Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Marekani ni taifa linaloheshimika duniani kwa kuwa na katiba ya kihistoria yenye kuheshimu haki za binadamu, pamoja na mfumo wa kidemokrasia ulio imara. Chaguzi za Marekani huendeshwa kwa uwazi na uhuru mkubwa. Licha ya hayo yote, bado katika Taifa hilo kubwa duniani, tunashuhudia matukio ya vurugu za kuipinga serikali, risasi na mabomu ya machozi kuzima maandamano, uhalifu mitaani, watoto wa shule kuingia darasani na bunduki na matendo mengi yasiyo ya haki miongoni mwa watu. Hii inazua swali kubwa: Kama wana katiba nzuri na uchaguzi wa haki, kwanini uasi na matatizo hayo hayaishi?
Nimetafakari na kugundua kuwa jibu kamili la swali hili halipatikani katika nyanja za kisiasa au kisheria bali linapatikana katika Neno la Mungu. Biblia inasema wazi kwamba chanzo cha matatizo yote tunayoyaona duniani ni dhambi ya mwanadamu.
“Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Warumi 3:23)
Katiba haiwezi kutakasa dhamiri ya mwanadamu, wala sheria haiwezi kugeuza moyo wa mtu. Sheria inaweza kuzuia tabia mbaya kwa nje, lakini dhambi hutoka moyoni. Vurugu hazianzi na bunduki, bali na moyo uliojaa chuki, uonevu na tamaa. Yesu anasema katika Mathayo 15:19
"Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano."
Hii ndiyo hali ya ulimwengu mzima. Kwa sababu mioyo ya watu wengi imejaa dhambi, kila taifa linashuhudia matokeo ya dhambi: vita, migogoro, chuki, na kutokuwepo kwa amani ya kweli.
Namshukuru Mungu hakutuacha bila tumaini. Biblia inasema:
“Lakini kufuatana na ahadi yake, sisi tunatazamia mbingu mpya na dunia mpya, ambayo haki hukaa ndani yake.”
(2 Petro 3:13)
cc: Mshana Jr Pascal Mayalla Doctor Mama Amon