Ugomvi wa kimipaka China anao dhidi ya mataifa mengi sana ikiwemo Turkey,India, Mongolia, Vietnam, Russia, Japan n.k na urafiki wa China Russia umetokana na falsafa ya kikomunisti iliyo waunganisha wakomunisti wa CPC walipo kuwa wanasaka ukombozi licha ya kuwa miaka ya mbeleni wakati wa Mao ugomvi ulizuka tena.
Urafiki wa China na Russia ni urafiki wa kimashaka kwa pande zote mbili, lakini je kwa sasa ugomvi mkubwa upo wapi Je ni China na Russia au ni China na U.S.A ? Uliizingatia na huo ujumbe wa general Mike ?
Lakini mkuu tunapaswa kukumbuka pia kuwa China na U.S.A haita kuwa mara ya kwanza kukumbana katika mgogoro/Vita moja tuki refer Korean na Vietnam wars.
Mkuu hapo kwenye Korean wars. China hataki kabisa Marekani amsogelee zaidi, China anazungukwa na bases za Marekani na washirika wake kina South Korea, Japan na Taiwan kisha anazungukwa na adui wakubwa wa Marekani hao Russia na North Korea. Hivyo China anakuwa karibu na Marekani kwa namna mbili, sasa hataki kuzungukwa kuzidi. Ndio maana kufa na kupona atahakikisha North Korea iko chini ya influence yake, jaribio lolote la kuleta demokrasia ndani ya North Korea ni kuifanya ifunguliwe duniani na kuwa wazi kwa mataifa ya kigeni ikiwemo Marekani. China ndio maana alikomalia North Korea kwenye vita ile, na hata sasa inamsaidia Kim Jong kiusalama, kifedha na kukwepa sanctions ya vitu muhimu. Ikitokea North Korea imepigwa na Marekani majeshi yakakaa hapo kutakuwepo na build up ya Marekani kujipanga dhidi ya Russia na China kwa vile N. Korea ina land border na nchi hizo mbili. China na Russia wako tiyari kulipa gharama yoyote N. Korea ikae hivihivi, waliipotezea South Korea si unaona hakuna land border nao
Urafiki wa Russia na China ni "the enemy of my enemy is my friend" hauna nguvu sana kama tunavyodhani. Kadri siku zinavyoenda Russia anapungua vitu vya kuoffer kwa China. China kafanya reverse engineering na licence production ya silaha za Urusi kamaliza sasa yuko na concepts zake mpya, kashapata kila kitu kwa Urusi kama nuclear program na fighter jet ila kanyimwa jet engine technology ambayo sioni kama atakaa hii miaka mitano bila kuwa sawa na Russia.
Haya mataifa yapo kimaslahi, ukikosa umuhimu unachukuliwa kawaida. Miaka ya 1980s Marekani iliiuzia Black Hawk helicopters China na ikaisaidia kutengeneza J-8 fighter jet hapo Wachina wakiwa na mawazo muda wowote vita na USSR itaanza. Na miaka hii, Russia inaiuzia silaha India wakati huo inaziuza kwa China tena na hao wawili ni maadui. Kinachowaweka pamoja China na Russia ni tishio la Marekani, sio upendo wao. China angalau inataka mshirika anayejiweza ila wale sio kufa na kupona kwamba ukivamia Ukraine nakuunga mkono, China inafanya assessment yake indepently inatafuta maslahi yake.
Na China kugombana na majirani ni sawa na Russia. Ila China kuamua sasa ifanye uvamizi kwa Marekani ni sawa na hakuna, wanagombea nini? Labda iwe preemptive strike.
At the right time China inazo sababu za kuivamia Urusi, haikutokea tu kwamba Urusi ina uwanda wa Siberia mkubwa vile.
Na Marekani ina uwezo wa kubadilisha adui kuwa rafiki ndani ya muda mfupi sana, inavyo vitu vya kuoffer. Na inaweza mfanya rafiki awe adui umuhimu wake ukiisha. Russia iliiuzia Marekani ile Alaska kipindi kile Uingereza na Marekani ni maadui wakubwa