Marekani wanasumbuliwa na Umasikini sio Ubaguzi

Robo ya watanzania wanaishi kwenye ufukara wa kutupwa,hawa hata kupata mahitaji muhimu ya binadamu kama milo 3 tu kwa siku bado ni changamoto kwao.
Marekani kipindi cha corona kila raia alipewa dollar 1200 na watoto wakapata $500 kila mmoja

Wale waliacha kazi kwa majanga ya corona wanalipwa kila wiki $ 700 na kuendelea.
Binafsi kazini kwangu naliowa $800 kazini kwangu na $ 700 kutoka serekalin kila wiki

Watu mwenye kipato cha chini walipewa bima na kadi ya chakula isitoshe wanapelekea chakula na bank food.

Tanzania...............?

Halafu tuulize nani mwenye njaaa?
 
Masikini wa tz ni tofauti na masikini wa Ulaya ama Marekani masikini wa tz hawezi kulala njaa...
jamaa kaongea point ya msingi sana sema umeshindwa kumuelewa....

Masikini aliyepo kwenye mfumo wa kijamaa na masikini aliyepo kwenye mfumo wa kibepari hawa ni watu wawili tofauti
Maskini wa Tanzania ndiye anayelala njaa ila maskini wa Ulaya na Marekani hawezi kulala njaa.
Tanzania sio nchi ya kijamaa,ni nchi ya kibepari.
 
Hivi watanzania wangap wamemilik hayo unayoyataja hapo
Familia nyingi za kifugaji, nenda umasaini, usukumani, nenda huko singida kwa wafugaji. Nimechukua kama sample. Hata Marekani kuna majimbo Watu wanaishi chini ya dollar moja.
 
Bongo kuna watu wana ekari 5 na ng'ombe ila hawana huduma ya hospitali karibu,watoto wao hawawezi kusoma shule bora,maji safi na salama hawana,watoto wao una utapiamlo na udumavu.
Hivi US mtu wa kawaida anaweza miliki shamba angalau heka 5? au anaweza fuga ng'ombe? bongo mtu anaweza kuwa anaingiza 10,000 kwa siku anaenda sokoni ananunua kila kitu na anabaki na akiba ya 5000, US mtu analipwa dollar 75 Au 100 kwa siku akienda super market pesa yote anaacha kule nani mwenye maisha magumu?
 
Maskini wa Tanzania ndiye anayelala njaa ila maskini wa Ulaya na Marekani hawezi kulala njaa.
Tanzania sio nchi ya kijamaa,ni nchi ya kibepari.
Wapo wengi tu wanalala njaa. Ulaya na Marekani. Wanawapa jina zuri la homeless. Wengine wanapata msaada makanisani. Hawataki kuwaita masikini. Mie mwenyewe nimeshuhudia wazungu kadhaa ambao hawakuwa na hela ya kula. Nawasaidia. Ulaya na Marekani kuna Watu wengi wanaishi maisha magumu ila kinachosaidia serikali zao zilishajenga mifumo mizuri ya huduma za kijamii. Lakini maisha ya mtu binafsi mengi magumu. Lishe mbovu. Watu wanaishi kwa kula mikate. Ndo maana Ulaya au Marekani kwa chakula daaah! Mtu hawezi kukukaribisha hiv hivi. Lakini Bongo!
 
Bongo kuna watu wana ekari 5 na ng'ombe ila hawana huduma ya hospitali karibu,watoto wao hawawezi kusoma shule bora,maji safi na salama hawana,watoto wao una utapiamlo na udumavu.

Hiyo ilikuwa zamani, kwasasa vituo vya afya vipo kila kata. Huo utapiamlo unazusha toa takwimu. Tanzania kuna campain ya mama na mtoto lishe. Hatuna idadi kubwa za utapia mlo. Umesikia Marekani wanao kufa wengi kwa Corona ni watu weusi na sababu kubwa nikwamba hawana lishe bora. Wengi wao ula junk food. Na wanaugumu wa maisha. Pia huduma ya afya Marekani bado ni tatizo. Obama alijaribu kuja na suruhisho lkn kuna mamillioni ya watu ni vigumu kumudu matibabu na hata masomo.
 
Umefafanua zaidi tu nilichoandika kwa kuonyesha tofauti ya maskini wa Tz na Ulaya. Halafu kwa nini unawasikitika wanaotumia mikate kama chakula? Unafikiri ugali na wali ndivyo vyakula vikuu kwa watu wote duniani?
Wapo wengi tu wanalala njaa. Ulaya na Marekani. Wanawapa jina zuri la homeless. Wengine wanapata msaada makanisani. Hawataki kuwaita masikini. Mie mwenyewe nimeshuhudia wazungu kadhaa ambao hawakuwa na hela ya kula. Nawasaidia. Ulaya na Marekani kuna Watu wengi wanaishi maisha magumu ila kinachosaidia serikali zao zilishajenga mifumo mizuri ya huduma za kijamii. Lakini maisha ya mtu binafsi mengi magumu. Lishe mbovu. Watu wanaishi kwa kula mikate. Ndo maana Ulaya au Marekani kwa chakula daaah! Mtu hawezi kukukaribisha hiv hivi. Lakini Bongo!
 
Robo ya watanzania wanaishi kwenye ufukara wa kutupwa,hawa hata kupata mahitaji muhimu ya binadamu kama milo 3 tu kwa siku bado ni changamoto kwao.

Tusifuate propaganda za wazungu. Swali hapa wangapi Ulaya na Marekani wanakula mlo ulio kamili? Kula mikate nao ni mlo? Niliwahi fika kanisa fulani. Huko mnakokusifia. Alikuwepo Pia kijana toka middle East, kila mtu aliulizwa nn tunakula nchini mwetu. Mie nilitaja nini nakula. Yule mchungaji hakuamini. Bahati nzuri kuna mama wa kizungu aliishiTanzania miaka ya nyuma, akasema kweli hivyo chakula kwa Tanzania ni saga. Yule mchungaji alinichukia hakutaka kuendelea nami. Akaona awe na Yule kijana middle East alosema kula ya shida. Huyu mama akasema naona wamekuacha but sie twendelee achana nao. So siwezi kujidharirisha kisa kuabudu uzungu wakati wao wanashida kedekede
 
Marekani ni taifa lenye watu wengi wenye hali mbaya kimaisha mfano 40% ya watu weupe wanaishi kwenye umasikini.

Pia watu wengi weusi wanaishi kwenye umasikini na msongo wa mawazo, yaani tuseme wanapata pesa ya kula na kulipia pango basi ili tatizo lipo pia South Africa na Kenya.

Mifumo ya Ubepari ni hatari sana duniani pamoja na mapungufu yake Baba wa taifa alifanya jambo kubwa sana kutoruhusu ubepari kuzagaa mapema Tanzania ukitoa mikoa ya Dar na Arusha mikoa mingine maisha ni rahisi kutoboa ila kwa wenzetu miji yao yote cost za maisha zipo juu sana.

Ndio maana ni vigumu sana kuona maandamano Tanzania lakini nchi kama South na Kenya pia Marekani jambo dogo tu unaweza kuta watu wanaandamana wanapiga police, wanapora mali huu ni umasikini wala sio ubaguzi, wanaficha matatitizo yao kwenye ubaguzi lakini ukweli ni hali mbaya ya uchumi mifukoni uku matajiri wakikusanya pesa yote.

Tanzania tuna umasikini lakini tuna low cost of living ndio maana Mashamba, Ng'ombe yanamilikiwa na masikini Tanzania.

Marekani wanasumbuliwa na demokrasia iloanguka pamoja na vita kati ya matajiri na maskini.

Demokrasia nchini Marekani ipo hoi kitandani na haiwezi kuundwa tena kwa kutumia misingi ya sasa ya ubepari na mifumo ya kijamii.
 
Umefafanua zaidi tu nilichoandika kwa kuonyesha tofauti ya maskini wa Tz na Ulaya. Halafu kwa nini unawasikitika wanaotumia mikate kama chakula? Unafikiri ugali na wali ndivyo vyakula vikuu kwa watu wote duniani?

Nimeongelea mlo kamili. Nadhani ufatilii habari. Wa Marekani wengi weusi wamekufa kwa covid 19 imeelezwa sababu lishe. Pia Tanzania chakula si ugali na wali pekee. Tunavyakula vingi zaidi. Nadhani ujaizungukia Tanzania.
 
Kwanza hakuna vituo vya afya kila kata na vituo vya afya sio hospital.Hospitali ni kama Muhimbili,KCMC,Tumbi,Agha Khan na nyingine za aina hii.
Hiyo ilikuwa zamani, kwasasa vituo vya afya vipo kila kata. Huo utapiamlo unazusha toa takwimu. Tanzania kuna campain ya mama na mtoto lishe. Hatuna idadi kubwa za utapia mlo. Umesikia Marekani wanao kufa wengi kwa Corona ni watu weusi na sababu kubwa nikwamba hawana lishe bora. Wengi wao ula junk food. Na wanaugumu wa maisha. Pia huduma ya afya Marekani bado ni tatizo. Obama alijaribu kuja na suruhisho lkn kuna mamillioni ya watu ni vigumu kumudu matibabu na hata masomo.
 
Wengi ni asilimia ngapi ya watu wote waliokufa?Wapi imeelezewa sababu ni lishe?
Italia,Ufaransa na Uingereza ambako maelfu ya wazungu wamefariki sababu nayo ilikuwa ni lishe?
Nimeongelea mlo kamili. Nadhani ufatilii habari. Wa Marekani wengi weusi wamekufa kwa covid 19 imeelezwa sababu lishe. Pia Tanzania chakula si ugali na wali pekee. Tunavyakula vingi zaidi. Nadhani ujaizungukia Tanzania.
 
Kwanza hakuna vituo vya afya kila kata na vituo vya afya sio hospital.Hospitali ni kama Muhimbili,KCMC,Tumbi,Agha Khan na nyingine za aina hii.

Nadhani unataka badili nilichisema. Nimesema kuna vituo vya afya. Hata Ulaya hawana hospitali kila sehemu. Wanavituo vya afya na hospitali huu ni mfumo kidunia. Uwezi kuwa na hospitali kilasehemu. Bali katika ward moja kuna kuwa na kituo cha afya. Nenda Ulaya Marekani, Australia popote mfumo ni huo. Hapa nilipo nipokatika nchi ambayo ina mifumo mizuri ya afya. Lakini hawana hospitali kila kata. Wanavituo vya afya ambapo ukiumwa unareport kama tatizo kubwa unaandikiwa kwenda hospitali kubwa.
 
Umeandika nini hapa? Haueleweki
Tusifuate propaganda za wazungu. Swali hapa wangapi Ulaya na Marekani wanakula mlo ulio kamili? Kula mikate nao ni mlo? Niliwahi fika kanisa fulani. Huko mnakokusifia. Alikuwepo Pia kijana toka middle East, kila mtu aliulizwa nn tunakula nchini mwetu. Mie nilitaja nini nakula. Yule mchungaji hakuamini. Bahati nzuri kuna mama wa kizungu aliishiTanzania miaka ya nyuma, akasema kweli hivyo chakula kwa Tanzania ni saga. Yule mchungaji alinichukia hakutaka kuendelea nami. Akaona awe na Yule kijana middle East alosema kula ya shida. Huyu mama akasema naona wamekuacha but sie twendelee achana nao. So siwezi kujidharirisha kisa kuabudu uzungu wakati wao wanashida kedekede
 
Wengi ni asilimia ngapi ya watu wote waliokufa?Wapi imeelezewa sababu ni lishe?
Italia,Ufaransa na Uingereza ambako maelfu ya wazungu wamefariki sababu nayo ilikuwa ni lishe?

Duuuh! Kweli Sasa nimechoka nilidhani unafatilia habari za ulimwengu na utakuwa aware na kinachoendelea. Pia ni kawaida kuwa most of people in USA wanakula junk food kutokana na urahisi wa gharama. Hii inafahamika uhitaji hata kufanya research. Hata Ulaya Pia watu kibao na junk food.
 
Umeandika nini hapa? Haueleweki

Kutoeleweka ni moja ya kufahamu uelewa wa halieshindwa kuelewa. Mwalimu akifundisha darasani kuna wanao mwelewa na wasio mwelewa. Ndo maana kuna slow learner na fast learner.
 
Huko nchi uliyopo ni kawaida wagonjwa kulundikana na kusongamana kumsubiria daktari kama Mwananyamala hospitali ya Tz?
Kuna wagonjwa wanashindikana kutibiwa nchini mwao na kuomba michango ya kukimbizwa India au South Africa?
Nadhani unataka badili nilichisema. Nimesema kuna vituo vya afya. Hata Ulaya hawana hospitali kila sehemu. Wanavituo vya afya na hospitali huu ni mfumo kidunia. Uwezi kuwa na hospitali kilasehemu. Bali katika ward moja kuna kuwa na kituo cha afya. Nenda Ulaya Marekani, Australia popote mfumo ni huo. Hapa nilipo nipokatika nchi ambayo ina mifumo mizuri ya afya. Lakini hawana hospitali kila kata. Wanavituo vya afya ambapo ukiumwa unareport kama tatizo kubwa unaandikiwa kwenda hospitali kubwa.
 
Research ndio muongozo kwa mtu makini.
Hata Tanzania kuna utapiamlo kwa sababu ya lishe duni,tafiti za hili zimejaa tele mtandaoni.
Duuuh! Kweli Sasa nimechoka nilidhani unafatilia habari za ulimwengu na utakuwa aware na kinachoendelea. Pia ni kawaida kuwa most of people in USA wanakula junk food kutokana na urahisi wa gharama. Hii inafahamika uhitaji hata kufanya research. Hata Ulaya Pia watu kibao na junk food.
 
Huko nchi uliyopo ni kawaida wagonjwa kulundikana na kusongamana kumsubiria daktari kama Mwananyamala hospitali ya Tz?
Kuna wagonjwa wanashindikana kutibiwa nchini mwao na kuomba michango ya kukimbizwa India au South Africa?

Naona weye unatafuta lawama tu, naipenda nchi yangu Tanzania. Siwezi kukaa nikaikashifu au kudharau kwa ushabiiki usiokuwa na maana. Kila nchi zinachangamoto zake. Uwezi kila wakati fananisha Ulaya au Marekani na Tanzania. Tanzania tunachangamoto zetu ambazo tutazitafutia ufumbuzi kulingana na hali yetu na utamaduni wetu. Ulaya nao wanachangamoto zao. Tusiwe na mawazo kuona kama wazungu ni malaika. Mie nilikuwa na kulelewa na hao wazungu unao wasifia. Nimeishi nchi za Ulaya na Marekani. Na hata Afrika Pia. Nikupe Siri tu mzungu anathamini cha kwake hata kama hataona hakifai. Wanauzalendo wa hali ya juu na hawapendi kusema udhaifu walonao. Niishie hapo.
 
Facts ni facts tu hazijali nchi yako au sio yako.
Fuatilia pia na masuala kama tofauti za Life span, maternal mortality rate na child mortality kati ya nchi yako na huko uliko kama ni kweli uko huko uliko
Kwani Marekani wote ni wazungu?
Kuilinganisha vizuri Africa na Ulaya au Marekani kaangalie Ted Talk ya Ali Mufuruki "Is Africa really rising?".

Back
Top Bottom