Marekani yamuonya Kagame kuacha kuisaidia M23 huko DRC

Marekani yamuonya Kagame kuacha kuisaidia M23 huko DRC

Hatimaye sasa its official kuwa Kagame analisaidia kundi la waasi wa M23 wanaopigana na serikali Mashariki mwa Congo DRC.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Blinken, amekutana na P. Kagame na kumpasulia wazi kuwa aache kuisaidia M23 , kikundi kinachoua na kutesa wananchi wa kawaida huko Mashariki ya Congo.

Kama mwizi aliyeshikwa na kiroba cha mbuzi wa kuibwa, bado Kagame amesikika akikaidi onyo hilo.

Asiyesikia la mkuu.

=======

Secretary Blinken’s Call with Rwandan President Kagame - United States Department of State

The below is attributable to Spokesperson Ned Price:

Secretary of State Antony J. Blinken spoke yesterday with Rwandan President Paul Kagame to discuss the importance of peace and stability in eastern Democratic Republic of the Congo (DRC). Secretary Blinken expressed strong support for regional mediation and dialogue led by Angola and the East African Community.

He underscored the need for concrete progress on and implementation of commitments made during these discussions, including the November 23 Luanda Mini-Summit on Peace and Security communiqué. Secretary Blinken made clear that any external support to non-state armed groups in the DRC must end, including Rwanda’s assistance to M23, an armed group that has been designated by the United States and the United Nations.

Secretary Blinken also shared deep concern about the impact of the fighting on Congolese civilians who have been killed, injured and displaced from their homes. Secretary Blinken condemned the resurgence of hate speech and public incitement against Rwandaphone communities, recalling the real and horrible consequences of such rhetoric in the past.

Stategov
Angalau Sasa Drc itahema...
 
Kumbe huna kitu cha maana.
Hatuwezi kuwategemea Marekani kusolve tha Rwanda incursions into DRC.

Tatizo ni sisi majirani na Congo yenyewe.

Kwa kuilaumu Rwanda at least yuko upande wa wanaompinga Kagame kwa kitendo chake.

We could make a step further kumshikisha adabu Kagame.
Kitendo Cha M23 kutangaza kuondoka kwenye maeneo waliyokuwa wameyateka inaonyesha hii kauli ya Marekani imesikika vyema na kutekelezwa na serikali ya Rwanda.
 
Sasa Tanzania itamfanya nini Kagame mbona unaipa umuhimu usio wa msingi. Kwanza uzi unazungumzia wahusika wanne, Marekani, Rwanda, DRC na M23 au na waasi wengine. Wewe unalazimika uhusika wa Tanzania ambao ni kiherehere tu. Na sijaitaja Green Berets kukutisha (maana inajipa umuhimu bure, Rwanda doesn't give a fck about Tz), nimetaja kukuonyesha jinsi Marekani inavyohusika na matendo ya Rwanda nchini Congo.

Tanzania gani hiyo ya kuivamia Rwanda? Unahisi vita wanakaa wanajiamulia tu. Unadhani maofisa wa Tanzania hawajui nani anampa kiburi Rwanda, kuna madhara gani Tanzania inapata kwa Rwanda kuwa DRC. Tuivamie Rwanda ili tugundue nini.

JK hajawahi kumfanya lolote PK, hakuna kikosi cha JW kiliwahi kanyaga ardhi ya Rwanda au kuua wanajeshi wa Rwanda nchini Congo. JW ilienda pambana na M23 the same na inachoenda kufanya Kenya. M23 ni kundi la miaka ya karibuni linaweza vunjwa likaundwa lingine au likapewa nguvu kundi jingine. Kabla ya hilo kundi Rwanda ilishasaidia makundi mengine kabla na ikifika hatua fulani inayapotezea inasaidia mengine.

Kama kuna mtu Kagame alimchukia zaidi ni Robert Mugabe aliyepeleka 30% ya wanajeshi wa Zimbabwe kupigana misitu ya Congo, ndio huyo huyo aliifanya Operation Kitona ifeli. Anayeweza fuatia kwa Kagame kumchukia ni Dos Santos wa Angola aliyeshiriki kumsaidia Laurent Kabila kwenye vita ile iliyoongozwa na Rwandese kwa uwazi. Sio aliyepigana na hawa vijana wa ovyo M23 hawana mbele wala nyuma.
Sahihi kabisa
 
Kitendo Cha M23 kutangaza kuondoka kwenye maeneo waliyokuwa wameyateka inaonyesha hii kauli ya Marekani imesikika vyema na kutekelezwa na serikali ya Rwanda.
True Mareani has no friends, only permanent interests.
 
..they are undermining themselves kwa kujiita Wacongo wenye asili ya Rwanda.

..wenzao hawajiiti Wacongo wenye asili ya Tanzania, Angola, etc wanajiita WACONGO.

..pia wanatumiwa vibaya ya Rwanda na Uganda.

..Pia the ruling class ya Rwanda na Uganda wametajirika sana kwa uporaji wa mali za Drc.

..Na utajiri huo ndio unawafanya wang'ang'anie madaraka, na kukandamiza demokrasia ktk nchi zao.

..Vilevile Wacongo need to govern their country better. Kuna matatizo mengi zaidi yanasababishwa na uongozi mbaya walionao.
Ina maana siku Rwanda na Uganda wakipata viongozi wapya nje ya zao la hawa waliopo, huenda ikawa mwanzo wa kupatikana kwa amani huko Drc ?
mtu chake zitto junior
 
Kwa hiyo mpaka hapo utaona kwamba madai kwamba kuna tishio la Fdlr yanakosa nguvu.
Chimbuko la Fdlr ni uwepo wa wakimbizi wa Kihutu wengi wao wakiwa maofisa wa jeshi na serikali wa utawala wa Marehemu Rais Habyarimana wa Rwanda (wengi wao wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari)......

ila wengine ni wahutu wa kawaida tu waliokimbilia huko Drc baada ya RPF kutwaa madaraka huko Rwanda.

maadam masalia ya hawa wakimbizi wa kihutu bado yapo (maana wengine walirudi Rwanda), Fdlr itaendelea kuwepo tu...

Uvamizi wa Rpf toka mwaka 1996 mpaka sasa (kupitia M23) umewadhoofisha tu ila umeshindwa kuwamaliza sababu kubwa ni pamoja na geographia ya huko inayowafanya wajifiche kirahisi na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa makundi washirika mfano maimai.

kama Fdlr bado wapo Drc basi waondoke wakamalize matatizo yao nyumbani kwao Rwanda.
Bado wapo japo hawana nguvu kubwa kijeshi na kurudi huko itategemea kama watawala wa huko watakubali hilo.
..Kagame had a problem with Tanzania and Mzee Kikwete.
Kikwete alishauri Rwanda iongee na Fdlr ndio ugomvi ulianzia hapo.
Mzee Uhuru Kenyatta ameshaziambia nchi majirani na makundi ya kigeni yenye silaha yaondoke ktk ardhi ya Drc.
Tusisahau sababu kuu ya kuwepo kwa hayo makundi ya kigeni huko ni udhaifu wa serikali husika pia unachangia......

isitoshe kuna wakati hayo makundi hutumika na watawala wa huko kupambana na nchi jirani hasimu pale mizozo ya kikanda inapozuka.
mtu chake zitto junior Moronight walker
imhotep
 
Uko kote ulipotaja tuliitwa. Comoros tuliitwa kurudisha hali ya usalama, DRC tuliombwa na serikali, Msumbiji tulikubaliwa na serikali. Kwahiyo unalenga kusema Tanzania itafanyaje kwa kauli yako ya ndoto za Rwanda haziishi DRC?

Kwamba Tanzania ivamie Rwanda ikiulizwa na UN iseme "ndoto za Rwanda haziishi DRC" au nini unamaanisha. Hata umtoe vichochoroni Rais aliyefeli mtihani wa chekechea akaishia hapo hajui kusoma wala kuandika, hawezi fanya huo upumbavu.

Unajua madhara ya kuvamia sovereign state inayotambuliwa mipaka yake na UN? Unajua war reparations kwa mvamizi zinavyokuwa? Unajua gharama za kuanzisha na kuendesha vita dhidi ya nchi?
Unajua hata foreign reserve tuliyonayo inatosha miezi mingapi? Unajua Rwanda inakuwa na kauli pale tukiivamia, hata ikitaka kukaribisha marafiki zake wanaoitumia kwenye hujuma zao kina Ufaransa kwenye mgogoro inaweza, na je unadhani nchi zote duniani zipo tu zinaiona Tanzania ilivyo zinaridhika?

Mbona Tanzania unaipa umuhimu wa kijinga. Nchi inasubiri COVID-19 itokee wazungu waigawie pesa ijenge vyoo watoto mashuleni wanye humo wewe unaishupalia as if ina Veto power ya UN Security Council.

Eti Tanzania ipigane na Rwanda kisa Congo, Tanzania hii inayonunua sidiria za mitumba kutoka China? Unadhani vita ni matako kila mtu anayo

Yote, lakini arguments zako ni baseless devoid of any material facts!
 
Kitendo Cha M23 kutangaza kuondoka kwenye maeneo waliyokuwa wameyateka inaonyesha hii kauli ya Marekani imesikika vyema na kutekelezwa na serikali ya Rwanda.

..M-23 wasiondoke tu maeneo wanayoyakalia, bali wapokonywe na silaha zao.
 
Mpaka Marekani kutamka wazi wazi kuwa Kagame ndiye M23, basi ameprove beyond doubt.
Sasa waafrika tumalize kazi.
MKUU MWAKA 1996 na 1998 ni USA walimsupport kagame kuvamia zaire ( DRC), vita vilivyochukua maisha ya wacongo 5 million mpaka 2003.
So USA wanajua kuwa alikuwa anaendelea kutumia wanajeshi wa rwanda ( RDF) kuunda makundi ya uasi kwa mkono wa watutsi waishio nchi congo.
USA kumwambia hivyo ni mabadiliko ya kisasa na WATU within USA government system, waliomsupport kipindi kile asilimia kubwa Hawapo madarakani, kumbuka hata Obama alimuonya kagame kuhusu congo.
Tena yule Obama ndo alitaka kumshitaki kabisa ila walishidwa, coz ni mtu wao, coz ni system ya MAREKANI ndo walimtumia kustart congo war.
 
Umeelewa in reverse, US will never support wauaji kama FDLR na wote wanaowatumia na kuwasaidia, US sio wajinga wa kulishwa propaganda ndio maana wako upande wa Kagame siku zote
Mkuu hata USA still wanasaidia kagame angali PK ndiye muaji mkuu wa mauaji ya kimbali ya rwanda na congo.
 
Yani ulikaa ukasubiri Mtanzania hapa hapa nchini akwambie mpango wa CIA ni nini. CIA gani hiyo na imeanza lini kujitolea taarifa kiholela juu ya mipango miovu ya taifa lao.
Kama ungekuwa mfuatiliaji ungepuuzia kauli ya Marekani, haina mashiko na impact yoyote ni business as usual kule CongoView attachment 2438178

Washington Post ya mwaka 1988 nanukuu,
"....But Kagame and his colleagues had designs of their own. While the Green Berets (makomandoo wa Marekani) trained the Rwandan Patriotic Army (jeshi la waasi la kina Kagame lililovamia kutoka Uganda na kuiangusha serikali ya Rwanda), that army was itself secretly training Zairian rebels. Rwandan forces then crossed into Zaire and joined with the rebels to attack refugee camps where exiled Rwandan extremists were holed up. That touched off a war that eventually toppled Africa's longest-reigning dictator, Zaire's Mobutu Sese Seko.

Although the United States shared the goals of dismantling the refugee camps and replacing Mobutu (zingatia hii sentensi), the invasion took Washington by surprise, sources in both countries say. And when the Rwandan forces became involved in massacres and other human rights abuses inside Zaire, now known as Congo, the United States faced a dilemma over how to react that persists to this day...."

https://www.washingtonpost.com/wp-srv/national/longterm/overseas/overseas3a.htm

Marekani na Rwanda wanajuana wanachofanya. Rwanda anaenda mbele zaidi ila Marekani kwa kawaida huwa hana shida na mshirika wake as long as maslahi yake yako secured na huyo mshirika haharibu kivile. Cameroon pale Paul Biya ana miaka 40 akiwa Rais na anakandamiza upinzani na huwezi sikia Marekani inasema lolote, ila muda huohuo Marekani haitaki Assad awe Rais wa Syria.

Congo haiachwi leo wala kesho. Atatoka Kagame aje mwingine, itatoka Rwanda ije nchi nyingine. Mabadiliko yoyote hayana unafuu kwa Congo mpaka waamue tu sasa basi tuache waishi kwa amani
👊
 
Una point nzuri sana, nafikiri demilitarized zone na Banyamulenge kupewa haki ya raia kamili wa Congo will solve 90% ya hii crisis, bado naamini tatizo kubwa zaidi la Congo ni utajiri wake + corrupt & unstable government na kuna powerful forces behind the scene hawataki hili tatizo liishe
Yes Banyamulenge KUPEWA haki Congo INAWEZA kusaidia sana Kuleta amani congo. Ila shida ni makabila wanaoishi Kule congo ya mashairiki walikuwa na huo ugomvi kwa mda mrefu sana. Na bado wanawachukia mpaka leo .
Kuna siku felix alisema banyamulenge wamezaliwa congo , wacongo wenyewe walikasilika na kumzomea felix


Cheki HIO video chini uwone wanavyochikiwa
 
Mkuu unajaribu kumwaga mchanga kwenye basic issue.
Issue hapa ni Kagame kupeleka majeshi yske DRC ikiwaita eti M23.
Huo kimsingi ni uchokozi.
Tanzania ina msimamo wa kuishi kwa amani na majirani zake, lakini mtu amnaye kwa miaka nenda rudi ana ndoto za kuingilia nchi nyingine basi ndoto hizo haziishii DRC.
Tanzania tuzisaidia nchi za Comoro, DRC yenyewe, Msumbiji n.k.
Mchokozi lazima apigwe ili aelewe kuwa havumiliki.
Mkuu ni kweli aslimia kubwa ya wanapiganaji wa m23 ni RDF( rwanda defense force) A.KA Killing machine force.
 
Wenzako wanapigana vita kwa maslahi au ulinzi wa border zao, na hakuna kitu kinaitwa kusaidia , ungejiuliza kwanini 80% ya coltan ambayo ndio yanafanya makampuni kama Apple na samsung kuwa mabilionea inatoka Congo lakini Congo ni maskini wa kutupwa, mtaendelea kumlaumu Kagame kwa ajiri ya ukabila wenu na ideology zenu za kipumbavu na vita haitaisha
Kulinda mpaka ndo kuanzisha war nchi jirani just think DRC uwe TZ na ndoa kagame hawe inafanya hivyo, ungejisikiaje mkuu. Kumbuka kagame kuanza kujihusisha na mgogoro wa congo ni baada ya mauaji ya kimbali rwanda hutu extremists na wahutu RAIA wema alienda zaire(congo) ili, 1996 October kwa msaada wa USA walivamia congo kwa lengo la kumaliza hutu extremists cha ajabu waliua mpaka WATOTO wa chini ya miaka 5 wa kihutu. 1998 walivamia congo kwa lengo la kumuondoa kabila ilishindikana kwa sababu ya angola na zibwambwe,
Kumbuka walikufa watu 5 million kule kwa vita alivyoanzisha kagame kwa msaada wa USA , fikilia ingekuwa TZ ungejisikiaje . Mamia na maelfu wa wanawake walibakwa Kule.
Kama analinda mpaka, FDLR HAWANA uwezo wa kumpindua kagame 100% ishu ni kwamba awarudishe wale wakimbizi kule walikuwepo drc na WAje rwanda ,
Tena kama kulinda mpaka si aweke wanajeshi WAKE mpaka kwake na si kwenda kuanzisha vita.
Hao m23 wiki iliyopita wameuwa watu zaidi ya 100+ VYANZO vingine INASEMA 100+ vyombo vingine vinasema ni 200+ fikilia ingekuwa TZ afu NDUGU yako anafanywa hivyo ungefikiliaje hapo.








Ndo analinda border ya mipaka yake hivyo sio.
 
Kitendo Cha M23 kutangaza kuondoka kwenye maeneo waliyokuwa wameyateka inaonyesha hii kauli ya Marekani imesikika vyema na kutekelezwa na serikali ya Rwanda.
MKUTANO wa angola m23 waliupuuzia walisema hawakutuma mwakilishi ijumaa yake wakaanzisha mpaigano tena.
Kenya waligoma kwenda kabisa.
Baada ya MAREKANI kumforce PK kuondoka m23 , Basi na hapo hapo na wao wakasema tunatii amani ya congo tutaondoka congo ili luketa amani , ishu ni USA baada ya kumwambia aache kusaidia m23.
Bila USA mapigano yangeendelea WAKUU, pk ni mtu wa kiburi asingefuata makubaliano ya mtu yeyete hapa mazima mkuu.
 
Tatizo Kagame Bado ni mchanga sana kwenye siasa hizi za kimataifa! hajui kuwa USA hawana Rafiki wala adui wa kudumu!!...ndo walivo! na mifano iko waziiiii!! siku USA wakimgeuka ndoa atajua kuwa hajui!

Wao USA wakishapata yao!! watampinga tu! tena na kumpleka int. criminal court! Savimbi, saddam,alfonso, wako wapi?? wametumiwa weeeee!! mwisho wa siku wakawa zawadia vifo!

Dos santos kajitenga na jamaa zake wa mstari wa mbele huyo hapo tumemzika juzi!! ........Isabela wanamzodoa lkn wajue atakuja kiongozi wasiye mjua atamrudishia mali zake zooote yule dada!
 
Back
Top Bottom