Marekani inafikiria kuizuia China kutumia mfumo wa Dollar kwenye malipo yoyote yanayohusu Dollar ya Marekani

Marekani inafikiria kuizuia China kutumia mfumo wa Dollar kwenye malipo yoyote yanayohusu Dollar ya Marekani

Tusichanganye mambo jamani. SWIFT ni mfumo tu wa mawasiliano ya kibenki na makao makuu yake yako Belgium sio USA. Hivyo transfers zinazohitaji clearing ya US Dollar ndiyo zitapitia USA. Lakini ziko clearing za currencies nyingine kama vile Euro na Stg Pounds. Na sasa Yuan inayo clearing system yake. Kumbukeni tu kuwa Yuan sasa hivi ni moja ya currency kubwa za dunia na kwenye composites ya Special Drawing Rights (SDR) Yuan ina occupy more than 10% ya weight ya SDR. Kama USA ataamua kuizuia China kutumia currency yake huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa USD duniani. Hesabu ndogo tu ni kwamba ili currency iwe na nguvu factors za uwezo wa kiuchumi wa nchi husika na mahitaji ya hiyo currency katika kufanya settlements ndio nguzo muhimu. China anazo sifa hizo. Mataifa mengi yanafanya biashara na China hivyo watu watahitaji tu Yuan kupata bidhaa kutoka China. Inatakiwa akili kubwa kuelewa consequences ya China kuacha kutumia USD.
Watu wengine! Mnajifanya wachumi wakati wenu unadidimia kila uchao na mpo tu hamna mnachofanya. Wataalamu wa uchumi wa huko Marekani eti wasijue hilo nyie wa vijiwe vya kahawa ndio mjue. Only cretins will take you seriously.
 
Tusichanganye mambo jamani. SWIFT ni mfumo tu wa mawasiliano ya kibenki na makao makuu yake yako Belgium sio USA. Hivyo transfers zinazohitaji clearing ya US Dollar ndiyo zitapitia USA. Lakini ziko clearing za currencies nyingine kama vile Euro na Stg Pounds. Na sasa Yuan inayo clearing system yake. Kumbukeni tu kuwa Yuan sasa hivi ni moja ya currency kubwa za dunia na kwenye composites ya Special Drawing Rights (SDR) Yuan ina occupy more than 10% ya weight ya SDR. Kama USA ataamua kuizuia China kutumia currency yake huo ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa USD duniani. Hesabu ndogo tu ni kwamba ili currency iwe na nguvu factors za uwezo wa kiuchumi wa nchi husika na mahitaji ya hiyo currency katika kufanya settlements ndio nguzo muhimu. China anazo sifa hizo. Mataifa mengi yanafanya biashara na China hivyo watu watahitaji tu Yuan kupata bidhaa kutoka China. Inatakiwa akili kubwa kuelewa consequences ya China kuacha kutumia USD.
Hivi kwa nini watu hawaoni kwamba hii move ya Trump ni out of hubris na itakuwa na counterproductive trend kwa US dollar?

Moja ya njia ya kusoma hii move, ni kuangalia general trend ya thamani ya dollar siku hii habari ilivyotangazwa, granted, dollar inaweza kuwa unaffected by other reasons, lakini ukiona thamani ya dollar imeshuka kwa kasi dhidi ya multiple currencies siku ya tangazo hili, hapo utaona markets zinechukulia habari hii negatively.

That is a very good way of reading this.

Sijaangalia bado, lakini, kama nina trade forex, halafu napata habari kesho hili tangazo litatolewa, nitajiandaa kuona dollar inashuka thamani na short term strategy itakuwa ni kuuza dollar haraka sana. Unless kuna strategy ya ku hild muda mrefu.
 
Utawala wa Bwana Donald Trump unafikiria kuizuia China kutumia mfumo wa Dollar kwenye manunuzi ya aina yoyote au wanaita dollar decoupling.

Dollar ya kimarekani ndio sarafu maarufu inayotumika kufanya malipo Duniani, zaidi ya 60% ya malipo Duniani yanafanyika kwa njia ya Dollar.

Dollar ndio safaru inayotumiwa na nchi nyingi Duniani kuthaminisha sarafu zao.

Trump anasema hii inaitwa financial nuclear option ya kuimaliza China.

US-China decoupling already under way, John Bolton says
Washashindwa kwa China...pamoja na janga la korona bado China ndo inarecord the highest rate za ukuaji wa uchumi....

Wamemshindwa trade war, sunction,kupandikiza ugaidi,kuigawanya Hong Kong kwa China,Macau, Tibet na xianjian ...wanahema tu ....hii nchi ya China waacheni tu....marekani Alie tu watakwama napo
 
Nadharia yako iko sahihi kinadharia, ila uhalisia kutokea hili sio rahisi. Kwenye information technology bado teknolojia nyingi ni za US au washirika wake. Kutengeneza hizo chip like EMV or So unahitaji teknolojia ambazo kwa kiasi kikubwa ni za Marekani. So theoretically that can happen but practically... doubtful!
Na mimi nimesema hiki si kitu cha kutokea mara moja.

Ila, ukweli kwamba si rahisi nyumba kushika moto haukufanyi baba mqenye nyumba ucheze na mto ndani ya nyumba kwa kusema nyumba haiwezi kuungua moto kirahisi. Unaweza kushindwa ku u control moto, nyumba ikaungua.

Trump anachofanya sasa hivi ni kusema kwamba nyumba haiwezi kushika moto kirahisi, anacheza na moto. Na kibaya zaidi, ana alienate si tu maadui wa US, bali mpaka marafiki.

Anajiweka katika nafasi ya ku fight nchi kama China alone. Kitu ambacho si kizuri.

Rais wa zamani wa US, Thwodore Roosevelt alikuwa na msemo wake, alikuwa anasema "speak softly and carry a big stick". Kwamba Marekani inatakiwa kuongea kwa sauti nzuri, lakini vitendo vyake viwe kitisho.

Maana yake ni kwamba nchi inaheshimiwa sana kwa uwezo wake kiasi haihitaji kutoa vitisho, unashawishi kwa diplomasia, na ukitaka kuikosea, daflao lake ukilifikiria kwa kuangalia utakavyopatilizwa, unajirudi mwenyewe bila hata Mmarekani kufanya kitu.

Sasa hivi Trump anapiga kelele, halafu zaidi ya vikwazo (ambavyo wa Iran wanaonekana kuvikabili bila kutetereka) hana karata nyingine.

Dollar kuanguka ni vigumu. Ina mfumo wenye kina kirefu, lakini, Trump ana undermine nguvu za dollar kwa sababu shallow za kisiasa.
 
Unadhani hawakufikiria hilo? Ukiona Eais wa nchi yeyote katoa maamuzi kama hayo, ujue hakuamka tu akaenda kwenye mic. Kuna strategy na strategist!
Hilo ni kweli kwa marais wa kawaida.

Trump si rais wa kawaida.

Tumeona mara kadhaa anapingana na wataalamu wa serikali yake, anawatungia conspiracy theories, anawaita Deep State, anapingana na wakuu wa majeshi mpaka wakuu wa diplomasia. Anasema anajua mambo ya ulinzi kuliko ma General. Kajiita yeye ni "a very stable genius"

Tunaona anavyokwaruzana na Dr. Fauci kwenye pandemic.

Kwa hiyo kusema Trump hawezi kujiamulia mambo mwenyewe tu si kweli.
 
Kama Mchina ana dollar zake, na anataka kununua mafuta ya MSaudi au dhahabu ya Mtanzania kwa dollar za Kimarekani, Mmarekani atamzuia vipi Mchina kutumia dollar?
Wanazuia global payment gateways kama ambazo ni Banks za kimataifa zilizo na ushirika na marekani zisiruhusu kufanya malipo yanayotokea China, na pia hata kufunga accounts zao za dola zilizo kwenye hizo Banks
 
Kwani Mchina hawezi kufanya money transfer kumlipa MSaudi bila kutumia mfumo wa Mmarekani?
 
Thamani ya dollar ya US, kwa sehemu kubwa, inatokana na ukweli kwamba dollar inatumika sana katika biashara ya kimataifa.

Siku watu wa dunia yote wakiacha kutumia US dollar, wakaweka treasury reserves zao kwa Chinese Yuan kwa mfano, na Mchina akanunua mafuta ya MSaudi kwa Yuan, US dillar itaanguka thamani vibaya sana.

Trump, kwa ukaidi au ujinga, anaiharakisha siku hii ya US dollar kuanguka.
SIjasomea uchumi kabisa, naomba niulize. Trump hana washauri wa kiuchumi ambao wabgeshauri Trump kwamba anachokifanya anakosea?
 
Suluhisho la mwisho ni kutumia Iranian option.

Yeyote atakaefanya biashara na Chinese Communist Party state anawekewa embargo ya kufanya biashara na USA.
 
Kwani Mchina hawezi kufanya money transfer kumlipa MSaudi bila kutumia mfumo wa Mmarekani?
Anaweza kwa kutumia Bank isiyo mshirika na Marekani, lakini kama Marekani watapewa baraka na WB ya hicho wanachotaka kufanya, bado WB wataadhibu hiyo Bank sababu International transfers zinaratibiwa na WB
 
SIjasomea uchumi kabisa, naomba niulize. Trump hana washauri wa kiuchumi ambao wabgeshauri Trump kwamba anachokifanya anakosea?
Anao,

Lakini anasema yeye ni "a stable genius", hasikilizi wahsuri. Wahauri wakimshauri tofauti na anavyotaka kusikia yeye, anasema hao ni mapandikizi ya Obama, ni Deep State.

Wataalamu wa serikalini Marekani wanalalamika sana kwamba Trump hasikilizi ushauri wa kitaalamu, anafanya anavyotaka yeye.

Kuna watu kibao wameacha kazi wameandika vitabu vya madudu waliyoona kwenye serikali ya Trump, kitabu cha hivi karibuni kabisa ni cha John Bolton kinaitwa "The Room Where It Happenned", ameelezea sana ubishi wa kijinga na ujinga wa Trump. Na huyo ni Republican mwenzake, wala si Democrat.

Pia kasome kitabu cha Andrew G. McCabe "The Threat: How The FBI Protects America in the Age of Terror and Trump".

Trump kasema yeye anajua masuala ya vita na ulinzi kuliko ma Jenerali wa jeshi.

Hasikilizi wataalamu.
 
USA wamechelewa, China amejipanga ERMs zitakufa kifo cha mende tutarudi kwenye Gold kama benchmark kama Trumpet atashinda U-rais.
 
Anaweza kwa kutumia Bank isiyo mshirika na Marekani, lakini kama Marekani watapewa baraka na WB ya hicho wanachotaka kufanya, bado WB wataadhibu hiyo Bank sababu International transfers zinaratibiwa na WB
World Bank kama sehemu ya UN hupitisha mambo yanayojadiliwa na kupitishwa na vikao vya UN.

Na hili kupitishwa kwenye vikao vya UN si rahisi.

Kumbuka, China si Iran, nayo ni permanent member wa Security Council UN, na ina ushawishi mkubwa.

Zaidi, ujinga inayoufanya serikali ya Marekani - Trump for the most part-sasa hivi ni kudharau hata rafiki zake, kujifanya inaweza kufanya mambo peke yake.

Sasa hapo ndipo utakapokuja muda wa kupiga kura halafu rafiki za China wote wakapiga kura na China, rafiki za Marekani nao wengine wakapiga kura na China, wengine wasipige kura na wachache wakapiga kura na Marekani.

Kwa hiyo Mmarekani kwa sasa akishindana na Mchina kwenye mambo kama haya, na ikaonekana wazi Mmarekani analeta ubabe, atachinjwa kwenye kura tu hapo UN.
 
Anao,

Lakini anasema yeye ni "a stable genius", hasikilizi wahsuri. Wahauri wakimshauri tofauti na anavyotaka kusikia yeye, anasema hao ni mapandikizi ya Obama, ni Deep State.

Wataalamu wa serikalini Marekani wanalalamika sana kwamba Trump hasikilizi ushauri wa kitaalamu, anafanya anavyotaka yeye.

Kuna watu kibao wameacha kazi wameandika vitabu vya madudu waliyoona kwenye serikali ya Trump, kitabu cha hivi karibuni kabisa ni cha John Bolton kinaitwa "The Room Where It Happenned", ameelezea sana ubishi wa kijinga na ujinga wa Trump. Na huyo ni Republican mwenzake, wala si Democrat.

Pia kasome kitabu cha Andrew G. McCabe "The Threat: How The FBI Protects America in the Age of Terror and Trump".

Trump kasema yeye anajua masuala ya vita na ulinzi kuliko ma Jenerali wa jeshi.

Hasikilizi wataalamu.
Ngoja nisake hizo manual mbili, najua nitaondoka angalau na wazo moja
 
Anaweza kwa kutumia Bank isiyo mshirika na Marekani, lakini kama Marekani watapewa baraka na WB ya hicho wanachotaka kufanya, bado WB wataadhibu hiyo Bank sababu International transfers zinaratibiwa na WB
WB iko waap? Mfadhil mkubwa ni nani? Mkuu wa WB kwa sasa ni nan?
 
Ngoja nisake hizo manual mbili, najua nitaondoka angalau na wazo moja
Ninazo kwenye pdf, ngoja nikutafutie.

Halafu kuna kingine katoa mtoto wa kaka yake Trump anaitwa Mary Trump, huyo ndiye kapiga ua galagaza kabisa, maana yeye katoa zile siri za familia ya Trump za ndanindani kabisa.

Kitabu kinaitwa " "Too Much and Never Enough: How My Family Created the World's Most Dangerous Man"

Nacho pia ninacho. Ninamalizia kazi fulani hapa nikipata muda nitaviweka.

Mary Trump's book breaks record with mammoth sales
 
Utawala wa Bwana Donald Trump unafikiria kuizuia China kutumia mfumo wa Dollar kwenye manunuzi ya aina yoyote au wanaita dollar decoupling.

Dollar ya kimarekani ndio sarafu maarufu inayotumika kufanya malipo Duniani, zaidi ya 60% ya malipo Duniani yanafanyika kwa njia ya Dollar.

Dollar ndio safaru inayotumiwa na nchi nyingi Duniani kuthaminisha sarafu zao.

Trump anasema hii inaitwa financial nuclear option ya kuimaliza China.

US-China decoupling already under way, John Bolton says
Trump anajiua mwenyewe anajipeleka shimoni
 
Hiiv jaman ni kwamba sisi ambao tuko Tanzania na si ajab wengi hapa hata Amsterdam tuu hamja cross ndio tunajua zaid ya hawa wamarekan? Kwamba wao wakati wanaamua haya hawajafikiria hilo?

Kwa hio all major banks pale kuanzia BA, JP, Chase bank, Lehman Brothers, Citi Bank, including Federal reserve hawa woote hawajaona haya ni sisi tu tunaona hii impact.....narudia tena msemo wake "we have gat all options on the table" kwa hio mchina yeye baada ya hilo achague njia yake then ndio tutaanza kuona zile options sasa pale mezan
Kama ambavyo hawakujua kuwa MChina atakuja kuwa tishio kwao ndiivyo hata haya maamuzi wanayafanya wakiwa na hasira tu
 
Back
Top Bottom