Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona Makonda kazuiliwa na maisha yanaendelea manka?Kwa Taarifa yako waliozuiliwa wengi ni viongozi wako japo wa Tume nao wamo , kuna lundo la viongozi wanaokutumikisha , halafu kingine unachopaswa kufahamu ni kwamba ukizuiliwa na USA , basi kuna mataifa mengine kama 10 hivi hutakanyaga , omba Mungu msiugue Tezi dume au maradhi mengine ya kukata viungo
Kwani wenye hizo sura kila wanaposafiri huwa wanakuarifu
Basi ujue hao jamaa zenu wana lao jambo na tanzania, mbona hawazungumzii uchaguzi wa uganda ila wao wanaleta ujinga tanzania?Na msiseme Makonda alifungiwa kwa kukataa mashoga, Museveni hataki hata kuwasikia mashoga Uganda lakini Marekani anakwenda.
Pompeo mwenyeqe anatupwa nje baada ya biden kuapishwa.Ni mwanzo mzuri sana, hawa wapuuzi akina jiwe na genge lake ni lazima wakutane na ombwe la demokrasia ya kweli kutoka kwa Rais Joe Biden. Good.
Unaishi kwenye ujima wewe!Si chini ya mwezi mmoja, Bunge la Umoja wa Ulaya limependekeza na kuridhia taratibu za vikwazo vinavyowekwa na Marekani kutumika pia Umoja wa Ulaya...
Hapo inatakiwa diplomacy ya hali ya juu sana hasa kwa serikali ya Biden!!! Kabudi hana diplomacy ni mtu wa maguv na hapo ndio tunawakumbuka watu kama marehemu Mahiga na uzoefu wao!!
Msiwe na wasiwasi; jamaa bado ana saa 20 tu madarakani. Jana alipokuwa Europe alisusiwa!Kupitia akaunti yake ya Twitter, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo ameandika "Kuna matokeo ya kuingilia mchakato wa kidemokrasia. Kuanzia leo, tunaweka vizuizi vya visa kwa wale wanaohusika na uvurugaji wa uchaguzi nchini Tanzania. Tunabaki kujitolea kufanya kazi pamoja kuendeleza demokrasia na ustawi wa pande zote kwa nchi zetu zote mbili."
View attachment 1681412
Soma pia: Visa Restrictions on Tanzanians for Undermining the Democratic Process and Human Rights - United States Department of State
___________________________________________________
Marekani imetangaza kuwawekea vikwazo vya vya kuingia nchini humo maafisa wa Tanzania ambao nchi hiyo inawatuhumu kwa kile wanachokitaja kuwa kuharibu uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka 2020.
Maofisa hao wanatajwa kuhusika kuingilia mchakato wa uchaguzi na kuminya utekelezaji wa demokrasia.
Hata hivyo taarifa hiyo ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijabainisha ni viongozi gani hasa kutoka Tanzania waliowekewa vikwazo vya kuingia Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, Waangalizi wa uchaguzi na mashirika ya kiraia wanadai kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi huo pamoja na uvunjifu wa haki za binadamu wakati na baada ya uchaguzi.
Marekani inasema kuzimwa ama kuzimika kwa mitandao, kuminywa kwa waandishi wa habari na nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Polisi kunafanya uchaguzi huo kutokua huru na wa haki.
Katika uchaguzi huo, baadhi ya wagombea kutoka vyama vya upinzani walienguliwa kwa sababu mbalimbali na wengine kukamatwa.
Tume ya uchaguzi nchini humo na hata Serikali kupitia waziri wake wa mambo ya nje, Palamagamba Kabudi ilieleza kwamba uchaguzi ulikua huru na wa haki.
Marekani inasema pamoja na hatua hii iliyochukua dhidi ya maafisa wa Tanzania, inaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya hoja hiyo, huku ikisema haitasita kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wanaominya demokrasia na kuvunja haki za binadamu.
''Tunaitaka Tanzania, kuwachukulia hatua wale wote waliohusika kuvuruga uchaguzi, kufanya vurugu na kuleta vitisho'' ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Juhudi za kumpata msemaji wa serikali ya Tanzania kuzungumzia suala hilo mpaka sasa hazijazaa matunda, na tutaendelea kuwatafuta kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo
Haya ni moja ya maamuzi ya mwisho ya utawala wa rais Donald Trump ambaye amebakiza saa chache kuachia mamlaka ya urais. Mpaka sasa haijafahamika iwapo utawala wa rais mpya Joe Biden kama utatekeleza maamuzi hayo. Tayari ofisi ya Biden imetangaza kuwa itatengua sera kadhaa za Trump mara tu baada ya kuingia ofisini kesho.
BBC.
No justification for violation of human rights!Hata aibu hauoni! Sisi hii tunaita last kick of 'dying animal'!!
"US baby group" naona kiswahili mfukoni! !!! Kwishiney habari yenu. Ha ha ha ha aa!!!Nisikie tena kelele zenu za haki ya kujieleza na demokrasia wakati walezi wenu wa hiyo liberty hawawezi kufanya hayo waagizayo yafanywe na nchi nyingine.
Acha ubishi we MATAGA, siku jiwe atakapochapwa na TEZI DUME ndipo utakapoona madhara ya hiyo "statement" ya Pompeo. Utarudi hapa na kulia lia tu.Mbona Makonda kazuiliwa na maisha yanaendelea manka?
Marekani kitu gani bhana dunia iko kiganjani!
"Massive" does not mean " Total" hence waliweza kuchagua you NUT! Ndio maana Democrats walishindwa TEXAS ambako voter suppression ilikuwa very significant compared to Georgia ambako Stacey Abrahams na network yake waliweza kuthibiti voter suppression significantly na hivyo Democrats kushinda!!
Nchi hii imejaa wajinga first class! Huyu nae sijui ni msukuma wa wapi?
Kwai india haipo au unadhani marekani ndo wajanja zaidi?Acha ubishi we MATAGA, siku jiwe atakapochapwa na TEZI DUME ndipo utakapoona madhara ya hiyo "statement" ya Pompeo. Utarudi hapa na kulia lia tu.
..njia rahisi zaidi ni kuishi vizuri na jumuiya ya kimataifa.
..hivi kuna ubaya gani kwa vyombo vya dola na tume ya uchaguzi kutenda HAKI sawa kwa vyama vyote vya siasa?
..2015 tulipoharibu uchaguzi wa Znz Wamarekani walitukatia msaada wa program yao ya MCC.