Marekani na Uingereza wafanya mashambulizi dhidi ya Kikundi cha Houthi nchini Yemen

marekani ametumia hadi submarines kupigana na wahouth !? Sasa ziara ya waziri wa mambo ya nje wa marekani huko mashariki ya kati ilikuwa na lengo gani wakati marekani na washirika wake ndio wanazidisha kuupanua mgogoro wa mashariki ya kati? Marekani ni mwoga sana sasa akae mkao wakutulia asubiri majibu makali
 
Shida unachanganya mambo. Hakuna taifa linaloishambulia Yemen kwani ni kanchi kamaskini ka kiarabu ila kufunga kwao shughuli za Baharini ndio kilichosababisha haya.

Juzi nilimsikia Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(PTA) akielezea madhara yanayosababishwa na hao Hauth kwenye uchumi wa Tanzania kwa kuzuia na kushambulia meli zinazopita ukanda huo. Hii ni sawa, waache kushambulia meli za mizigo na kufanya uharamia wa Baharini kwani madhara yake ni makubwa kwenye uchumi wa Duniani.
 
Wakawashambulie na warusi kama wanaume maana wanaingamiza Ukraine
 
huo ndo uthibitisho wako kua meli imelipuliwa/imezamishwa?
umeenda mtandaoni kuokota picha ya mwezi Desemba 2023 una kuja kuihusisha na tukio ilo lililo tokea leo? kijana una akili kweli wewe??
 

Attachments

  • Screenshot_20240112-061903_Chrome.jpg
    190.1 KB · Views: 2
third world war itatokea kabla ya mwaka 2030
Tangu 1990 ikitokea hata mvua ikanyesha sana na kusababisha mafuriko watu wanakimbilia kusema third world war inakuja. Ikaja vita ya Ghuba, watu wakadai third world war, September 11 US aliposhambuliwa watu wakadai third war. Wanafunzi wa Tambaza walipokua wakifanya vurugu miaka ile, watu wakadai third war inakuja.

Yakaja ya Ukraine na Russia, Israel na Hezbollah, Israel na Hamas, Syria kote huko watu mnakimbilia kudai World war inakuja.

Hii imeshakuwa chiboko sasa, leo hii wanashambuliwa maharamia na migambo ya Houth mnadai lazima World War ije!! Ikiwa Russia kaingizwa vitani jumla jumla hata kutishia kutumia nuclear lakini mpaka sasa nchi pekee inayoonekana kuwa naye bega kwa bega ni Belarusi pekee, ingawa hata yenyewe haijapeleka wanajeshi sasa leo ndiyo iwe hicho kikundi cha Houth? Russia na ukubwa wake, na 'ushawishi' kaishia kuungwa mkono kwa katuni za kuchorwa tu,na kashindwa kusababisha third world war, ndiyo leo ikaanzie na houth?
 
Jipe moyo ni tiba ya stress ewe kikongwe
 
Haya we kaa mkao wa kula usubiri habari kutoka America wakikiri wamezamishiwa meli yao
 
Hiyo ziara alilenga kuongea na magaidi ya Houthi?
Tulieni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…