Marekani na mataifa mengine ya magharibi yaiwekea vikwazo mbalimbali vikiwemo vya kiuchumi nchi ya Urusi

Wapuuzi hawa wanajua kabisa vikwazo vinaathiri dunia nzima
Leo London mafuta ya gari yameishapanda na bahati jana nilijaza ila yataisha na hayo yanasubiri

Msifurahie sana Sanctions maana hata nyie nyumbani yanakuja lazima msifikiri mko mbali au mmejifungia na maisha yenu

Wote tutaimba wimbo mmoja tu awe mweupe, mweusi na hata njano
 
Wewe uko kwenu buchosa au kibondo huko unasimama na ukraine kwani wanakujua wewe kula ugali wako ulale
Oyaaa, wa Kibondo tuna akili nyingi, hatuwezi kuwa kama huyo tengua kauli yako kwanza in the name of Putin
 
Kusota ni pande zote 2 acha mziki wa kukosa gesi waanze kuupata huko ulaya hasa ukija msimu wa baridi na kumbuka ukraine pia alikua anailisha ulaya magharibi kwa asilimia kubwa......hio inflation haitaiacha serikali yeyote salama huko
😃😃😃
Aisee
 
Putin is unstoppable
 
Kama walimuwekea vikwazo Magufuli na Makonda alafu Tanzania ikaingia uchumi wa kati watamuweza Putin?

Tanzania haijawahi kuwekewa vikwazo vya kiuchumi. Ni makonda alizuia kuingia marekani. Fikiria hatuna vikwazo lakini tozo kwenda mbele, siku marekani pekee akituwekea vikwazo wewe mwenyewe utaona mabadiriko.
 
Tanzania haijawahi kuwekewa vikwazo vya kiuchumi. Ni makonda alizuia kuingia marekani. Fikiria hatuna vikwazo lakini tozo kwenda mbele, siku marekani pekee akituwekea vikwazo wewe mwenyewe utaona mabadiriko.
Mkuu unaijua kweli historia ya Tanzania mpaka unasema hatujawahi kuwekewa vikwazo.
Unafikiri kufeli kwa ujamaa ulitokea kwa sababu ya mismanagement ya Watanganyika tu.
Walitupiga vikwazo vya kufa muda wa miaka kumi mpaka National team ya mpira ikawa inacheza kidali wazi
 
Kwa mtazamo wa karibu , athari ya vikwazo huwezi iona lakini!!mwisho wa siku ni lazima tu uchumi wako utaathirika tu, na hasa kwa wananchi wako!! Mfano awekewe vikwazo vya kutotumia dola ya US, pauni, na euro, hiyo athari yake ni kubwa sana!!
Usisahau nusu ya Ulaya gas inatoka Russia ambayo ni cheap ndio sababu kwa nini ujerumani haiingii kwa nguvu.

Ukiiwekea vikwazo Russia ni kama umeiipiga vikwazo Ulaya[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Croatia na Hungary zimeshasema vita haiwahusu wataendelea kushirikiana na Urusi kama kawaida.

Ufaransa anakumbuka maumivu ya kugeukwa na Marekani kwenye mradi wao wa submarine na Marekani na Uingereza kuhusu Australia yupo neutral.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…