Marekani: Spika wa Bunge, Nancy Pelosi anaweza kusababisha vita kali kati ya China na Marekani

Marekani: Spika wa Bunge, Nancy Pelosi anaweza kusababisha vita kali kati ya China na Marekani

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Hiki kibibi ambacho kimekaribia kuhitimisha maisha yake hapa duniani kinaweza kusababisha maelfu ya watu wakiwemo watoto na vijana kufariki kama kitaendelea na chokochoko chake cha kulazimisha kuingia Taiwan kinyume na matakwa ya China ambayo ndiyo mmiliki halali wa Taiwan. China ilishaionya Marekani kuwa kama kibibi hicho (Nancy Pelosi) kitaamua kutaka kuingia Taiwan kinguvu basi Marekani itakuwa inataka kuchezea moto na lazima itaungua. Tishio hilo liliifanya Ziara ya Pelosi kutokuwa na kituo cha Taiwan kwenye ziara yake ya mashariki ya mbali.

Cha kushangazwa leo jioni Marekani imetangaza kuwa anatazamiwa kuingia Taiwan kesho jumanne!! China imesema imeziagiza ndege zake kukesha zikikizunguka kisiwa cha Taiwan kuhakikishga kuwa Pelosi hatii mguu wake Taiwan!! Marekani imesema inaelekeza meli zake zilizoko karibu na maeneo hayo zielekee huko ili kumlinda Pelosi!! Sijui hili picha litaishaje, lakini waswahili walisema mzaha mzaha hutumbua usaha1! Wote Pelosi na Biden ni wazee na hawana kiu kubwa sana ya kuendelea kuishi lakini kiburi cha kutaka kuonesha umwamba dhidi ya China inaweza kupelekera vita ya tatu ya dunia!! Mungu aepushe balaa hilo!!

Pelosi to visit Taiwan – CNN​

The top US official will be staying overnight in Taipei, the news network reports
CNN has confirmed from sources both in the US and in Taiwan that US House Speaker Nancy Pelosi plans to visit the self-governed island this week, despite objections from Beijing, which considers the island part of its territory.

A Taiwanese official said that Pelosi is expected to spend the night in Taiwan, but didn’t offer any details about the time of her expected arrival. A US official said the Pentagon was “working around the clock” to ensure the speaker's safety. Both spoke on condition of anonymity.

Maoni yangu: Marekani anatishia tu wala Pelosi hatothubutu kuingia Taiwan. Ikitokea kweli Pelosi akaingia Taiwan na China ikaingia baridi kutekeleza kitisho chake, China itadharaulika mbele ya dunia na mbele ya Marekani milele!! Japo China kukubali kudharaulika ndio itakuwa wokovu wa dunia kuepushwa na vita kuu ya tatu kwa sasa!!

1659374062867.png

Kibibi hicho kinataka kuiletea balaa wakati chenyewe kimeshaifaidi dunia kwa miaka 82!!



1659374274704.png

Kibabu Biden cha miaka 79 chenyewe kimeshaifaidi dunia kwa miaka 79 kinataka kuleta kizazaa duniani kisababishe watoto wadogo na vijana kwa maelfu wapoteze maisha ili mradi tu kionekane kibabe mbele ya China!! Dunia ikipinge hiki kibibi na hiki kibabu kwa nguvu zote!! Wawaache na wenzao wafikishe ile miaka waliyofikia wao!!
 
Ila ninachokiona hapa ni kuwa Marekani haamini kama China anavyotishia kuuwasha moto anamaanisha, Marekani inaamini kuwa China inachimba mkwara tu na haitothubutu kumzuia kinguvu Pelosi kuingia Taiwan!! Hali kadhalika China haiamini kuwa ni kweli Marekani imekusudia kumpeleka Pelosi Taiwan ila inachimba mkwara tu. Itafikia kila mmoja ataona kuwa kumbe kila mmoja anamaanish!! Ikifikia hapo mchokozi Marekani atafyata mkia na kurudi nyuma!! Lakini kabla hajarudi nyuma atachimba mkwara mmoja mzito sana na akiona China haijatishiwa na mkwara huo fasta marekani itaufyata halafu itatafuta njia ya kujikosha ili kupunguza aibu ya kuufyata!! Mahali walipofikishana, yeyote atakayeufyata atapambana na fedheha na aibu, iwe Marekani, iwe China!! Ila Marekani mchokozi sana, amesafiri maelfu ya maili kwenda kuleta ugomvi nyumbani kwa watu!!
 
Back
Top Bottom