Marekani imedhamiria kuitoa Huawei sokoni, imeituhumu kuwa ni tawi la jeshi la China

Marekani imedhamiria kuitoa Huawei sokoni, imeituhumu kuwa ni tawi la jeshi la China

Wewe mambo ya kitalaam unaleta siasa?!
MKUU siasa hapo imekaa wapi ?!
Mbna nimeleta ishu ambazo zipo wazi kabisa hem tuekane sawa hapo MKUU siasa iko wapi ili niirekebishe

Niko tayr kurekebishika mzee kaka kweli nimeleta siasa.....
 
Chip making ni moja ya teknolojia ambazo ndizo habari ya mjini kwa sasa na ndicho kitu mojawapo kinachoisumbua China hivi sasa pamoja na jitihada ilizozifikia.

Katika kuzalisha chips za kisasa zaidi hivi sasa hasa za kiwango cha nanometa saba (7) na kuendelea kunahitajika teknolojia ya juu sana ambayo China mpaka hivi sasa bado haijafika huko. Kuna kampuni nyingi zenye kuzalisha chips lakini kuna viwango fulani ambavyo ni world class.

Mfano, kuna teknolojia kama vile Extreme Ultraviolet Lithography (EUVL) na miundombinu zake. Mwenye teknolojia hii hivi sasa ndiye anayeutawala ulimwengu wa kisasa wa chip designing, teknolojia ambayo ni advanced sana, China bado haijaifikia.

Tumekuwa na chips za viwango vya nanometa 7 na hivi karibuni tumeingia sasa katika 5nm chips zenye performance kubwa zaidi ambapo uzalishaji wake umeanza mwaka huu. Kampuni kama vile Intel, Samsung pamoja na TSMC tayari zimekuwa katika uwekezaji wake muda mrefu na miaka michache baadaye tutafikia nanometa 3. Teknolojia inazidi kukua haraka sana.

Kampuni kubwa za uzalishaji wa semi-conductor equipments, EUVL materials n.k. ni za kimagharibi na kupata access ya tech zao ni kuingia mikataba ya kupata leseni za kuzalisha ama kuzinunua. China ni mnunuzi mzuri wa teknolojia za wengine hasa kutoka nchi za magharibi na kutokana na vikwazo kadha wa kadha ni wazi kuwa China itaathirika.
 
Kampuni nyingi tu zinalipana mirahaba. Mirahaba hiyo ni sehemu ndogo sana ya Huawei. Ukisoma hiyo habari Huawei imepokea mrahaba wa $1.4B huku imelipa $6B. Unaweza kuona tofauti.
Mkuu ni 6m sio b, hiyo mirahaba inatokana na nini unahisi?
 
Hawajaelewa kua US anazilenga non US companies ambazo zinatumia teknolojia yake.

Mkono mkubwa wa USA haukwepeki.
Ilikua zamani sio sasa MKUU wameukwepa INDIA wakaukwepa SOUTH KOREA wakaukwepa CHINA wakaukwepa RUSSIA kupitia kunua mafuta ya IRAN licha yavikwazo walivyoekewa IRAN juzi hapa tukaona VENEZUELA wamepokea mafuta toka IRAN licha yavikwazo walonavyo IRAN.....
 
Ukiwaletea data kama hizo wanakwambia ni CCP propaganda eti...[emoji2][emoji2][emoji2]
China has successfully put into orbit the final satellite in its BeiDou-3 navigation system, further advancing the country as a major power in space.

Tuesday's launch will allow China to no longer rely on the US government-owned Global Positioning System (GPS).

The $10bn (£8bn) network is made up of 35 satellites and provides global navigation coverage.
_113042815_gettyimages-1221997703-1.jpg

Mdogo mdogo Us atabaki na technology zake! China itakapo jiondoa kwenye GPS na kuanza kutumia yake na wadau wake!
 
Nikiona haya mambo ya ubabe wa USA,harafu kuna wajinga wanovaa za kijani,wanafikiri unaweza kuivimbia USA na wenzake wa magharibi,kama China anakimbizwa mchakamchaka,sembuse sie,ambao licha ya kuwa na maji ya kutosha,hatujaweza hata kuzalisha ngano ya kututosha,
✓Waafrika mahindi yalishaaribu vichwa vyetu akili zimebaki za kushindia Facebook na Instagram
 
USA wako overrated kwa maoni yangu hivi sasa. Technology imekuwa sana na mataifa mengi yanaweza kuishi bila kutegemea USA. Tatizo kubwa walimweka Trump kufikiri kwamba dunia ni ile ile ya zamani. Angalia mataifa yanayopiga hatua hivi sasa yako mengi tu na hakuna taifa linalopiga hatua ambalo halipingwi na USA na washiriki wake. Kuanzia the tigers group, India, Nigeria, Ethiopia, Tanzania, na Southern American Countries (Mexico, Brazil, Uruguay etc.)

USA na washiriki wake wanajidanganya, miaka 10 ijayo ulimwengu unarudi kutumia Gold kama exchange mechanism ya pesa kwenye mataifa kuondokana na ulaghai wa nchi za magharibi.
 
China has successfully put into orbit the final satellite in its BeiDou-3 navigation system, further advancing the country as a major power in space.

Tuesday's launch will allow China to no longer rely on the US government-owned Global Positioning System (GPS).

The $10bn (£8bn) network is made up of 35 satellites and provides global navigation coverage.
View attachment 1489395
Mdogo mdogo Us atabaki na technology zake! China itakapo jiondoa kwenye GPS na kuanza kutumia yake na wadau wake!
Naam mambo mdogo mdogo mzee....
 
USA wako overrated kwa maoni yangu hivi sasa. Technology imekuwa sana na mataifa mengi yanaweza kuishi bila kutegemea USA. Tatizo kubwa walimweka Trump kufikiri kwamba dunia ni ile ile ya zamani. Angalia mataifa yanayopiga hatua hivi sasa yako mengi tu na hakuna taifa linalopiga hatua ambalo halipingwi na USA na washiriki wake. Kuanzia the tigers group, India, Nigeria, Ethiopia, Tanzania, na Southern American Countries (Mexico, Brazil, Uruguay etc.)

USA na washiriki wake wanajidanganya, miaka 10 ijayo ulimwengu unarudi kutumia Gold kama exchange mechanism ya pesa kwenye mataifa kuondokana na ulaghai wa nchi za magharibi.
facts.....
 
Huawei ilikua inakuja vizuri sana kwa miaka 3 iliyopita. Ghafla bin vuu mwaka jana ikawekwa kwenye black list ya serikali ya Marekani ikaanza kupambana na vikwazo.

Sasa Huawei imeanza kupoteza hata ile miradi na mikataba iliyokua imepata ya kufunga mitambo ya 5G. Uingereza iliipa Huawei ila sasa imebadilisha msimamo, inategemewa hivyo hivyo kwa Hispania, na nchi kadhaa kubwa Ulaya kujiondoa kwenye mikataba na Huawei.

Uingereza inasema ni kwa sababu ya vikwazo vipya vinavyotegemewa kutangazwa September, Huawei haitakua na uwezo wowote wa hata kuzalisha vifaa vinavyohitajika sio kwa 5G wala kwa simu zake zote kwa sababu haitakua na uwezo wa kutengeneza chip yake ya Krin.

Sababu ni moja kubwa, teknolojia ya kisasa zaidi inayotumika kuzalisha vifaa vya 5G au chip za simu 90% ina mkono wa Marekani. Kwa sasa Huawei hupata baadhi ya teknolojia kwa kibali maalumu cha serikali ya Marekani. Inategemewa kuanzia September hali inaweza kua mbaya zaidi kwa Huawei.

Marekani imebadilisha tuhuma kwa Huawei kua ni tawi la jeshi la China hivyo itakabiliwa na vikwazo vyote vinavyohusu jeshi la China.

Why Huawei's days in the UK could be numbered

Huawei wangeweza kuwatangulia US kwenye biashara ya 5G network, wange dominate future yake kwa kiasi kikubwa. US anajaribu kumfungia China kwenye jengo lisilopitisha hewa. Wachina wako wengi. Ni ngumu sana kuwamaliza kwa uharaka
 
Back
Top Bottom