Marekani kupigana vita na China 2025, Jenerali wa Marekani bw. Mike

ASIWAJU

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2022
Posts
1,938
Reaction score
1,632
Jenerali wa jeshi la anga la Marekani Bw. Mike Minihan ameliandikia ujumbe jeshi la Marekani kuwa tayari kwa ajili ya kupambana na China mwaka 2025.

Vyanzo vya habari:
Screenshot_20230130-093746.jpg
Screenshot_20230130-093856.jpg
Screenshot_20230130-093800.jpg
Screenshot_20230130-093506.jpg
Screenshot_20230130-093615.jpg

Swali kutoka kwa lieutenant katika jeshi la marekani hili hapa :
Screenshot_20230130-093359.jpg

Maswali yangu:
1. Ipi ni athari kubwa ya ujumbe wa jenerali huyu kwa Marekani na China?

2. Yapi ni matokeo ya ujumbe huu katika siasa za kimataifa kati ya China na Marekani?

3. Je tutegemee kuona mgogoro mkubwa katika Indo- Pasific?

Karibuni kwa maoni yenu na maswali ya ziada.
 
Hayo ni maoni binafsi ya huyo General. Kasema hisia zake zinamtuma hivyo, foreign policy haiendeshwi na hisia za mtu mmoja hata angekuwa ndiye Rais wa Marekani.

Na China hawashangai juu ya hilo, nani asiyejua jeshi la Marekani linajipanga kuikabili China. Kila mwaka Pentagon hutoa assessment na kuelezea advancement ya jeshi la China. China hawakurupuki kwenye sera zao za kigeni, wanaonekana wapole kwa nje ila muda wao kuonyesha ubabe bado.

Huwa naona it's very likely Marekani kuanzisha vita na China kuliko kuanzisha na Urusi. Na vilevile uwezekano wa China kuishambulia Russia ni mkubwa kuliko kuishambulia Marekani.
 
Kwamba China ishambulie Urusi aisee sio lazima ukoment ili upunguze kujiaibisha.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Hayo ni maoni binafsi ya huyo General. Kasema hisia zake zinamtuma hivyo, foreign policy haiendeshwi na hisia za mtu mmoja hata angekuwa ndiye Rais wa Marekani.
Lakini maoni yake sidhani kama ni bora katika diplomasia ya haya mataifa mawili makubwa ukizingatia kuwa yeye ni high ranked general katika jeshi la taifa la marekani.
Na China hawashangai juu ya hilo, nani asiyejua jeshi la Marekani linajipanga kuikabili China. Kila mwaka Pentagon hutoa assessment na kuelezea advancement ya jeshi la China. China hawakurupuki kwenye sera zao za kigeni, wanaonekana wapole kwa nje ila muda wao kuonyesha ubabe bado.
Ni kweli jeshi la marekani lina jiandaa kuikabili China katika swala la Taiwan licha ya kuwa China hawa kurupuki katika hilo lakini je jumbe kama hizi za majenerali wa marekani haziwezi kufanya China kubadili hiyo Operation yake anayo panga kufanya hapo Taiwan kwa kupeleka muda mbele au kurudisha muda nyuma wa kuanza ?
Huwa naona it's very likely Marekani kuanzisha vita na China kuliko kuanzisha na Urusi.
Kwa nini mkuu?
Na vilevile uwezekano wa China kuishambulia Russia ni mkubwa kuliko kuishambulia Marekani.
Kwa nini China aishambulie Russia wakati wapo upande mmoja na sio Marekani?
 
Wenzetu hawakurupuki kuropoka kama yule wa Uganda, huenda kuna oda alipewa na wakuu ili akamilishe baadhi ya mambo ya kijeshi kwa ajili ya kuingia mzigoni.

Wenzetu hawakurupuki kwamba mmegombana leo au kutofautiana mtazamo basi asubuhi unatupa maguruneti, ni mipango ya muda ili kujua mwenzako ana nini na wewe uzalishe au kuagiza nini ili umvae.
 
Hayo ni maoni binafsi ya huyo General. Kasema hisia zake zinamtuma hivyo, foreign policy haiendeshwi na hisia za mtu mmoja hata angekuwa ndiye Rais wa Marekani.
Na China hawashangai juu ya hilo, nani asiyejua jeshi la Marekani linajipanga kuikabili China. Kila mwaka Pentagon hutoa assessment na kuelezea advancement ya jeshi la China. China hawakurupuki kwenye sera zao za kigeni, wanaonekana wapole kwa nje ila muda wao kuonyesha ubabe bado.

Huwa naona it's very likely Marekani kuanzisha vita na China kuliko kuanzisha na Urusi. Na vilevile uwezekano wa China kuishambulia Russia ni mkubwa kuliko kuishambulia Marekani.
Nimesoma maelezo yako umeelezea vizuri Sana. Ila hapo uliposema "uwezekano wa China kuishambulia Russia ni mkubwa kuliko kuishambulia Marekani". Naomba ufafanuzi. How?

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Wenzetu hawakurupuki kuropoka kama yule wa Uganda, huenda kuna oda alipewa na wakuu ili akamilishe baadhi ya mambo ya kijeshi kwa ajili ya kuingia mzigoni.

Wenzetu hawakurupuki kwamba mmegombana leo au kutofautiana mtazamo basi asubuhi unatupa maguruneti, ni mipango ya muda ili kujua mwenzako ana nini na wewe uzalishe au kuagiza nini ili umvae.
Marekani hawezi thubutu kuingia vitani na China, angekuwa na hizo guts angeshaipiga Iran siku nyingi.
 
Kwamba China ishambulie urusi aisee sio lazima ukoment ili upunguze kujiaibisha.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Huwezi elewa kwa vile umejifungia akili. USSR na China waligombea mipaka miaka ya 1960s mwishoni hadi vifaru vilihusika na watu walikufa kwenye mapigano ya rasharasha kwa miezi zaidi ya mitano. Baadaye ndio wakasaini ceasefire na kurudia mipaka ya zamani, walikuja kusaini makubaliano kumalizana na madai 2008 au 2009 kama sikosei.

Wakati China ikiwa weak enzi za dynasties kina Qing na Ming na wengine pale Russia ilichukua maeneo kadhaa na ilikiuka mikataba ya mipaka. Miaka mingine maeneo yalichukuliwa, mji wa Vladivostok pale Russia ni eneo la China lile. Waulize Wachina wakwambie Outer Manchuria ni nini, eneo lote la Russia lililoibiwa kutoka China wanaita hivyo.

Mapigano kati ya Russia/USSR na China yametokea kwenye mipaka yao ila mapigano kati ya Marekani na China hayajatokea kwenye mipaka. Kwenye WW2 Marekani ilifanya airlifting campaign "The Hump" kuipa silaha China ipigane na Japan. Zilipitia India na kuvuka nyanda za milima mikali kukwepa eneo la Manchuria lililokaliwa na Japan.

China na Marekani ni wagomvi kimaslahi na kuishawishi, ila China na Russia ni mgogoro wa mipaka ambao ni frozen na mgogoro wa mipaka huwa haufi kirahisi. Ugomvi wa China na Marekani ni baada ya WW2, ila China na Russia wana fujo zao since 1800s uko.
 
Wapigane tu! Ingawa najua wababe hao wa dunia wakinyukana madhara mpaka sisi wanyonge tutayapata.
 
Lakini yake sidhani kama ni bora katika diplomasia ya haya mataifa mawili makubwa uliizingatia kuwa yeye high ranked general katika jeshi la taifa la marekani.

Ni kweli jeshi la marekani lina jiandaa kuikabili China katika swala Taiwan licha ya kuwa China hawa kurupuki katika hilo lakini je jumbe kama hizi za majenerali wa marekani haziwezi kufanya China kubadili hiyo Operation yake inayo panga kufanya hapo Taiwan kwa kupeleka muda mbele au kuirudisha muda nyuma wa kuanza ?

Kwa nini mkuu ?

Kwa nini China aishambulie Russia wakati wapo upande mmoja na sio Marekani ?
General hajaambia waandishi wa habari wala hajayasema maneno yale in public. Kulingana na elimu yake, uzoefu, cheo na intelligence anayoweza access amefanya prediction muda wa vita ya Marekani na China ni 2025 na hapo ndio akaandika memo kwenda kwa maofisa. Alichokifanya ni kazi yake, kawaambia wanajeshi ambayo ndio kazi yao hiyo kukaa chonjo dhidi ya adui.

Hayo yangesemwa na Defence Secretary kwenye press conference ndio ungekuwa utata. Na uzuri wa US kuna uhuru wa habari hata memo ya siri inavuja na watu wanahoji au kuripoti. Hata China na Russia wanafanya assesment vizuri na kutoa mapendekezo ila hayatajwi hadharani.
Sio suala la kuiogofya China hili. Sio classified materials zile, memo ya mawazo ya mtu.

Na hiyo Taiwan haivamiwi kirahisi kama watu tunavyofikiria. Nchi inayotengeneza 40% ya microchips duniani sio ya kizembe na akili zao hazijalala hivyo na udogo wake. Na imezungukwa na maji, unahitaji one of the biggest naval landing operation kuwavamia fukwe zao zile na kusalimika anti ship missiles zao kwa kiasi fulani, sacrifice ya asilimia kadhaa ya kikosi cha kuvamia. Taiwan sio nchi ya China kupanga leo na ikavamia siku tatu zijazo, inahitaji wiki za maandalizi ambazo surveillance itaonyesha maandalizi hayo na Marekani itahamisha Pacific fleet kuja kazini (probability ni kubwa Marekani kuingilia kati)

Ili Marekani ichelewe kuingia Taiwan inabidi China iwe na navy kubwa kuliko sasa jambo ambalo wanakuja kasi, ila iwe na logistics nzuri zaidi. Pia Marekani ikomae kwenye microchips industry ijitosheleze ili isiogope source ya Taiwan kupotea. Yakitokea hayo mawili China inaweza vamia haraka ikapigana siku chache na kuingia Taiwan kukutana na resistance ya army kisha Marekani ikachelewa kurespond baadae ikaona haina haja sana kupigana na China (kama umuhimu wa Taiwan kwake umepungua). Hii scenario inategemeana ila inategemea ubeti kitu kimoja muhimu, response ya Marekani.

Ni maoni yangu
 
Wenzetu hawakurupuki kuropoka kama yule wa Uganda, huenda kuna oda alipewa na wakuu ili akamilishe baadhi ya mambo ya kijeshi kwa ajili ya kuingia mzigoni.

Wenzetu hawakurupuki kwamba mmegombana leo au kutofautiana mtazamo basi asubuhi unatupa maguruneti, ni mipango ya muda ili kujua mwenzako ana nini na wewe uzalishe au kuagiza nini ili umvae.
Ujumbe huu hauwezi kuwa na athari kubwa kwa U.S.A?
 
Marekani katafuta kibonde wa kumtolea matamko na kumtisha kwa vita ,angesema hivyo kwa Russia uone mchezo kama haujezwa mwaka huu.

Tuacheni masihara Russia anaogopwa sana na Marekani na hiyo ni kutokana na kwamba Marekani anaijua Urusi na anajua anateknolojia za Siri mno.

Mmarekani kwa Mchina: Marekani itapigana na china 2025

Mmarekani kwa Mrusi: Russia sio taifa la kulichezea na uamuzi wa kupigana ni Urusi ni kutotumia akili
 
Unazungumzia Urusi hii hii inayopigana na Ukraine mwaka mzima kwa silaha za kuomba omba kutoka kwa nchi za Ulaya na Marekani ama kuna Urusi nyingine nje na hii?.
 
Huwezi elewa kwa vile umejifungia akili. USSR na China waligombea mipaka miaka ya 1960s mwishoni hadi vifaru vilihusika na watu walikufa kwenye mapigano ya rasharasha kwa miezi zaidi ya mitano. Baadaye ndio wakasaini ceasefire na kurudia mipaka ya zamani, walikuja kusaini makubaliano kumalizana na madai 2008 au 2009 kama sikosei.

Wakati China ikiwa weak enzi za dynasties kina Qing na Ming na wengine pale Russia ilichukua maeneo kadhaa na ilikiuka mikataba ya mipaka. Miaka mingine maeneo yalichukuliwa, mji wa Vladivostok pale Russia ni eneo la China lile. Waulize Wachina wakwambie Outer Manchuria ni nini, eneo lote la Russia lililoibiwa kutoka China wanaita hivyo.

Mapigano kati ya Russia/USSR na China yametokea kwenye mipaka yao ila mapigano kati ya Marekani na China hayajatokea kwenye mipaka. Kwenye WW2 Marekani ilifanya airlifting campaign "The Hump" kuipa silaha China ipigane na Japan. Zilipitia India na kuvuka nyanda za milima mikali kukwepa eneo la Manchuria lililokaliwa na Japan.

China na Marekani ni wagomvi kimaslahi na kuishawishi, ila China na Russia ni mgogoro wa mipaka ambao ni frozen na mgogoro wa mipaka huwa haufi kirahisi. Ugomvi wa China na Marekani ni baada ya WW2, ila China na Russia wana fujo zao since 1800s uko.
Ugomvi wa kimipaka China anao dhidi ya mataifa mengi sana ikiwemo Turkey,India, Mongolia, Vietnam, Russia, Japan n.k na urafiki wa China na Russia umetokana na falsafa ya kikomunisti iliyo waunganisha na wakomunisti wa CPC walipo kuwa wanasaka ukombozi licha ya kuwa miaka ya mbeleni wakati wa Mao ugomvi ulizuka tena.

Urafiki wa China na Russia ni urafiki wa kimashaka kwa pande zote mbili, lakini je kwa sasa ugomvi mkubwa upo wapi Je ni China na Russia au ni China na U.S.A ? Ukizingatia na huo ujumbe wa general Mike ?

Lakini mkuu tunapaswa kukumbuka pia kuwa China na U.S.A haita kuwa mara ya kwanza kukumbana katika mgogoro/Vita moja tuki refer Korean na Vietnam wars.
 
Back
Top Bottom