Marekani wanasumbuliwa na Umasikini sio Ubaguzi

Marekani wanasumbuliwa na Umasikini sio Ubaguzi

Hivi unaujua umasikini wa watanzania kweli ?

Narudia tena unawajua wabongo walivyo choka mbaya ?

Hivi unajua mpaka sasa walimu wa shule ya msingi wanalipwa Tsh 340,000 ( USD 150 ) Gross kwa mwezi ?

Kukaa Kimya Mnadhani Wabongo Wanaishi PEPONI ?
Kumbe ukiwa bongo ukawa na kipato cha dollar 1000,uko vizuri eeh
 
Hivi US mtu wa kawaida anaweza miliki shamba angalau heka 5? au anaweza fuga n'gombe? bongo mtu anaweza kuwa anaingiza 10,000 kwa siku anaenda sokoni ananunua kila kitu na anabaki na akiba ya 5000, US mtu analipwa dollar 75 Au 100 kwa siku akienda super market pesa yote anaacha kule nani mwenye maisha magumu?
Kumbe ukiwa bongo una kipato cha dollar 1000 uko vizuri eeh
 
Hivi US mtu wa kawaida anaweza miliki shamba angalau heka 5? au anaweza fuga n'gombe? bongo mtu anaweza kuwa anaingiza 10,000 kwa siku anaenda sokoni ananunua kila kitu na anabaki na akiba ya 5000, US mtu analipwa dollar 75 Au 100 kwa siku akienda super market pesa yote anaacha kule nani mwenye maisha magumu?
Look at another side of coin bro. Simu unayotumia USA unajua ni half of the price uliyonunua.

Nguo unazovaa mpaka usubir wazungu wavae wachoke ndyo uvae wewe alafu unasema wao maskini.

Magari mnayonunua wao wanatumia yakifikisha km za kuwa recycled mnaletewa huku bongo na mnalipia tax 100% ya bei uliyoagizia. Alafu unakuja unasema USA masikini sana.

ARVs mnasubiri msaidiwe na USA. Serikali zenu haziwezi kununua ARVS wala raia wenu hawawezi kununua ARVS.

Watanzania hamna hata uwezo wa kutarii mbuga zenu za wanyama mnalilia mabeberu ndyo waje kutalii alafu mnasema nyie matajiri.

Ukipita kila kona unakutana na Mabango ya " kwa msaada wa watu wa marekani" then bila aibu mnasema nyie matajiri kuliko USA? Nenda USA unitaftie bango linalosema " kwa msaada wa watu wa Tz", nitembee uchi mwaka mzima.
 
Kweli mkuu ujawah kufika marekani.

Marekani watu wanamiliku mashamba makubwa tu mkuu.
Hata ngoombe wanafugwa pia kuna viwanda vya kuchinja nyama ya ngonbe pia.

Chakula cha $ 100 unaweza kutumia hata wiki mbili,alafu wanakuambia hivi kama kipato chako hakitoshi unaruhusiwa kuomba kadi ya chakula watakupa unakuwa unatumia kadi hautolipa hela yako.

Kama huwezi kulipia nyumba kuna nyumba za serekali wanakupa unaweA kuwa unalipa $ 100 au 200 kila mwez

Hata kwenye swala la matibabu ni hivyo ,binafsi nilienda hospitali kufanyiwa upasua wa sikio nilitakiwa nilipe $elfu 17.
Lakin kuna mashirika ya kusaidia kama huna uwezo wa kulipa,pesa hiyo nililipiwa yote na wakaongeza nyingine.natiwaga bure tu.

Sasa hapo unataka nini?

Hayo mambo tanzania lini mkuu?
Mkuu apo kwenye " natiwaga bure tu" sijaelewa yani!
 
Marekani ikiwa pesa yako inaishia kwenye pango na chakula.
Serekali iko kwaajili yako.

Mfanounalipwa $ 1500 fanya hivi
Apply nyumba ya serekali kila mwez utakuwa unalipa $ 200

Apply kadi ya chakula kila mwez watakuwa wanakupa $ 200

gharama yako ni nyumba tu.
Mkuu nafanyaje kuwa Raia wa Marekani?
 
Acha uongo.. marekani maskini anamiliki vipi shamba au ardhi.. Tanzania mtu hana hata mia lakini ana shamba lake la kulima .

Tanzania kila ukoo una shamba.. kila familia ina shamba kijijini kwao...je usa ardhi inapatikana kiurahisi kama Tanzania
Unaongelea ardhi ambayo Tz tumejaza mapori tu ipo Useless. Unafikiri watu pesa wanatoa kwenye ardh tu. Hebu acha akili za kitoto.
 
We ungekuwa umewahi fika USA ungeongea ukaeleweka Tz ndo kuna umaskini wakutupwa sio USA.

We jamaa sikutegemea kuwa kichwani ni empty.
Inaonekana huyu mtoa mada haelewi hata maana ya umasikini
 
Yawezekana uchumi wa marekani unamilikiwa na watu wachache kwa kiwango kukubwa ,je wale kajamba nani hali ikoje?
Kwa hiyo unataka watu walingane? Lazima kuwe na tajiri na maskini ili tutegemeane .

Ila umaskini wa Tz huwezi linganisha na USA.

Tz mtu akimiliki gari tu anaonekana tajiri kumbe wenzetu uko tajiri mpaka umiliki fancy car.
 
Marekani ni taifa lenye watu wengi wenye hali mbaya kimaisha mfano 40% ya watu weupe wanaishi kwenye umasikini.

Pia watu wengi weusi wanaishi kwenye umasikini na msongo wa mawazo, yaani tuseme wanapata pesa ya kula na kulipia pango basi ili tatizo lipo pia South Africa na Kenya.

Mifumo ya Ubepari ni hatari sana duniani pamoja na mapungufu yake Baba wa taifa alifanya jambo kubwa sana kutoruhusu ubepari kuzagaa mapema Tanzania ukitoa mikoa ya Dar na Arusha mikoa mingine maisha ni rahisi kutoboa ila kwa wenzetu miji yao yote cost za maisha zipo juu sana.

Ndio maana ni vigumu sana kuona maandamano Tanzania lakini nchi kama South na Kenya pia Marekani jambo dogo tu unaweza kuta watu wanaandamana wanapiga police, wanapora mali huu ni umasikini wala sio ubaguzi, wanaficha matatitizo yao kwenye ubaguzi lakini ukweli ni hali mbaya ya uchumi mifukoni uku matajiri wakikusanya pesa yote.

Tanzania tuna umasikini lakini tuna low cost of living ndio maana Mashamba, Ng'ombe yanamilikiwa na masikini Tanzania.
Uko Sahihi mkuu. uzuri nimefika na kuishi kwenye zote ulizotaja japo huko kwa weupe sio sana ila naamini unachokisema kwa asilimia mia. Maisha kule ni hand to mouth. Hakuna kusave hata mia. Wamefanya hesabu kabisa kuwa wakikulipa mia tano lazima mwisho wa mwezi iishe yooote na uingie tena ukiwa mtupu kabisa. Labda ufanye kazi usiku na mchana kama wabongo wengi wanavyofanya huko majuu. Mfano mzuri ni Lemutuz alivyotua bongo bila hata mia
 
Mkuu $700 kwa wiki unaniambia inakupeleka wapi?.

Tufanye hivi:
Kodi ya nyumba nalipa $600 kwa mwezi

Umeme $40
WI FI 50
Chakula200

Jumla kama 890 kwa mwezi

Turudi sasa
700 x 4=$2800
2800-890= 1910 hiyo ndio pesa unaweka akiba
$890 kwa mwezi!!! Kwa mwaka=10680!!!! Upo maeneo gani chief?
 
Marekani kipindi cha corona kila raia alipewa dollar 1200 na watoto wakapata $500 kila mmoja

Wale waliacha kazi kwa majanga ya corona wanalipwa kila wiki $ 700 na kuendelea.
Binafsi kazini kwangu naliowa $800 kazini kwangu na $ 700 kutoka serekalin kila wiki

Watu mwenye kipato cha chini walipewa bima na kadi ya chakula isitoshe wanapelekea chakula na bank food.

Tanzania...............?


Halafu tuulize nani mwenye njaaa?
Achana na huyo anayeleta stori za vijiweni!
 
Mshahara wa serikali upo juu na hasa ukilinganisha na muda unaotumika kufanya kazi. Watumishi wa umma muda wanaotumia kufanya kazi ni mdogo mno. Kutoka kazini kwenda shughulikia maswala nje ya kazi kama vile kunywa chai, chakula, benki nk na anaetaka huduma kuambiwa asubirie, aje baadae au kesho ni jambo la kawaida.
Eti mtu anaingia kazini saa 2 asubuhi na kutoka saa 8 au 9 uku aitoka kunywa chai, kula cha mchana maana yake alipoteza masaa 2 pia. hivyo katika masaa 24 kafanya kazi masaa 5 tu akilipwa dollar 200 kwa mwezi ni sawa maana ana muda wa ziada kufanya biashara au kazi nyingine ili atengeneze dolla 300 au 400 nyingine.
 
Yaani mwalimu wa shule ya msingi huko marekani anapanga likizo yake aje kupanda mlima kilimanjaro na akae mwezi mmoja kwenye 5star hotel pale arusha, upande wa pili tafuta mwalimu wa shule ya msingi bongo, huruma.
 
Back
Top Bottom