Marekani: Donald Trump ajeruhiwa kwa risasi akihutubia mkutano wa hadhara

Marekani: Donald Trump ajeruhiwa kwa risasi akihutubia mkutano wa hadhara

Ulitaka wafike faster kabla ya risasi? Yaani washindane mbio na risasi? Tafsiri yako kuhusu ulinzi mkali ni ipi? Au kwako ulinzi mkali ni ramli?
ulinzi mkali ni kuzuia kabla, i mean amewezaje kufika eneo hilo akiwa na siraha ya udunguaji pia kabla trump hajainama yani ku take action ye mwenyewe zimepita risasi kadhaa mpaka iliyompata sikio na walinzi walikuwa hawajafika!. pia inasemekana kuna mtu aliwaambia kwenye hilo jengo alikuwepo mtu anasiraha na hawakutake action huoni kuna upungufu hapo!..

totally kilichotokea ni bahati tu kwa trump kupona na sio kwamba ulinzi ulifanya kitu!, hiyo risasi iliyomchuna sikio ingekuwa imempata kwenye paji la uso tungekuwa tunazungumzia kitu chengine hapa!.. ulinzi wakulinda viongozi hautegemei adui afanye kosa ndo kiongozi apone! kama na hapa haujaelewa hiyo itakuwa ni shughuli yako sasa mi nishakuelewesha.
 
Tunapoelekea ulinzi wa viongozi wengi duniani utakuwa mdogo sana maana maarifa yameongezeka na watu wamebadilika sana mfano tukio kama hili huenda kukawa na watu kadhaa kwenye circle ya ulinzi wamehusika
Ni kweli kabisa secret service wamechelewa mno kufika kama sio Juhudi za trump mwenyewe kuinama huenda angekula risasi au kama muuaji angetumia kilipuzi kikubwa zaidi huenda madhara yangekuwa makubwa
Lakini namna ameondoka ilikuwa kama wanafanya jaribio la kuokoa mbishi hata kuinama ndani ya shield ye anatoa mkono awe che Guevara
hata hivyo historia yao inawatafuna viongozi wao wakuu mara kadhaa wamekuwa wakishambuliwa si jana si leo!
 
Assassins wa siku hizi ni wajinga wajinga hasa... nilishangaa ishu ya Sativa kushindw kudedishwa. Hata huko USA pia sniper kashindwa kumdondosha mtu ambaye alikuwa hana movement yoyote ile.. (Static position).

Ok umemkosa, na watu (Walinzi) wamekuja kufanya Covering. Why usitumie heavy guns kupenetrate bullet from one body to another..?

Inasifika USA wana highend tools why mlio wa risasi usikike? Hakuna stealth mechanism iliyotumika (kiwambo)?

Or ni warning tu hawakutaka kumuua?
Nadhan Kuna lengo la kuua na lengo la kumfundisha adabu, huyo saliva au Lissu wote lengo lilikuwa n kufundishwa adabu tuu na sio kuuawa, na naamini ht Trump nae lengo sio kuuawa, yn serikali ya USA na uwezo wake wa jeshi lishindwe kuna na sniper wa kumuondoa trump kweli?
 
Marekani kumbe hamna usalama ni majingambo tu ya kwenye sinema.
Amerika siyo salama. Kule ukimletea mtu za kuleta unakula "shaba".

Ndiyo taifa linaloongoza kwa raia wake kuuana kwa risasi kuliko taifa lolote duniani.
 
Siasa za Marekani sasa zinaanza kufuata njia za bara la Afrika.
Walitubeza kiasi cha kutosha, nao wanaingia kwenye aibu.
We jamaa wewe itakuwa siasa za marekani huzijui. Tafuta muda some American Hostory, kwa habari yako Trump sio wa kwanza kushambuliwa kwa risasi, wapo marais wa Marekani walioshambuliwa kwenye mikutano yao. Tanzania hatujafikia viongozi kuwa attempted kwa risasi kwenye mikutano yao zaidi ya kuwashugurikia watu wanaokosoa wenye mamlaka. Ikifika huko bhasi mkuu jua tupo kwenye viwango vikubwa vya political intolerance.
 
Bado haijajulikana kuwa damu zinazotiririka kutoka usoni ni sababu ya risasi au kuanguka chini ameondolewa akiwa mzima huku akiinua mkono kusalimia na kuaga akiwa anavuja damu usoni

Itakuwa ni baada ya kupalazwa na risasi maana kabla hajatake cover aliinua mkono wake kugusa sikio lake, kisha akatazama mkono kabla hajajilaza chini kwa haraka...
 
Hawa wapuuzi Marekani wanatakiwa kuja kujifunza siasa Tanzania, Taifa lina miaka zaidi ya 300 bado wanaviaziana kuuwana wakati Tanzania Taifa lina miaka 60 tu Wanasiasa wanakunywa Juice Ikulu.
Aaa wapi...wapuuzi ni POLISI wa CCM jombaa....tukio kama hilo wangefika wakarusha mabomu ya machozi na kisha kudondosha pale bendera ya CHADEMA....Halafu ungesikilizia sasa hilo tamuko la IGP siyo RPC tena mbele ya vyombo vya habari......
 
Hawawezi kumshinda kwa kura!

Wamejaribu lawfare, nayo imeshindikana.

Sasa wanataka kumuua!

Democraps.
Kwa yanayo endelea pale Ukraine, chama cha Democrats na NATO nzima zinaona Trump nihatari sana kushika madaraka haswa kwa kipindi hiki..
Kwao nihasara kubwa kusimamisha vita pale Ukraine, Trump akishinda uraisi hakutakuwa na vita tena Ukraine, lengo kuu la NATO ni kuanzisha vita ya 3 ya Dunia
 
Back
Top Bottom