Marekani imehusika kwa kiwango cha kutosha kabisa katika kuisaidia Israel kuitandika Iran

Sasa nimeanza kuelewa kwa nini Putin anamsanifu Trump.

Imagine Marekani nayo ianze kuishambulia Iran, Trump atapata wapi moral authority ya kutaka kuumaliza mgogoro wa Ukraine?
 
Iran hakujifunza kilichompata Gaddafi kwakuamini kuwa upande wa Russia itamsaidia asishambuliwe na west. Hakujua kuwa hawa jamaa wana common interest Ila wanatofautina mechanism tuu.
 
Sasa nimeanza kuelewa kwa nini Putin anamsanifu Trump.

Imagine Marekani nayo ianze kuishambulia Iran, Trump atapata wapi moral authority ya kutaka kuumaliza mgogoro wa Ukraine?
Wala hamsanifu,hapo wamegawana ndio maana Trump aliwaambia Ukraine kuwa swala la kurudishiwa ardhi asahau.
 
Bi kweli
 
Kinachomsumbua mzee Nyani Ngabu ni chuki alizo nazo na Israel lakini chuki zake hazitazuia kichapo, shukurani kwa Trump aliyeizuia Israel asiondoke na kichwa cha Ayatollah,Iran ndiyoinayosaidiwa na Marekani kwa kuifunga seeped governor Israel vinginevyo mambo yangekuwa tofauti.
 
Msitake kumung'unya maneno.
Iran alizidiwa akili na Israel kama ambavyo Hezbollah alizidiwa akili. Wao kichwani hamna kitu, badala yake wakawa wanajaza masilaha mazito mazito ya missile.
US yes amewasaidia Israel kwa intelligence na intercepting the heavy barrages of missiles. Lakini ujue kule Iran yuko na China, Russia na North Korea unataka kusema hawakumsaidia? Uongo bali wamezidiwa maarifa.
Kingine nikwambie wewe na ninafikiri wewe siyo ISLAMIST. Lengo la ISLAMISTS la kufutilia mbali Israel yenye historia ya mwanae yesu kuwepo hapa duniani, Mungu wa Biblia hawezi liruhusu. Nyinyi hajui ni kwanini Kukatokea Regime change kule Syria tena ikichochewa na adui wa Israel- Turkey. Kuondoka kwa Assad kukafanya Israel awe na NJIA nyeupe ya kupitisha NDEGE zake kwenda kushambulia Iran.
Sasa NIKWAMBIE KITU? Kuanguka kwa Ayatollah Khamenei huenda kukaleta Anguko la PUTIN KULE RUSSIA. Mark my words. Kwa sababu Putin naye ni kikwazo kwa Amani ya Dunia na amekuwa akiwatesa watu wa Mungu wa Biblia. Utakumbuka maneno yangu kama vile tuliwaambia humu JF kuwa the fact that Iran has Theocratic Government inapingana na unabii wa Biblia
 
Kama makombora ya Iran yataendelea kutua Tel- Aviv na kuongeza madhara basi shinikizo la ndani kwa Netanyau kusimamisha hii vita haliepukiki.

Ila kiasi Fulani haya mashambulizi ni ngumu kwa Sasa kusema kama yatahitimisha kabisa mpango wa nyuklia wa Iran, labda 'assesment' ikifanyika baada ya mzozo kusimamia itajibu hilo.

Mossad kwa sasa imejitahidi kujipenyeza Iran.

T14 Armata
 
Duh....hivi unajua vifaa vingi vya kivita Iran anatumia vya USA na Russia?....ndege za kivita karibia zote za Iran alinunua USA miaka 40 iliyopita, kuna ambazo alinunua Russia, Vifaa vya kulinda Anga vyote kanunua Russia.
 
No! no. Nyani Ngabu hana chuki na Israel. Tazama kinachotokea Tel Aviv na Haifa ! Dunia nzima ipo kimya na kwa siri wanashangilia. Si kwasababu wanaichukia Israel, bali Israel imevuka mipaka yote ya Jumuiya ya Kimataifa. Kabla sijakueleza hayo, fikiria Brazil na S.Africa zinailani Israel. Brazili!

1. Israel ilishambulia Ubalozi wa Iran Syria na kuua maafisa wa Ubalozi. Anaglifanya hivyo mwingine angeitwa Gaidi.
2. Israel ikamuua Mkuu wa shughuli za Nyuklia za Iran. Siyo mmoja ni wengi. Dunia kimya, angelikuwa mwingine angeitwa Gaidi
3. Israel imeshambulia Iran, kwanza, kuua wanasayansi, makamanda na mabomu ya vinu ya nyuklia

Ulitegemea Iran ifanye nini baada ya hayo

4. Israel ina silaha za nyuklia, hazikaguliwi na chombo chochote kile. Nani alitoa kibali
5. Tazama Gaza, wanakusanya watu wenye njaa kisha kuwapiga mabomu waki wa rekodi na kucheka, unadhani dunia haioni

Hamas walipopiga Israel, nchi za magharibi zilisimama na Israel. Katika hili kila mtu anaona ni ''too much''

Ukitaka kuonyesha chuki ya Nyani Ngabu, chukua point zake then debunk them halafu tuonyeshe chuki.
Hisia zako haziwezi kuwa chuki. Please vijana wa Tanzania, jifunzeni mijadala
 
Hivi Matokeo ya Hivi vita Mshindi alikuwa niNani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…