Marekani wanasumbuliwa na Umasikini sio Ubaguzi


Kweli mkuu ujawah kufika marekani.

Marekani watu wanamiliku mashamba makubwa tu mkuu.
Hata ngoombe wanafugwa pia kuna viwanda vya kuchinja nyama ya ngonbe pia.

Chakula cha $ 100 unaweza kutumia hata wiki mbili,alafu wanakuambia hivi kama kipato chako hakitoshi unaruhusiwa kuomba kadi ya chakula watakupa unakuwa unatumia kadi hautolipa hela yako.

Kama huwezi kulipia nyumba kuna nyumba za serekali wanakupa unaweA kuwa unalipa $ 100 au 200 kila mwez

Hata kwenye swala la matibabu ni hivyo ,binafsi nilienda hospitali kufanyiwa upasua wa sikio nilitakiwa nilipe $elfu 17.
Lakin kuna mashirika ya kusaidia kama huna uwezo wa kulipa,pesa hiyo nililipiwa yote na wakaongeza nyingine.natiwaga bure tu.

Sasa hapo unataka nini?

Hayo mambo tanzania lini mkuu?
 
Why wanaiba vitu?
 
Hivi unaujua umasikini wa watanzania kweli ?

Narudia tena unawajua wabongo walivyo choka mbaya ?

Hivi unajua mpaka sasa walimu wa shule ya msingi wanalipwa Tsh 340,000 ( USD 150 ) Gross kwa mwezi ?

Kukaa Kimya Mnadhani Wabongo Wanaishi PEPONI ?
Mtanzania anayelipwa USD 150 per month akiwa Tanzania ni Afadhari kuliko mmarekani anayeishi Newyork analipwa USD 1500 inaishia kwenye pango, usafiri na chakula.
 
Hata wewe mkuu Mungu angekupa dunia iwe mali yako ungeona haitoshi ungetaka uchukua sayari nyingine.

Mambo ya kawaida tu mwanadamu hatosheki
Umeachishwa kazi...unahitaji kulipa bills, kodi ya nyumba, chakula n.k...unaishi jiji kubwa!! USD 700 weekly inakupeleka wapi?
 
Mtanzania anayelipwa USD 150 per month akiwa Tanzania ni Afadhari kuliko mmarekani anayeishi Newyork analipwa USD 1500 inaishia kwenye pango, usafiri na chakula.

Marekani ikiwa pesa yako inaishia kwenye pango na chakula.
Serikali iko kwaajili yako.

Mfano unalipwa $ 1500 fanya hivi
Apply nyumba ya serikali kila mwezi utakuwa unalipa $ 200

Apply kadi ya chakula kila mwezi watakuwa wanakupa $ 200

Gharama yako ni nyumba tu.
 

Acha uongo.. Marekani maskini anamiliki vipi shamba au ardhi.. Tanzania mtu hana hata mia lakini ana shamba lake la kulima .

Tanzania kila ukoo una shamba.. kila familia ina shamba kijijini kwao...je usa ardhi inapatikana kiurahisi kama Tanzania
 
Umeachishwa kazi...unahitaji kulipa bills, kodi ya nyumba,chakula n.k...unaishi jiji kubwa!! USD 700 weekly inakupeleka wapi?

Mkuu $700 kwa wiki unaniambia inakupeleka wapi?.

Tufanye hivi:
Kodi ya nyumba nalipa $600 kwa mwezi

Umeme $40
WI FI 50
Chakula200

Jumla kama 890 kwa mwezi

Turudi sasa
700 x 4=$2800
2800-890= 1910 hiyo ndio pesa unaweka akiba
 
Ninavyojua Mimi, Huko US Kama wewe ni raia wa nchi ile ufanye kazi usifanye kazi huwezi kukosa chakula Wala kulala nje kwenye mtaro labda uamue mwenyewe kuishi kwenye mtaro otherwise Kodi ya nyumba haiwezi mfanya raia wa US aishi mtaroni
 
Ndio maana nimekwambia kuna umasikini kama hakuna kwanini watu wapewe misaada? na watu wenye stress ni wale wanaopewa pesa! Yaani watu wasio na maisha magumu wanapora supermarket!
 
Acha uongo.. marekani maskini anamiliki vipi shamba au ardhi.. Tanzania mtu hana hata mia lakini ana shamba lake la kulima .

Tanzania kila ukoo una shamba.. kila familia ina shamba kijijini kwao...je usa ardhi inapatikana kiurahisi kama Tanzania

Kuwa na shama si kigezo cha wewe umemzidi mtu anaeshi marekani.watu wa dar wengin hawana mashamba lakini wana maisha mazuri kuliko hao ambao wana mashamba vijijini.

Mfumo wa marekani ukiwatowa watu katika umaskini na kuwafanya watu kuwa sawa na ndomana hata mtaani uwezi kumjua alienacho na hasiekuwanacho.

Kama huna huakika wa kula kuna kadi serekali inakupa uwe unanunua chakula.je tanzania yapo?

Kama huwezi kulipa nyumba kisa kipato kidogo serekali inakupa nyumba utalipa kidogo je tanzania vipo?

Istoshe kila mwaka watuwanalipwa tax zao,kuna watu wanapa hata dollar elfu 18 kila mwaka je tanzania hayo mambo yapo?.

Wasukuma wanagoombe nyingi lakini bado wanaishi katika mzingira magumu.
 
Ndio maana nimekwambia kuna umasikini kama hakuna kwanini watu wapewe misaada? na watu wenye stress ni wale wanaopewa pesa! Yaani watu wasio na maisha magumu wanapora supermarket!

Ni msaada ni wajibu wa serekali kwa raia wake maana wanalipa kodi na serekali inawajibika kuwahudumia.

Nimekuambia mkuu hata wakupe dunia utatamani upewe na mars pia
 
Point yako nini mkuu.
Uliishi marekani kwa muda gani?
Anae mwita mwenye gunia 10, mashamba na ng'ombe kuwa maskini ni haki. Ana umasikini wa akili, wa kushindwa kupanga kuzitumia raslimali alizonazo kutajirika. Ana mashamba na unasema ana gunia 10, mkulima wa USA hecta 1 ya mahindi anatumia mbolea mifuko 6 na anavuna gunia zaidi ya 40! Tanzania tu maskini wa uongozi, wa kushindwa kusimamia mipango ya maendeleo na kukwamisha mipango binafsi ya wananchi kwa kuweka mizengwe na utitiri wa kodi kwa kila utalojaribu kufanya.
 
Hivi unaujua umasikini wa watanzania kweli ?

Narudia tena unawajua wabongo walivyo choka mbaya ?

Hivi unajua mpaka sasa walimu wa shule ya msingi wanalipwa Tsh 340,000 ( USD 150 ) Gross kwa mwezi ?

Kukaa Kimya Mnadhani Wabongo Wanaishi PEPONI ?
Mshahara wa serikali upo juu na hasa ukilinganisha na muda unaotumika kufanya kazi. Watumishi wa umma muda wanaotumia kufanya kazi ni mdogo mno. Kutoka kazini kwenda shughulikia maswala nje ya kazi kama vile kunywa chai, chakula, benki nk na anaetaka huduma kuambiwa asubirie, aje baadae au kesho ni jambo la kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…