Kuna utofauti mkubwa wa mila, desturi na tamaduni.
Hapa tuko kwenye mada tusitoke nje ya mada. Hawa wazungu kwanza hawataki mwafrika au mtu mweusi hawazidi. Wanataka siku zote uwe chini yao. Na ukijaribu kujinyenyekeza kwao ndo watajifanya wanacheka nawe lkn mioyoni they look down you! Nilihudhuria moja ya vikao vyao. Kuna profesa mmoja ni maarufu sana. Amekuwa na Nyerere karibu na anamheshimu sana. Anamkubari sana. Kwann Nyerere hakujikomba kwao aliwapa ukweli. Huyu profesa aliongelea Demokrasia nchini Tanzania. Tulibishana nae sana. Nilimwambia demokrasia inaendana na utamaduni, au mila na desturi za eneo husika. Uwezi beba demokrasia ya Ulaya au Marekani ukaichukua kama ilivyo haitofanya kazi. Nilimwambia Afrika inahitaji demokrasia kulingana na mazingira yake na utamaduni wake. Baada ya kumpa mifano kadhaa alinielewa. Hatuwezi kuiga kila kitu kama kilivyo. Tunatofauti kubwa ya kimazingira, mila na desturi. Mchina ameendelea kwa sababu akuhamisha kila kitu kutoka nje. Alichofanya ni kuweka mambo kuendana na tamaduni na mila zao. Lakini Afrika tunataka tufanye kila kitu kama alivyo mzungu. Copy and Paste! Hatutafanikiwa kamwe. Tumeacha mila na desturi zetu tunaiga mzungu. Hadi corona leo imetufanya tukumbuke dawa za mababu zetu. Tulizozizarau na kuona mzungu tu. Ebu tuwe proud na vyakwetu. Ebu tuwaoneshe siye ni wathamani. Naongea haya uzuri nimelelewa na kuishi nao hao wazungu. Toka Ulaya na Marekani. Nawajua toka utoto wangu. Na wanajua misimamo yangu na wanaiheshimu. Kamwe hawaongei ujinga mbele yangu. Na wengi wamekuja Tanzania kuitembelea na wamependa Tanzania.