Kitengo cha upelelezi cha Marekani (FBI) kimemkamata mlinzi wa anga mwenye umri wa miaka 21 huko mjini Massachusetts kwa madai kuhusika kwenye uvujishaji wa nyaraka za siri za kijeshi (Wizara ya Ulinzi wa nchi hiyo, Pentagon). Soma:
Nyaraka za siri za Marekani na mpango wa kumuua Putin zaanikwa
FBI walimkamata Jack Teixeira akiwa nyumbani kwake katika mji wa Dighton Kaskazini. Akifafanua tukio hilo, Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Merrick Garland, amethibitisha kukamatwa kwa mlinzi huyo, huku akieleza kuwa kwamba Teixeira, anashikiliwa kwa kuhifadhi na kusambaza taarifa za siri za Wizara ya Ulinzi wa taifa".
Inaelezwa kuwa Teixeira amekamatwa kutokana na kuongoza kundi sogozi mtandaoni (Online Chat Group) lililokuwa likiwekwa picha na nyaraka nyingi za siri. Kundi hilo lilijiita
Thug Shaker Central lilianzishwa Machi, 2022 na mamia ya picha na taarifa nyingi za siri zimekuwa zikiwekwa hapo.
Kutokana na tukio hilo Teixeira atakabiliwa na mashtaka chini ya Sheria ya Ujasusi. Inaelezwa kuwa kila shtaka chini ya sheria hiyo linaweza kubeba hadi kifungo cha miaka 10, Waendesha mashtaka wanaweza kuchukulia kila hati iliyovuja kama hesabu tofauti katika mashtaka yake.
Sehemu muhimu zaidi ya nyaraka hizo inahusu utayari wa mji wa Kyiv katika kujiandaa na mashambulizi ya Urusi yanayotarajiwa kuwapata. Mistari mingine ya nyaraka hizo inaonesha namna mataifa mengine yatashiriki kuingia katika mgogoro huo jambo linaloweza kusababisha matatizo makubwa ya kidiplomasia.
Zaidi ya hayo, nyaraka hizo zinaonesha uchanganuzi uliofanywa na Shirika la Ujasusi la Ulinzi la Marekani ambao unabainisha mambo 4 ya kidhahania ikiwa ni pamoja na mpango wa kuuawa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, mabadiliko ya uongozi wa vikosi vya jeshi la Urusi, na mashambulizi ya Ukraine dhidi ya ikulu ya Rais wa Urusi, Kremlin.
Uvujishaji huo wa nyaraka za kijasusi na zenye usiri mkubwa za Pentagon unatajwa kuwa mkubwa zaidi wa masuala ya usalama tangu ule uliofanywa na WikiLeaks 2013, ambao ulijumuisha zaidi ya nyaraka 700,000, video na jumbe za kidiplomasia.
---
The FBI has arrested a 21-year-old air national guardsman in Massachusetts suspected of being responsible for the leak of US classified defence documents that laid bare military secrets and upset Washington’s relations with key allies.
Jack Teixeira was arrested at his home in the town of North Dighton by FBI agents. Helicopter news footage showed a young man with shorn dark hair, an olive green T-shirt and red shorts being made to walk backwards towards a team of agents standing by an armoured vehicle dressed in camouflage and body armour, pointing their rifles at him.
In Washington, the US attorney general, Merrick Garland, confirmed the arrest, saying Teixeira was being held “in connection with an investigation into alleged unauthorized removal, retention and transmission of classified national defence information”.
Garland’s use of language suggests that Teixeira will be facing charges under the Espionage Act. Each charge under the act can carry up to a 10-year prison term, and prosecutors could treat each leaked document as a separate count in his indictment. He could be facing a very long jail sentence.
Garland said the air national guardsman would make an initial appearance at the Massachusetts district court in Boston.
Airman first class Teixeira was in the 102nd Intelligence Wing of the Massachusetts air national guard under the duty title of “cyber transport systems journeyman”, responsible for keeping the internet working at airbases. He joined the guard in 2019.
Teixeira is
believed to have been the leader of an online chat group where hundreds of photographs of secret and top-secret documents were first uploaded, from late last year to March. The online group called itself Thug Shaker Central, made up of 20 to 30 young men and teenagers brought together by an enthusiasm for guns, military gear and video games. Racist language was a common feature of the group.