Nyuma ya pazia Marekani nchi za kiarabu na Iran waongea kuhusu hilo shambulizi linoandaliwa na Iran lakini Iran lazima watafanya shambulizi.
Iran ana options nyingi tu na si lazima iwe ni makombora.
Iran yaweza kufanya mashambulizi ya "cyber attacks" ili kuua uwezo wa Israeli kwenye mitandao ya internet na mashambulizi mengine ya kimkakati.
"Miscalculations" yoyote italeta athari kubwa ndo maana bado Iran wametumia muda kupata shambulizi murua.
Lengo la Israeli na Marekani ni kutaka Iran akosee kufanya mashambulizi ili wapate sababu ya kushambulia vinu vya nyuklia jambo ambalo litaleta athari Iran zaidi kuliko Israeli na Marekani.
Ila Israeli atafaidika kwa kuwa na uhakika ametibua vinu vya nyuklia vya Iran visiwe na nguvu.