Marekani yajitosa kesi ya Freeman Mbowe

Marekani yajitosa kesi ya Freeman Mbowe

M-mbabe

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2009
Posts
13,203
Reaction score
23,027
Kukamatwa na kushitakiwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumeibua mjadala, ambapo nchi ya Marekani imeshauri kuwepo na majadiliano kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na vyama vya upinzani.

Hayo yameelezwa jana na Naibu Waziri wa Nchi wa Masuala ya Siasa wa Marekani, Victoria Nuland alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kufuatia mkutano wake na Rais Samia na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa hapo jana.

Waziri huyo alisema miongoni mwa mambo aliyozungumza na Rais Samia ni hofu ya Marekani kwenye utaratibu uliotumika kumkamata na kumshitaki Mbowe, huku akiomba Serikali ifuate misingi ya haki na sheria katika kesi hiyo.

“Ni muhimu kabisa kwamba hali hii itatuliwe kwa njia itakayofuata sheria kwa uharaka na uwazi. Hiyo ni muhimu katika kukuza nguvu ya demokrasia nchini Tanzania,” alisema.


Nuland alisema ana matumaini kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi kwa majadiliano baina ya pande zote mbili, baada ya wote kuonyesha utayari wa kukutana na kulizungumza.

“Kwa mtazamo wangu pande zote mbili ni wazalendo na wana malengo mema, kwa hiyo ni vyema wakatumia nafasi hii ya utayari walionao kupata ufumbuzi wa kidemokrasia,” aliongeza.

Waziri huyo pia amemuomba Rais Samia kujenga kasi ya hatua zilizochukuliwa wakati wa siku za kwanza za urais
wake ambako alijitahidi kuondoa vizuizi kwa vyombo vya habari na kutangaza mazungumzo makubwa na asasi za kiraia.

Pia alimsihi Rais Samia, kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu na raia wote watendewe haki chini ya sheria, bila kujali ushirika wao kisiasa.

“Wakati anaanza na matamanio makubwa kidemokrasia na wapinzani pia walionyesha utayari kumuunga mkono, hatua nzuri sana zilishachukuliwa mwanzoni,” alisema.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi, Liberata Mulamula alisema Rais Samia alipanga kukutana na wapinzani lakini ratiba zikaingiliana.

Chanzo: MWANANCHI, 5 AUGUST 2021


My take:
Sarakasi za wahafidhina wanaomshinikiza Samia ndani ya CCM zinaelekea ukingoni. Soon
 
Mbowe amekosea timing......huu sio muda wa Siasa za matusi na zilizokosa adabu. Cdm wasingatie sheria hakuna aliye juu ya sheria.

Never underestimate woman...she is iron lady in polite face. Siku Mia moja tu alibadili mfumo mzima wa mtawala mwenzake! She is who she is....watahitaji huruma sana ya mataifa ya nje. Watakuja,watasema,wataongea mwisho wataondoka.
 
Marekani ndiyo nchi pekee duniani iliiyojitosa kutokomeza UGAIDI duniani, ilifanya hivyo kumtokomeza Osama na genge lake, IS na vikundi vingi vingi tu vya ugaidi duniani.

Sasa juzi wamesikia kuna GAIDI mwingine kagundulika hapa hapa Tanzania, sasa kwa kuwa Marekani na Tanzania ni nchi zenye uhusiano mkubwa tangu enzi za Mwalimu na Rais wao Keneddy - wameona ni vema waje kuangalia huyu Gaidi mpya wa East Africa ni nani..ili basi ikiwezekana watoe msaada wa FBI kuusaka mtandao wake wote popote ulipo duniani.

Kwa hiyo ndugu zangu Marekeni ipo kufuatilia UGAIDI ulioibuka Tanzania... stay turned....
 
Akili yako umeisahau nyumbani. Chama cha siasa kilichosajiliwa katika nchi hii kufanya kongamano la ndani la katiba ni ku-underestimate mtu? Mbona nchi hii imejaa wajinga kiasi hiki?
Mbowe amekosea timing......huu sio muda wa Siasa za matusi na zilizokosa adabu. Cdm wasingatie sheria hakuna aliye juu ya sheria.

Never underestimate woman...she is iron lady in polite face. Siku Mia moja tu alibadili mfumo mzima wa mtawala mwenzake! She is who she is....watahitaji huruma sana ya mataifa ya nje. Watakuja,watasema,wataongea mwisho wataondoka.
 
Mambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.
Tanzania is a sovereign coutry.
ila Chadema hakikufaa kabisaa kuwa chama cha upinzani nchini Tanzania kwa tabia ya mara kwa mara wanayo ionyesha inapo tokea jambo lolote basi wanaenda kuichongea Tanzania kwa mataifa makubwa wakitegemea Viongozi wetu wataogopa!! thubutu!!!! kamwe tusivumilie tabia hii ya kizandiki!!! labda wakafanye siasa zao Burundi lkn sio Tz..
Tunaomba viongozi wetu wasiyumbe kabisa, wawe imara kusimamia sheria za nchi.
Demokrasia sio kuvunja amani.
 
Back
Top Bottom