Uchaguzi 2020 Marekani: Kuanzia leo, tunaweka vizuizi kwa waliohusika na kuvuruga Uchaguzi nchini Tanzania

Ni mwanzo mzuri sana, hawa wapuuzi akina jiwe na genge lake ni lazima wakutane na ombwe la demokrasia ya kweli kutoka kwa Rais Joe Biden. Good.
 
Mbona Makonda kazuiliwa na maisha yanaendelea manka?

Marekani kitu gani bhana dunia iko kiganjani!
 
Si chini ya mwezi mmoja, Bunge la Umoja wa Ulaya limependekeza na kuridhia taratibu za vikwazo vinavyowekwa na Marekani kutumika pia Umoja wa Ulaya.

Nadhani wewe ni Mchanga sana na hujui impact ya travel Ban. Kwa taarifa yako ni kuwa hao watu na familia zao wataweza kwenda Asia na nchi na Africa tu. Na ikitokea wamepigwa na Ban za kufanya miamala ya kifedha ndo wameumia maana systems za kibank duniani karibu zote ziko chini ya hao hao.

Kikubwa kwa sasa ni watu wasali wasiwepo kwenye hiyo list Ila wakiwepo tu wameumia.
 
Na msiseme Makonda alifungiwa kwa kukataa mashoga, Museveni hataki hata kuwasikia mashoga Uganda lakini Marekani anakwenda.
Basi ujue hao jamaa zenu wana lao jambo na tanzania, mbona hawazungumzii uchaguzi wa uganda ila wao wanaleta ujinga tanzania?
 
Ni mwanzo mzuri sana, hawa wapuuzi akina jiwe na genge lake ni lazima wakutane na ombwe la demokrasia ya kweli kutoka kwa Rais Joe Biden. Good.
Pompeo mwenyeqe anatupwa nje baada ya biden kuapishwa.
 
Hapo inatakiwa diplomacy ya hali ya juu sana hasa kwa serikali ya Biden!!! Kabudi hana diplomacy ni mtu wa maguv na hapo ndio tunawakumbuka watu kama marehemu Mahiga na uzoefu wao!!

..njia rahisi zaidi ni kuishi vizuri na jumuiya ya kimataifa.

..hivi kuna ubaya gani kwa vyombo vya dola na tume ya uchaguzi kutenda HAKI sawa kwa vyama vyote vya siasa?

..2015 tulipoharibu uchaguzi wa Znz Wamarekani walitukatia msaada wa program yao ya MCC.

..serikali inafanya mambo ya hovyo ambayo sidhani kama yanaweza kurekebishwa kwa kuwa na waziri wa mambo ya nje mwenye weledi.
 
Msiwe na wasiwasi; jamaa bado ana saa 20 tu madarakani. Jana alipokuwa Europe alisusiwa!
 
No justification for violation of human rights!
 
Biden aje apige vikwazo kabisa tena kama vile vya Iran ili akili ziwakae sawa MATAGA na wananchi wanyonge wa ccm
 
Nilitamani maneno haya angesema Meko sio wewe alafu tuone majibu ya Marekani Taifa kubwa watasemaje?
 
Mbona Makonda kazuiliwa na maisha yanaendelea manka?

Marekani kitu gani bhana dunia iko kiganjani!
Acha ubishi we MATAGA, siku jiwe atakapochapwa na TEZI DUME ndipo utakapoona madhara ya hiyo "statement" ya Pompeo. Utarudi hapa na kulia lia tu.
 
Uongo mtupu na story za matango pori ya vijiweni.Mara ya mwisho mgombea wa Democrat kushinda Texas ni mwaka 1976. Texas ni red state pimbi
 
Acha ubishi we MATAGA, siku jiwe atakapochapwa na TEZI DUME ndipo utakapoona madhara ya hiyo "statement" ya Pompeo. Utarudi hapa na kulia lia tu.
Kwai india haipo au unadhani marekani ndo wajanja zaidi?
Ujinga umewafunga macho.
 

Kama nchi siku hizi ule utamaduni wa kushauriana juu ya mambo muhimu ya nchi hakuna tena!! Tumemuachia mtu mmoja asiyekuwa na hulka ya kushauliana afanye maamuzi peke yake!!! Maendeleo ya nchi hupatikana kwa haraka zaidi kama wananchi wana uhuru wa kutoa maoni yao juu ya nchi yao! Hata ndani ya chama tawala ule uhuru wa mawazo umepokwa na ndio maana Mwenyekiti wao ndio anachagua nani atagombea katika chaguzi zote tofauti na huko nyuma!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…