Marekani yajitosa kesi ya Freeman Mbowe

Marekani yajitosa kesi ya Freeman Mbowe

Kukamatwa na kushitakiwa kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumeibua mjadala, ambapo nchi ya Marekani imeshauri kuwepo na majadiliano kati ya Rais Samia Suluhu Hassan na vyama vya upinzani.

Hayo yameelezwa jana na Naibu Waziri wa Nchi wa Masuala ya Siasa wa Marekani, Victoria Nuland alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kufuatia mkutano wake na Rais Samia na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa hapo jana.

Waziri huyo alisema miongoni mwa mambo aliyozungumza na Rais Samia ni hofu ya Marekani kwenye utaratibu uliotumika kumkamata na kumshitaki Mbowe, huku akiomba Serikali ifuate misingi ya haki na sheria katika kesi hiyo.

“Ni muhimu kabisa kwamba hali hii itatuliwe kwa njia itakayofuata sheria kwa uharaka na uwazi. Hiyo ni muhimu katika kukuza nguvu ya demokrasia nchini Tanzania,” alisema.

Nuland alisema ana matumaini kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi kwa majadiliano baina ya pande zote mbili, baada ya wote kuonyesha utayari wa kukutana na kulizungumza.

“Kwa mtazamo wangu pande zote mbili ni wazalendo na wana malengo mema, kwa hiyo ni vyema wakatumia nafasi hii ya utayari walionao kupata ufumbuzi wa kidemokrasia,” aliongeza.

Waziri huyo pia amemuomba Rais Samia kujenga kasi ya hatua zilizochukuliwa wakati wa siku za kwanza za urais
wake ambako alijitahidi kuondoa vizuizi kwa vyombo vya habari na kutangaza mazungumzo makubwa na asasi za kiraia.

Pia alimsihi Rais Samia, kuhakikisha ulinzi wa haki za binadamu na raia wote watendewe haki chini ya sheria, bila kujali ushirika wao kisiasa.

“Wakati anaanza na matamanio makubwa kidemokrasia na wapinzani pia walionyesha utayari kumuunga mkono, hatua nzuri sana zilishachukuliwa mwanzoni,” alisema.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi, Liberata Mulamula alisema Rais Samia alipanga kukutana na wapinzani lakini ratiba zikaingiliana.

Chanzo: MWANANCHI, 5 AUGUST 2021

My take:
Sarakasi za wahafidhina wanaomshinikiza Samia ndani ya CCM zinaelekea ukingoni. Soon

Kwamba?

"Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Balozi, Liberata Mulamula alisema Rais Samia alipanga kukutana na wapinzani lakini ratiba zikaingiliana."

Ratiba zikaingiliana? Vipaumbele vya ustawi wetu vinaeleweka?

Baada ya siku 100 SSH kathibitisha wanahitaji kuzodolewa kama mwendazake tu.
 
Ninaomba msaada jinsi ya kujiunga na space ya Maria Sarungi
 
Mbowe amekosea timing......huu sio muda wa Siasa za matusi na zilizokosa adabu. Cdm wasingatie sheria hakuna aliye juu ya sheria.

Never underestimate woman...she is iron lady in polite face. Siku Mia moja tu alibadili mfumo mzima wa mtawala mwenzake! She is who she is....watahitaji huruma sana ya mataifa ya nje. Watakuja,watasema,wataongea mwisho wataondoka.
Mwambie kama kweli ni iron lady akuze uchumi aache siasa za kishamba hazisaidii nchi.Kama una akili timamu hiyo ni kesi ya kubumba so usishabikie ujinga .
 
Mambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.
Tanzania is a sovereign coutry.
ila Chadema hakikufaa kabisaa kuwa chama cha upinzani nchini Tanzania kwa tabia ya mara kwa mara wanayo ionyesha inapo tokea jambo lolote basi wanaenda kuichongea Tanzania kwa mataifa makubwa wakitegemea Viongozi wetu wataogopa!! thubutu!!!! kamwe tusivumilie tabia hii ya kizandiki!!! labda wakafanye siasa zao Burundi lkn sio Tz..
Tunaomba viongozi wetu wasiyumbe kabisa, wawe imara kusimamia sheria za nchi.
Demokrasia sio kuvunja amani.
Ujinga mtupu.
 
Usalama gani wa kubambikia watu kesi,kwa hiyo unashabikia watu kuonewa .Mimi nataka Kila raia wa Tanzania bila kujali chama chake awe na haki ,haya mambo ya kuoneana hayakubaliki kwa watu wanaojielewa .
 
Mambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.
Tanzania is a sovereign coutry.
ila Chadema hakikufaa kabisaa kuwa chama cha upinzani nchini Tanzania kwa tabia ya mara kwa mara wanayo ionyesha inapo tokea jambo lolote basi wanaenda kuichongea Tanzania kwa mataifa makubwa wakitegemea Viongozi wetu wataogopa!! thubutu!!!! kamwe tusivumilie tabia hii ya kizandiki!!! labda wakafanye siasa zao Burundi lkn sio Tz..
Tunaomba viongozi wetu wasiyumbe kabisa, wawe imara kusimamia sheria za nchi.
Demokrasia sio kuvunja amani.
Mbona Mandela na Nyerere ndio walikua wanaomba duniani kuwapiga vikwazo Afrika Kusini na S.Rhodesia? Ni kitu cha kawaida kuomba intervention ya Nchi washirika hata Burundi wakivurugana au Rwanda tunaona kina Mkapa wanaenda kusuluhisha unless haujui maana ya diplomasia
 
Chadema wanastahili kubinywa mbupu zao mpaka zitoe damu....wameona mbabe kaondoka wameanza kuleta vurugu,wakati wa magu walitulia kama hawapo aliposema hakuna siasa walielewa....sasa kaja huyu mama wanaona wamepata mteremko chadema heshimuni sheria kuweni wastaarabu,movement wakati wa jiwe mlisitisha sasa acha mbowe apate joto la jiwe huko aliko huku lissu anakula bata ulaya.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Hawa nao wanafuatilia chanjo zao Tu maana aliwapromote Akisema watu wachanjwe kwalazima

Marekani wapuuzi Tu Kwa nini wasiwafuatilie wakorea au wachina [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Movement za katiba mpya...wakati hamjawahi kukaa sehemu mkafundisha wananchi katiba waielewe wajue mapungufu yaliyopo mnakimbilia kumezesha watu sumu waandamane kudai kitu ambacho hawakielewi haingii kichwani kwa sisi std 7,iweje kwa wasomi wanaokaza mishipa ya fuvu.

Sent from my SM-G570F using JamiiForums mobile app
 
Mbowe amekosea timing......huu sio muda wa Siasa za matusi na zilizokosa adabu. Cdm wasingatie sheria hakuna aliye juu ya sheria.

Never underestimate woman...she is iron lady in polite face. Siku Mia moja tu alibadili mfumo mzima wa mtawala mwenzake! She is who she is....watahitaji huruma sana ya mataifa ya nje. Watakuja,watasema,wataongea mwisho wataondoka.
Mbowe alimtukana Nani na wapi mbowe alifanya siasa za matusi
 
Mambo ya usalama wa ndani ya nchi yatabaki kuwa ya nchi.
Tanzania is a sovereign coutry.
ila Chadema hakikufaa kabisaa kuwa chama cha upinzani nchini Tanzania kwa tabia ya mara kwa mara wanayo ionyesha inapo tokea jambo lolote basi wanaenda kuichongea Tanzania kwa mataifa makubwa wakitegemea Viongozi wetu wataogopa!! thubutu!!!! kamwe tusivumilie tabia hii ya kizandiki!!! labda wakafanye siasa zao Burundi lkn sio Tz..
Tunaomba viongozi wetu wasiyumbe kabisa, wawe imara kusimamia sheria za nchi.
Demokrasia sio kuvunja amani.
We mjinga kwa hiyo mnaona fahari kuonea wapinzani wenu kisa ni sovereign country acheni ushama nyie lumumba Ila ipo siku mtatamani kukaa na hao mnao waita magaidi lakini mtakuwa mmesha chelewa tendeni haki mtabalikiwa
 
Screenshot_2021-08-05-11-16-08-87.png
 
Kuna mtu anakwenda kustaafishwa kwa manufaa ya umma AKAVUTE KOKORO...
 
Back
Top Bottom