Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Facts ni facts tu hazijali nchi yako au sio yako.
Fuatilia pia na masuala kama tofauti za Life span, maternal mortality rate na child mortality kati ya nchi yako na huko uliko kama ni kweli uko huko uliko
Kwani Marekani wote ni wazungu?.
Sihitaji kubishana, uzuri nimekuelewa nikupe ushindi. Ila sintokaa kuichafua nchi yangu au kuidharau kwa sababu ya facts. Kama kunachanga moto nitajitahidi nichangie kupunguza. Mfano miaka iliyopita nilisomesha wanafunzi sekondari wasiopungua miamoja. Ilikuwa kipindi wanafunzi wanalipa Ada wa sekondari. Niliwatafutia ufadhili wanafunzi watano wa vyuo vikuu waliokoswa mikopo wakati huo. Niliwasaidia walemavu wasio na uwezo kujiajiri kwa kupewa mitaji na mashirika ya kitanzania. Pia nilisaidia baadhi ya vijana kupata ajira katika sekta binafsi. Uwa sina muda wa kulaumu nchi yangu na kuikashfu. Bali nipo kutoa mchango wangu ktk Taifa langu. Kikubwa nione ni nini nimefanyia nchi yangu. Naona fahari kuwa mtanzania na natangaza mazuri ya nchi yangu. Changamoto zilizopo haziishi siku kwa siku moja. Hivyo mawazo au nilichonacho kidogo nashirikiana na watanzania wenye nia njema kusaidia kupunguza tatizo. Na sio kubeza na kuikashfu. Tusisubiri viongozi kutuletea maendeleo tujumuike kama jamii. Bila kujali nafasi zetu au uwezo wetu. Hata leo Mungu akinichukua akaniuliza uliifanyia nn nchi yako ninalao la kumwambia na kujivunia. Kuwa niliitumikia nchi yangu kwa haya.