Marekani yaongeza ushuru wa asilimia 104% kwa China

Marekani yaongeza ushuru wa asilimia 104% kwa China

Wabongo mna focus na China huku kawaumiza hapo bongo kuliko maelezo, kaongeza 10% , kaua contract zote za AGOA vile viwanda vyote vya jeans , korosho na kila kitu sasa kaua maelfu ya kazi kwisha, ARV na USAID projects zote kaua, misaada ya budget kwisha na soon mtawekwa kwenye list ya travel ban, chekeni tuu ila maelfu ya wabongo wameumizwa kuliko China
Wako hapa ooh china super power,us atasanda
Hawawaziii nchi yao
 
Attachments

  • IMG-20250409-WA0002.jpg
    IMG-20250409-WA0002.jpg
    16 KB · Views: 22
Hana uwezo huo,uchumi WA china umekua kiujanja ujanja na hauna miziz imara,na waliitumia USA kukua.
Hujui historia mzee kaa kimya kabisa. Yaani strategy aliotumia china kufika pale unasema ni ujanja ujanja. Umesahau jamaa walipfunga mipaka yao hadi wakapigwa na njaa kali ila wakakataa misaada ya chakula kutoka USA? Acha kuropoka vitu usivovijua. Au hata policy ya 'Made in China' utasema ni janja janja. Top engineers kwa sasa USA wana origin ya uchina wwe unaita ujanja janja?

Watu wametengenea 100 years plan wakaboresha kila kitu kuanzia education hadi production na policies zikawekwa na kusimamiwa bila kupepesa macho, wewe huku uliekulia kwenye serikali ya kichawa chawa unakuja kusema wametoboa kwa janja janja. Hebu kuweni na adabu aiseee... bando la jero lisifanye uropoke ushuzi tu hapa
 
Hebu tuambie uvumbuzi au kifaa chochote unachojua kinatambulisha ni technology ya china.
China history Yao ni utengenezaji vyungu na dawa ya asili na si technologia.
Wewe unavyoona MADE IN CHINA jua ni technological copy ya mtu/nchi Fulani na wamefanikiwa sana maana chochote ukipeleka kina pigwa copy tu.
 
Dunia imeishakuwa uwanja wa fuja. Baada ya Trump kuwapiga China na Tarriff ya 34% China wakajibu kwa 34%. Trump kawajibu kwa 104%!! Na zinaanza kazi kesho tarehe 9!! Kila mtu ajitafutie kashamba ka kulima mihogo, kufuga kuku, sungura, simbilisi nk. Nunua na baiskeli phoenix.

Seriously, haya yanamaanisha nini kwa dunia na sisi wa dunia ya tatu?
Ina maana sisi wa dunia ya tatu tuache wehu,uvivi,wizi na uzembe,na kuacha kuwa omba omba.
 
Rais Donald Trump anatarajiwa kuweka ushuru wa kushangaza wa asilimia 104 kwa bidhaa zote zinazoingia kutoka China kuanzia Jumatano, kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, aliyezungumza Jumanne.

Awali, China ilikuwa tayari inakabiliwa na ongezeko la asilimia 34 katika ushuru kuanzia Jumatano kama sehemu ya mpango wa Trump wa "ushuru wa kisasi."

Hata hivyo, rais ameongeza asilimia nyingine 50 baada ya Beijing kushindwa kufuta ahadi yake ya kuweka ushuru wa asilimia 34 kwa bidhaa kutoka Marekani kufikia saa sita mchana Jumanne – hatua ambayo imeongeza ushuru wa jumla hadi asilimia 84 zaidi.

Mapema Jumanne, Wizara ya Biashara ya China ilisema inapinga vikali ushuru huo wa ziada wa asilimia 50 dhidi ya bidhaa zake, ikielezea hatua hiyo kama “kosa juu ya kosa.” Wizara hiyo iliahidi kulipiza kisasi kwa kiwango kikubwa zaidi dhidi ya bidhaa kutoka Marekani.

President Donald Trump is set to impose an astounding 104% in levies across all Chinese imports on Wednesday, White House Press Secretary Karoline Leavitt announced on Tuesday. This comes on top of Chinese tariffs that were in place prior to Trump’s second term.

China was already set to see tariffs increase by 34% on Wednesday as part of Trump’s “reciprocal” tariffs package. But the president tacked on another 50% after Beijing didn’t back off on its promise to impose 34% retaliatory tariffs on US goods by noon Tuesday, adding an additional 84% in duties.

Earlier Tuesday, China’s Commerce Ministry said it “firmly opposes” the additional 50% tariffs on Chinese imports, calling it “a mistake upon a mistake.” The ministry vowed to escalate its retaliation on US exports.

Source: CNN

​
The power of intelligence
 
Hebu tuambie uvumbuzi au kifaa chochote unachojua kinatambulisha ni technology ya china.
China history Yao ni utengenezaji vyungu na dawa ya asili na si technologia.
Wewe unavyoona MADE IN CHINA jua ni technological copy ya mtu/nchi Fulani na wamefanikiwa sana maana chochote ukipeleka kina pigwa copy tu.

Sio kila kitu China Ina Copy Boss.....
A. Hivi unajua kuwa, China Inazalisha Internet yake peke yake, tofauti na huku Africa na Ulaya tunategemea Internet kutoka marekani? Na hii imefanya iwe vigumu sana kuwadukua.
B. Kwa sasa Wachina wamekuja na software ya computer na simu ( Harmony OS) ambayo tayari inafanya vizuri sana kule kwao tofauti na hizi za Microsoft zinazotegemewa na Ulaya na Africa....
C. Wachina wanakitengo kikubwa kuliko vyote duniani kwa ajili ya Ubunifu wa Tecnologia ambapo vijana wenye pass za juu kabisa kwenye Sayansi (vyuo vikuu) wanafadhiliwa na serikali kwa ajili ya Innovation tofauti na Marekani ambayo inasubiri mtu abuni technologia Nchini kwake halafu impore/imnunue na kumpa uraia ili iseme ni wamarekani wamegundua....
D. Hivi umewahi Kusikia ndege ya kichina ya kivita The Chengdu J-20, ambayo pia hujulikana kama "Mighty Dragon" kuwa mwangalifu kabla hujaibeza china!!!

Baadhi ya makampuni original from China na yenye mauzo makubwa ni;

1. Xiaomi:
A well-known phone manufacturer with a global following, known for its price-performance ratio.
2. TP-Link:
A company specializing in network-related products like modems and wireless routers.
3. UGREEN:
Known for producing USB cables and chargers of decent quality and design.
4. Haier:
A major appliance manufacturer that has been increasing its focus on innovation and quality.

USIWACHUKULIE POA WACHINA, WALE NI HABARI NYINGINE KABISA!!!
 
Mwamba anapambania uchumi wa nchi yake kwa kujitoa muhanga,na hamskizi yeyote.
Walichelewa sanaaa,China viwanda ndo vimempaisha na nchi yeyote yenye viwanda vingi lazima ipae kiuchumi.
Sasa viwanda pekee vilivyokua vimebaki na uhakika wa biashara ni viwanda vya silaha TU,Na silaha sharti lake ili uuze lazima upiganishe vita kwa kumwaga damu za watu.
Hatua ya Trump kiuchumi ni kubwa sana na China anaenda kudondoka kiuchumi si muda mrefu Kwa kua marekani uwezo wa kuidhibiti anao tena ni chap tu.
Wafanya biashara wa Marekani wanataka kuingiza ubinafsi TU wakati wanaitwa warudishe viwanda ndani watu wapate ajira,walipe Kodi,wajenge nchi kama ilivyokua miaka ya 1970'S.

China aendelee kuteneneza mafake yake aje alete kwetu mafeki zake,kwa Dunia ya kwanza lazima
Kwa hiyo usa ameshaajenga hivyo viwanda tiari
 
Rais Trump baada ya kuona hali ngumu, sasa ametangaza kuondoa ushuru kwa simu na laptops, kwa sababu Marekani inategemea sana China kwenye upatikanaji wa bidhaa hizo. Kama nilivyogusia awali, China ina uwezo mkubwa zaidi wa kuvumilia maumivu ya ushuru kuliko Marekani.
 
Hizi % ndio wanazotoza TRA kwa magari used kutoka nje. Gari ya milioni 8 TRA wanachukua milioni 10
 
Sio kila kitu China Ina Copy Boss.....
A. Hivi unajua kuwa, China Inazalisha Internet yake peke yake, tofauti na huku Africa na Ulaya tunategemea Internet kutoka marekani? Na hii imefanya iwe vigumu sana kuwadukua.
B. Kwa sasa Wachina wamekuja na software ya computer na simu ( Harmony OS) ambayo tayari inafanya vizuri sana kule kwao tofauti na hizi za Microsoft zinazotegemewa na Ulaya na Africa....
C. Wachina wanakitengo kikubwa kuliko vyote duniani kwa ajili ya Ubunifu wa Tecnologia ambapo vijana wenye pass za juu kabisa kwenye Sayansi (vyuo vikuu) wanafadhiliwa na serikali kwa ajili ya Innovation tofauti na Marekani ambayo inasubiri mtu abuni technologia Nchini kwake halafu impore/imnunue na kumpa uraia ili iseme ni wamarekani wamegundua....
D. Hivi umewahi Kusikia ndege ya kichina ya kivita The Chengdu J-20, ambayo pia hujulikana kama "Mighty Dragon" kuwa mwangalifu kabla hujaibeza china!!!

Baadhi ya makampuni original from China ni;

1. Xiaomi:
A well-known phone manufacturer with a global following, known for its price-performance ratio.
2. TP-Link:
A company specializing in network-related products like modems and wireless routers.
3. UGREEN:
Known for producing USB cables and chargers of decent quality and design.
4. Haier:
A major appliance manufacturer that has been increasing its focus on innovation and quality.

USIWACHUKULIE POA WACHINA, WALE NI HABARI NYINGINE KABISA!!!
Uko sahihi
 
Back
Top Bottom