Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Ukraine na Ulaya wamejifunza kwa uchungu sana, Marekani yawakataa

Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Ukraine na Ulaya wamejifunza kwa uchungu sana, Marekani yawakataa

Ni wakati wa nchi za Ulaya kuwa na ushirikiano na China na Russia dunia ya sasa inahitaji win-win cooperation sio sera za Marekani za win-lose cooperation

Tatizo la nchi za Ulaya zimekubali kuwa U.S vassal states, wamekubali internal na foreign policies zao zitegemee sera za Marekani wanaumia sana, ndicho anachopitia Japan, South Korea, Canada, Australia na U.S vassal states nyingine.

Leo uchumi wa Ujerumani unaotegemea viwanda, uzalishaji viwandani umeporomoka kwa sababu ya kupanda kwa gharama za nishati ambazo awali walikuwa wananunua Urusi kwa bei rahisi, Marekani akalipua Nord Stream pipeline ili awauzie LNG kwa bei kubwa

Mafuta wanauziwa na India ambayo nayo inanunua Urusi na kuwauzia kama third party kwa gharama kubwa

Na bado Marekani inawatisha kwa kuwapandishia tariffs bidhaa zao.

Mchina aliona mbali kafanya juu chini kuhakikisha kuwa soko lake kubwa la bidhaa lisitegemee Marekani, kwa sasa soko kubwa la China ni Global South countries.

Ukiwa trade partner mkubwa wa Marekani lazima akutese sana kama Canada, Mexico na Japan zinavyoteswa na tariffs.

Siku hizi Mchina anafanya tit for tat Marekani akitia tariffs na yeye anampandishia tariffs kwa sababu soko la Marekani sio kipaumbele kwake.

Marekani ni kwenda naye kibabe kama Urusi na China zinavyofanya
Wewe kijana wewe acha basi,hebu punguza madini,mtu unatema madini Hadi najisikia kama natembea juu ya maji😄
 
We are strong together than alone.

Ukraine inahitaji support ya kila aina kutoka Nchi wananchama wa NATO, kama Marekani imekataa kwa sababu zake za siasa za ndani, basi wanachama waliobaki wajipange au waunde ummoja mpya na wamkaribishe mwenzao wakimuacha wanamkaanga.

Acha ajitoe akili lakini iko siku atatamani kushirikiana na yeyote hata Somalia na hatopata. Inaweza kuwa dua la kuku.
Hawawezi, hao ni maskini km maskini wengine ndo maan wanaendeshwa na Marekan. Wanashindwa hata kupeleka MICHANGO yao kwa wakati huko NATO sasa ndo watoe misaada kwa Ukraine peke yao.
 
Wamempiga nyuki busu wakajua maumivu yake alafu wewe unashauri waendelee na huu mchezo?

Tangu 2014 nawaambia wajinga kama wewe kuingia vitani na Urusi ni sawa na kudumbukia kwenye tanuru la kuyeyusha vyuma.
Falme nyingi zimeijaribu urusi zikapotea usije kufikiri marekani ni mjinga
Muue 🤣🤣🤣🤣🤣🙏
 
hv unajuwa hali ya Urusi sas hv ? Urusi wamefikia hatua ya kusema liwalo na liwe ika sio kwamba ukimya wao unamaanisha wapo vzr , Trump katumia busara , Hii vita imempa fursa nying China na lzn wafanye maamuz kama haya ili China asiwapige gap kubwa , kipind cha hii vita ndo China kapata ushawishi mkubwa baran kwake Asia ambako wengi walikiwa hawamtaki pia Ndo kipind China kawatoa rasmi wazungu huku Afrika , pia ndo kipind China kaanza tawala soko la Ulaya , pia ndo kipind China amepanya option ya kuiangusha USA kwa kuitumia Urusi , so ni lzm Trump arud nyuma aweke sw ila bila uwepo wa China kama superpower bas USA angemvagaa Urusi na kumdunda vzr maana hata kama angerud nyuma bas bado angekuwa kileleni maana kutoka yeye hadi mtu wa tatu anamzid krb mara 2 ila huyu wa pili yake yupo makalion , USA akidelay kdg China anakaa Mbele zaid , so uwepo wa China km mshindani wa USA ndo umefanya Trump afanye hayo maamuz
Unaongea utumbo
 
Mwaka 1968 aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje ya Marekani Henry Kissinger alisema:

"Inaweza kuwa hatari kuwa adui wa Marekani, lakini kuwa rafiki wa Marekani ni majanga."
– Henry Kissinger

Na Marekani imethibitisha kuwa Kissinger alikuwa sahihi. Mara kwa mara, Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Zamu hii Ukraine na Ulaya wamejifunza.

Akizungumza na washirika wa NATO mjini Brussel, Belgium, Waziri wa Ulinzi wa Marekani alitoa matamshi ambayo naamini mpaka sasa Zelensky na viongozi wa Ulaya hawaamini macho yao.

"Hakuna uanachama wa NATO kwa Ukraine"

"Hakuna vikosi vya Marekani kwenda nchini Ukraine"

"Hakuna askari wa NATO kwenda nchini Ukraine. Lakini nchi za Ulaya zinaweza kutuma wanajeshi wao wenyewe.”

"Lazima tuanze kwa kutambua kwamba kurudishwa kwa mipaka ya Ukraine ya kabla ya 2014 ni lengo lisilowezekana, kufuatia lengo hili lisilowezekana kutaongeza muda wa vita na kusababisha mateso zaidi."

"Wanajeshi wowote wa Uingereza au Ulaya ambao walitumwa nchini Ukraine hawatakuwa chini ya misheni ya NATO au na dhamana ya kifungu cha 5 cha muungano huo, watategemea usaidizi kutoka kwa mataifa yanayoshiriki."

– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)

Na kama haitoshi naye Trump alifanya mazungumzo na Putin kwa saa 1:30 wakaafikiana kuwa watakutana Saudi Arabia mada kuu itakuwa suala la vita ya Ukraine.

Lakini wakati huohuo Trump alitumia dakika 10 tu kuongea kwenye simu na Zelensky.

Ukraine imepoteza mamia ya maelfu ya askari, mamilioni ya Waukraine wamekimbia nchi yao, wamepoteza karibu 20% ya ardhi yao na uchumi na miundombinu mingi kuharibiwa na Urusi.
Mzee ana akili kuliko mbumbumbu wote wa ulaya na Ukrain ndio maana.
 
We are strong together than alone.

Ukraine inahitaji support ya kila aina kutoka Nchi wananchama wa NATO, kama Marekani imekataa kwa sababu zake za siasa za ndani, basi wanachama waliobaki wajipange au waunde ummoja mpya na wamkaribishe mwenzao wakimuacha wanamkaanga.

Acha ajitoe akili lakini iko siku atatamani kushirikiana na yeyote hata Somalia na hatopata. Inaweza kuwa dua la kuku.
Ukraine sio mwana chama wa NATO na the facts are, one of the reason why Russia aliamua kuivamia Ukraine ni hilo tishio la wao kujiunga na NATO.
Twendeni mbele kidogo, why Nyerere aliamua kulazimisha muungano wetu na Zanzibar? Zanzibar imeachiwa uhuru wa kila kitu except ulinzi na mengine haya ni ziada tu, wameachiwa bendera, wimbo wa taifa, serikali ya kitaifa etc but ULINZI ni marufuku; same as this, unajua why USA alikua na ugomvi na Cuba ya Fidel Castor for over 70 years? Issue ni hiyo hiyo tu, security. Trump/USA haitaruhusu eti Canada ijiamulie inavyo taka, ishirikiane na inaemtaka, ng'o. Haitatokea na ndio maana juzi Trump alidiriki kusema, Canada ni jimbo la 51 la USA, he meant business, hakua anatania; sasa hvi anavitaka visiwa vya Greenland, why? Sio utalii, same reasons, security. Itokee leo eti Russia apeleke silaha za ulinzi Panama? Weee, hakuna rangi tutaacha kuziona from USA. Trump na management yake ya sasa wapo sahihi kwa Russia, kuendelea kuing'ang'ania Ukraine kuta escalate mambo mengi from Russia, nae ataanza chokochoko America ya kusini, anaweza kuzirudisha nchi za ulaya ya mashariki kwenye himaya yake; bora kuachana nae watu wawe salama
 
Nguvu ya marekani kwa nchi za ulaya ni kubwa sana kuliko mnavyidhani saivi waziri wa mambo ya nje wa marekani na Elon mask wansagia kunguni waziri mkuu wa German kuwa hafai kuwa waziri mkuu na uchaguzi ni mwezi wa 4 mwaka huu kwa mategemeo halisi ni kuwa chama chake kitapiteza vitu na ataanguka huu uchaguzi ataingia serikali ambayo inapinga vita vya ukrein na itakata support ni swala LA muda atabaki France mwenyewe kusaport hii vita na kidogo UK japo naye kwa marekani haongei sababu ndyo aliyeshikilia uchumi wake na mshikira wa kumtegemea
 
Mwaka 1968 aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje ya Marekani Henry Kissinger alisema:

"Inaweza kuwa hatari kuwa adui wa Marekani, lakini kuwa rafiki wa Marekani ni majanga."
– Henry Kissinger

Na Marekani imethibitisha kuwa Kissinger alikuwa sahihi. Mara kwa mara, Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Zamu hii Ukraine na Ulaya wamejifunza.

Akizungumza na washirika wa NATO mjini Brussels, Belgium, Waziri wa Ulinzi wa Marekani alitoa matamshi ambayo naamini mpaka sasa Zelensky na viongozi wa Ulaya hawaamini macho yao.

"Hakuna uanachama wa NATO kwa Ukraine"

"Hakuna vikosi vya Marekani kwenda nchini Ukraine"

"Hakuna askari wa NATO kwenda nchini Ukraine. Lakini nchi za Ulaya zinaweza kutuma wanajeshi wao wenyewe.”

"Lazima tuanze kwa kutambua kwamba kurudishwa kwa mipaka ya Ukraine ya kabla ya 2014 ni lengo lisilowezekana, kufuatia lengo hili lisilowezekana kutaongeza muda wa vita na kusababisha mateso zaidi."

"Wanajeshi wowote wa Uingereza au Ulaya ambao walitumwa nchini Ukraine hawatakuwa chini ya misheni ya NATO au na dhamana ya kifungu cha 5 cha muungano huo, watategemea usaidizi kutoka kwa mataifa yanayoshiriki."

– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)

Na kama haitoshi naye Trump alifanya mazungumzo na Putin kwa saa 1:30 wakaafikiana kuwa watakutana Saudi Arabia mada kuu itakuwa suala la vita ya Ukraine.

Lakini wakati huohuo Trump alitumia dakika 10 tu kuongea kwenye simu na Zelensky.

Ukraine imeambulia kupoteza mamia ya maelfu ya askari, mamilioni ya Waukraine wamekimbia nchi yao, wamepoteza karibu 20% ya ardhi yao na uchumi na miundombinu mingi kuharibiwa na Urusi.
Ukrain watalipa madeni ya silaha mpk vitukuu vyao plus kuchukuliwa malighafi, person of interest hajawahi acha mtu salama
 
Back
Top Bottom