Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Sasa ni rasmi na hiyo ndege itakuwa retrofitted kabla haijaanza kutumika kumsafirisha Rais.
Marekani imepokea ndege iliyokusudiwa kwa ajili ya msafara wa Air Force One kutoka Qatar — zawadi ambayo imezua ukosoaji mkubwa, hata kutoka kwa baadhi ya wafuasi wakubwa wa Rais Donald Trump.
“Waziri wa Ulinzi amekubali ndege ya Boeing 747 kutoka Qatar kwa mujibu wa sheria na kanuni zote za serikali ya shirikisho,” alisema msemaji mkuu wa Pentagon, Sean Parnell, katika taarifa siku ya Jumatano.
Ndege hiyo itahitaji kufanyiwa marekebisho kabla ya kutumika kama sehemu ya msafara wa Air Force One — chombo rasmi cha usafiri wa anga cha rais wa Marekani.
Ikulu ya White House imesisitiza kuwa zawadi hiyo ni halali kisheria, lakini tangazo la uhamisho huo wiki moja iliyopita liliibua mjadala mkali.
Ndege hiyo imetolewa na familia ya kifalme ya Qatar na inakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 400 (sawa na pauni milioni 300). White House imesema kuwa ndege hiyo mpya itahamishiwa kwenye maktaba ya urais ya Trump mwishoni mwa muhula wake.
www.bbc.com

US defence officials confirm acceptance of Qatari plane for Air Force One
The White House insists that the gift is legal, but some of Trump's biggest backers have criticised the deal.