Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Timu ya wataalam kutoka Hospitali ya Changzheng ya Shanghai, China, ikishirikiana na Akdemia ya Sayansi ya China hivi karibuni walitumia seli za shina kuunda upya mfumo wa insulini mwilini, na kufanikiwa kumponya mgonjwa wa kisukari mwenye umri wa miaka 59, ambaye anatarajiwa kuacha kabisa kutumia tena dawa ya insulini. Teknolojia hii imeleta matumaini mazuri kwa zaidi ya wagonjwa milioni 500 duniani.
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba, badala ya kuipongeza China kwa kubuni teknolojia hiyo nzuri, Marekani huenda itaiwekea China vikwazo. Ni kwa nini Marekani haipendi teknolojia hiyo inayoweza kunufaisha watu wengi duniani? Sababu ni rahisi, ni kwamba teknolojia hiyo itatishia maslahi ya kampuni kubwa za dawa nchini humo.
Takwimu zinaonesha kuwa nchini Marekani kuna takriban wagonjwa milioni 34 wa kisukari, na kati yao wengi wanategemea dawa za insulini kuishi maisha ya kawaida, hata kuokoa maisha yao. Lakini bei ya dawa hizo ni ghali sana, na chupa moja ya insulini nchini Marekani hugharimu zaidi ya dola 200 za Kimarekani. Katika miaka 40 iliyopita, bei ya insulini katika soko la Marekani imeongezeka kwa kasi kubwa. Tangu mwaka 1984, bei za bidhaa za kawaida nchini Marekani zimeongezeka zaidi ya mara mbili tu, lakini bei ya insulini imepanda karibu mara 14. Hata hivyo, gharama ya uzalishaji wa dawa hizo haijaongezeka sana. Kulingana na ripoti iliyotolewa mapema mwaka huu na Shirikisho la Udaktari nchini Marekani, gharama ya uzalishaji wa chupa moja ya insulini ni dola kadhaa tu za Kimarekani. Kwa Wagonjwa wa kawaida gharama ya matibabu ya ugonjwa wa kisukari inachukua karibu asilimia 10 ya kipato chao kila mwezi. Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris aliwahi kusema Mmarekani mmoja kati ya wanne walio na ugonjwa wa kisukari hawezi kumudu dawa za matibabu.
Nchini Marekani dawa za insulini zinadhibitiwa na kampuni tatu kubwa ya dawa, yaani Eli Lilly, Novo Nordisk, na Sanofi, ambazo zinapata faida kubwa mno kutokana na wagonjwa wa kisukari. Lakini teknolojia mpya ya China inatarajiwa kuponya kabisa wagonjwa wa kisukari, na baadaye hawatahitaji dawa za insulini tena, hali ambayo italeta hasara kubwa kwa kampuni hizo. Hivyo sasa zinahangaika kuishawishi serikali ya Marekani kuiwekea China vikwazo, ili kuzuia teknolojia hiyo kuingia nchini humo.
Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imeweka vikwazo dhidi ya China mara kwa mara ili kulinda maslahi ya mabepari wakubwa, huku ikipuuza maslahi ya watu wa kawaida. Hivi sasa kiwango cha mfumuko wa bei nchini Marekani kimeendelea kuwa cha juu, na kuleta maumivu makubwa kwa maisha ya watu. Licha ya utoaji wa fedha kwa wingi kupita kiasi, kuongeza ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za China, na kuiwekea China vikwazo mbalimbali pia ni sababu muhimu ya kuongezeka kwa mfumuko mkubwa wa bei.