Maskini Tanzania, ana ng'ombe 500 hadi 1000. Ana mbuzi na kondoo wapatao 100, anakuku wa kienyeji ambao ukimtembelea muda wowote unachinjiwa, Maskini huyu anamashamba hekari si chini ya ishirini, anaishi kijijini, hana TV wala hana simu ya touch. Zaidi anasimu ya button. Ok wewe unaelipwa na serikali umekatiwa na bima. Ukijilinganisha na Maskini wa Tanzania wa kijijini ni nani alie na vitega uchumi. Nimeishi Ulaya mara nyingi niliwaambia swala si umasikini ni "life style" kwa sababu Mmasai anae kaa porini na kuitwa masiki wakati ana ng'ombe 1000 hadi 5000 si sawa. Au msukuma aliye na ng'ombe na mashamba kusema ni masikini sidhani. Kwani Ulaya au Marekani kuna wengi wasio na uwezo wa kumiliki ng'ombe 5000 kuwa na mashamba na nyumba hata ukiwambia waje huku kununua. Wengi wanaishi kupata hela kulipia pango na kula basi. Chukulia mfano yule mzee wa kimasai alojenga shule yake kwa familia alikuwa na watoto Zaidi ya 80. Wote aliwalisha. Huko Marekani wewe unaejisifia kupewa hela na serikali ungeweza? Hata ulipwe na serikali miaka 10 uwezi mfikia huyu mzee. RIP Mzee wetu wa Ngorongoro. Watu wanazuzuka tu na maisha ya Ulaya na Marekani lakini hakuna kitu. Tazama vijana walioko Tanzania wanavyopata mafanikio Zaidi ya walioishi Ulaya miaka kibao.