Marekani: Iran imehusika kuangusha ndege ya Ukraine

Marekani: Iran imehusika kuangusha ndege ya Ukraine

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,303
Reaction score
23,064
1578630980081.png

Idara ya Ujasusi ya Marekani imeripoti kwamba, Iran imehusika na kuanguka kwa ndege ya Ukraine Boeing 737-800 kwa kuangishwa kwa bomu.

=====

Iran mistakenly shot down the Ukrainian plane that crashed on Wednesday near Tehran with 176 people on board, US media report.

US officials say they believe the Ukrainian International Airlines Boeing 737-800 was hit by a missile, CBS says.

Ukraine earlier said it was examining whether a missile strike brought down the aircraft - but Iran ruled this out.

The crash came just hours after Iran carried out missile strikes on two airbases housing US forces in Iraq.

CBS News quoting US intelligence said a satellite detected infrared "blips" of two missile launches, followed by another blip of an explosion.

====
Ushahidi unaashiria kuwa kombora la Iran lilidungua ndege ya abiria ya Ukrain iliyoanguka karibu na Tehran, kimakosa, viongozi wa magharibi wanasema.

Viongozi wa Canada na Uingereza wanataka uchunguzi wa kina ufanyike kubaini chanzo halisi kilichosababisha, ajali iliyowaua watu wote 176 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Ukraine awali ilisema kuwa inachunguza endapo ndege yake iliangushwa na kombora, jambo ambalo mamlaka za Iran zilikanusha vikali.

Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.

Awali maafisa wa serikali ya Marekani kwa mujibu wa runinga ya CBS wanaamini ndege hiyo ilidunguliwa na kombora na kuiangusha karibu na Jiji la Tehran na kuua watu wote 176 waliokuwa ndani yake.


CBS imevinukuu vyanzo vya kijasusi vya Marekani vinavyodai kuwa picha za satelaiti zinaonesha mwanga wa makombora mawili ambao ulifuatiwa na mwanga wa mlipuko.

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Alhamisi alisema: "nina mashaka" juu ya (kuanguka) kwa ndege. "Inawezekana kuna mtu amefanya kosa kubwa."

Iran imetangaza kutokabidhi kisanduku cheusi cha kuhifadhi taarifa za ndege kwa kampuni ya ndege ya Boeing ama serikali ya Marekani kwa uchunguzi wa ajali hiyo.

Hatua hiyo inatokana na mzozo uliokomaa baina ya Marekani na Iran, hasa baada ya Trump kuagiza shambulio la anga lililomuua Jenerali wa Iran Qasem Soleimani Januari 3.

Chini ya sheria za kimataifa za usafiri wa anga, Iran ina haki ya kuongoza uchunguzi wa ajali hiyo lakini kawaida huwa kampuni iliyotengeneza ndege pia hushirikishwa kwa karibu.

Ndege hiyo ni Boeing 737-800 ambayo imetengenezwa Marekani, nchi ambayo ni hasimu wa Marekani. CBS na Newsweek wanaripoti kuwa maafisa wa ujasusi wa Marekani na Iraq wana hakika kuwa ndege hiyo iliangushwa na makombora ya Iran.

CBS wamechapisha taarifa inayodai kuwa mitambo ya rada ya Marekani ilibaini makombora mawili yakirushwa muda mfupi kabla ya ndege hiyo kulipuka.Kwa upande wa Newsweek wamewanukuu maafisa wa Marekani na Iraq ambao wanaamini ndege hiyo ilidunguliwa na makombora ya Kirusi aina ya Tor M-1 ambayo Nato huyaita Gauntlet.

Maafisa wawili kutoka makao makuu ya jeshi la Marekani wameithibitishia Newsweek kuwa shambulio hilo lilikuwa la bahati mbaya.

Hata hivyo, Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Iran Ali Abedzadeh amesema: " Ndege hiyo ambayo awali ilikuwa ikielekea magharibi baada ya kupaa ilikata kona kulia kutokana na hitilafu ya kiufundi na ilikuwa ikirejea uwanja wa ndege pindi ilipoanguka."

Abedzadeh ameongeza kuwa mashuhuda waliona ndege hiyo "ikiwaka moto" kabla ya kuanguka na kuwa marubani hawakutoa taarifa yoyote ya dharura kabla ya kujaribu kurudi uwanja wa ndege wa Imam Khomeini.

"Ndege kadhaa za ndani na nje zilikuwa zikipaa katika anga la Iran katika usawa wa futi 8,000 (kama ndege ya Ukraine). Hivyo suala la kupigwa na makombora haliwezi kuwa na ukweli wowote," ameongeza.

Afisa huyo amedai kuwa taarifa za awali za uchunguzi zimeshapelekwa Ukraine na Marekani, ambapo ndipo makao makuu ya Boeing.

Taarifa hizo pia zimepelekwa Sweden na Canada ambao pia wamepoteza raia wao.




Source: BBC NEWS
 
Wewe dada sijui unasimama kwenye nini, kwenye ule mjadala wa Iran kukataa kupeleka Black box Boeing ulikuwa kama pilipili

Sasa hivi unasema una suspect ndege ilitunguliwa

Unafikiria kwanini Boeing wali request black box from the first place?

Hata mimi nafikiria hivyo. Too sad. Watu wasio na kosa lolote wamekufa. Iran lazima ahide hii. Maana kishasema black boxes zimeharibika. I believe this in not true. Iam strongly conviced that,the plane was hit by one of the Missiles.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo tatizo la kukurupuka kushindana na mkubwa wako. Iran bado mtoto mdogo ktk matumizi ya sayansi na teknolojia hivyo aache kufurukuta na kujitutumua ktk masuala makubwa mawili ya Geopolitics na military power, ataingia ktk mabalaa mengi.

George Friedman : Geopolitics matter :



Source: Danube Institute
 
Ndiyo tatizo la kukurupuka kushindana na mkubwa wako. Iran bado mtoto mdogo ktk matumizi ya sayansi na teknolojia hivyo aache kufurukuta na kujitutumua ktk Geopolitics ,ataingia ktk mabalaa mengi.
Russia mbona nao walitungua ndege bahati mbaya si suala la teknolojia sometimes yanatokea tu.
Hao US wenyewe waliahi tungua ndege ya abiria ya Iran wakaua watu wote onboard
 
We ndo uliowaumba mpaka useme hawana kosa lolote au ndo akili za mtindi
Hata mimi nafikiria hivyo. Too sad. Watu wasio na kosa lolote wamekufa. Iran lazima ahide hii. Maana kishasema black boxes zimeharibika. I believe this in not true. Iam strongly conviced that,the plane was hit by one of the Missiles.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekan wanacngizia bomu la Iran ili kuficha kashfa ya kampuni ya boing Kama inatengeneza vitu vibovu Ila Ukrain wenyewe wamesema tatiz la kiufund
Ndiyo tatizo la kukurupuka kushindana na mkubwa wako. Iran bado mtoto mdogo ktk matumizi ya sayansi na teknolojia hivyo aache kufurukuta na kujitutumua ktk masuala makubwa mawili ya Geopolitics na military power, ataingia ktk mabalaa mengi.

George Friedman : Geopolitics matter :



Source: Danube Institute


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom