1. Russia alisema atakayemsaidia Ukraine atakutana na mkono mzito, kila leo misaada inaenda Ukraine. Kwanini Russia asimchape US?
2. Biden alisema Russia akiivamia tu Ukraine wanalipua bomba la mafuta, na ni kweli US aliripua hilo bomba.
US tusimchukulie wa mchezo mchezo. Mtu ambae kila kona ya dunia yupo ameweka base, na takribani miaka 50 sasa kila mwaka ana vita na operations kibao anazifanya, jamaa yupo vizuri.
Sasa hivi amekiwasha huko Ukraine. Na bado vile vile alikuwa tayari kukiwasha Taiwan dhidi ya China. Nitajie mjinga gani hapa duniani anaweza akawa na guts kama hizi?.
Leo hii Iran, S.Korea pawake moto, unafikiri Russia anaweza kunyanyua miguu yake kuwasaidia hao? Lakini US anaweza akapambana huko Ukraine, Taiwan pia akapeleka misaada, na bado uko Korea au Japan kukinuka akapeleka misaada na majeshi kupambana.
Nenda google, bajeti ya ulinzi ya US, chukua bajeti za ulinzi z UK German France, China, Russia, Canada n.k zijumrishe kwa pamoja na hawafiki nusu ya bajeti ya ulinzi jamaa.