Marekani: Kijana aua watoto 19 wa shule ya msingi kwa kuwafyatulia risasi darasani

Inasikitisha sana hawa watu akili zao hafifu kabisa..
 
Sheria ya ununuzi/umiliki silaha marekani wanaiona ni Bora kuliko maisha ya raia wao..
 
Utasikia ana tatizo la afya ya akili,na tatizo hilo analo toka akiwa na umri wa miaka 5
Ila ingekua wa dini ile wangesema ni Gaidi.

Hilo tunalijua
Sababu ya kwanza mgonjwa
Tena kwa kuwa ni Latino ndio wamemuua
Angekuwa ndugu yao wangemuomba aweke silaha chini na kujisalimisha

Ni weupe wachache wanawauwa kwa bahati mbaya
Wakiwashika wanapelekwa hospitali ya wehu

Ila huko sio kwa kuishi
 
Ni upumbavu tu na chuki ndio wanavyoviwaza kwanza
 
Jamani hii Dunia inakoelekea sijui wapi
 
Sasa wamefikia 21, halafu walivyokua wajinga hawaiti ugaidi huu, vitoto maskini havijui chochote vimeuwawa kinyama na gaidi
ugaidi lazima uwe na sifa mkuu.

uwe na lengo la kushinikiza,kutisha mamlaka,na kuzua taharuki,kwa malengo ya kidini au kisiasa.

kinyume na hapo mhusika anakuwa mgonjwa wa akili tu,hata kama ana sijda.
 
Ubalozi wa Tanzania nchini Jamiiforum una utaarifu umma na raia wake kuwa hivi sasa Marekani sio sehemu salama kwa usalama wao.
 
Hilo eneo wakazi wengi ni walatino..naamini haya idara yao ya polisi wengi na inaongozwa na hao hao..
 
... pole zao! Wamarekani wasipoangalia upya sera yao ya umiliki wa mabunduki itawagharimu sana. Muuwaji ni race gani? Asili ya wapi? Utimamu wa afya ya akili? Hizo ni parameters muhimu.
Ukistaajabu ya Mussa,Kuna baadhi ya maeneo yenye sheria kali zaidi huko ndio haya matukio hayaishi..Chicago,CA, na NY..kwa uchache tu..
 
Anders na Timothy wote ni magaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…