonga mlango wako sio kosa. Huyu jamaa anapaswa kushtakiwa,"Bw Crump alisema.

CHANZO: BBC
Aseee! Maisha ya USA ni ya kibabe sana baadhi ya sehemu
 
Huyu ni Ghost kabisa...[emoji83][emoji49][emoji48][emoji84]
FB_IMG_1681800454286.jpg
 
Jamaa mwenyewe aliyempiga dogo ndio huyo hapo kwenye picha kushoto

View attachment 2591680
Hili zee lililompiga risasi huyo Bwana Mdogo, nalifananisha sana na zee moja la kuitwa "Don Emilio" kwenye tamthilia moja ya Kifilipino. Ila anaonekana hayuko timamu.

Mwenyezi AmsimamiebBwana Mdogo apate kurudia Utimamu wake wa mwili na Akili...Amina.
 
Back
Top Bottom