Uchaguzi 2020 Marekani yawasihi NEC na Magufuli kujali misingi ya demokrasia kwenye Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Marekani yawasihi NEC na Magufuli kujali misingi ya demokrasia kwenye Uchaguzi Mkuu 2020

Tatizo kubwa la afrika viongozi awaandaliwi Bali wanaokotwa tu, watu awaangalii hata background ya mtu alilelewaje, wanaokota tu yeyeto
 
Kwenye hyo barua hiyo sentensi ya mwisho hataa Mimi imenishangaza kama ilivuomshangaza Huyo senator. Eti wajumbe Wa NEC wanachaguliwa na Rais,nadhani dunia nzima hakuna nchi yenye huo mfumo,itakuwa ni Tanzania tu.
 
Tanzania sasa hivi ni nchi ya mfano sana ndiyo maana wanapiga kelele hivyo. Zamani tukiwa shamba la bibi walikuwa hawasemi kitu; na hata nchi zote zinazotuzunguka kama Rwanda ambayo inaongozwa kimabavu sana hawaisemi kwa vile haina manufaa sana kwao. yeye anshiwndwa kuzungumzia jinsi wapiga kura wa Marekani wanavyobanwa wasipige kura anakuja kuongelea mambo ya Tanzania.
Yaani wanajikangaja sasa; balozi ambaye ndiye yuko Tanzania anaongea mambo mengine, wakati yeye yuko huko milimani Idaho anaongea mambo mengine ya kufikirika tu.
Aisee sasa tumefikia pazuri, yan mpaka ccm sasa wanakiri jiwe ni dikiteita mbaya sana maana kama A ni sawa na C na B ni sawa na C basi A ni sawa na C pia ikimaanisha kama Kagame ni dikiteita mbaya sana aliyesababisha hali mbaya kwa Rwanda na kama Kagame huyo huyo ndiyo rafiki mkubwa na role model wa jiwe basi jiwe naye ni dkiteita mkubwa sana aliyesababisha hali mbaya sana kwa Tanzania, mbaya kuliko hata ile ya Rwanda..Jiwe lazima ling'oke.
Umoja wa Mataifa tusaidieni tafadhali tupate uchaguzi huru haki uwazi na usawa. Msituache hadi tutumbukie katika vita ya wenyewe kwa wenyewe sababu ya tamaa ya mtu mmoja tu na kakikundi kake kadogo. Asiposhinda kwa haki na ang'olewe tu.
 
Ishu sio kutishwa ishu Ni kuingia gharama kubwa Sana za kuhudumia wakimbizi sababu ya matumbo ya wachache kina jiwes and company.Kumbuka watawala wa kiafrica wanachoweza kwa bidii ni kuzalisha wakimbizi duniani na sio kuhudumia wakimbizi.
Shida ni viongozi wa kiafrika ama watu weusi ndivyo tulivyo mkuu, maana yake hata ukipewa wewe nchi utafanya hivyo Kwa sababu waafrika ndivyo tulivyo siyo?

Ningetaka kujifunza zaidi hapo mkuu
 
Uchaguzi wa Marekani unaotarajiwa kufanyika November mwaka huu umeingia kasoro nyingi kiasi kwamba Rais Trump amekataa kutoa ahadi ya kukubali matokeo yatakayotangazwa na tume.

Trump amesema kuwa utaratibu wa kupiga kura umepangwa kwa mtindo unaolenga kukandamiza wapiga kura wanaomuunga mkono.

Vilevile kumekuwa na hours kuwa matokeo ya uchaguzi huo yatachelewa kutolewa kwa sababu uhesabuji kura katika baadhi ya majimbo utaendelea kwa siku 4 baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa.
Wew siasa za Marekani hauzijui vzr na simfuatiaji au lugha ya kwao inakupa shida kuelewa unategemea taarifa zilizotafsiliwa kwa mlengo wa mtafusili. Marekani kuna carfew, wanapendekeza kura ya posta kwa sabab ya covid 19 jambo ambalo haliko kwenye utamaduni wa upigaji kura wa nchi hiyo. Jambo ambalo liko nje ya utaratibu Katiba yao inasema uamuliwa kwa maridhiano ya pamoja. Hicho ndo kinampa shida Trump sio kukataa matokeo. Hypocrite!!
 
Sasa utaendelea vipi bila kushirikiana na mabeberu, niambie kuna nchi gani imekuwa fukara kwa kushirikiana na mabeberu.
Madikteta awawapendi mabeberu sababu wanawanyima usingizi na kuwapunguza speed ya kuuwa watu,kuiba Kodi za wananchi,kuuwa demokrasia kwa hofu ya kunyimwa misaada na kupelekwa the Hague bila vitu viwili hivi madikteta yangemaliza watu.
Mkuu, kusema ule ukweli kabisa, ushirikiano wa Mabeberu Kwa nchi zetu hizi ni wa Wao Mabeberu wanufaike zaidi

Lakini Kwa nini kusingelikuweko na ushirikiano wa mambo ya Technologies Pekee na mambo ya kubadirishana mambo ya ujuzi Tu"

Maana hayo mengine ndugu yangu ni wizi Wao tu
 
NEC na CCM naona mmekaliwa kooni balaa!! Dr. Wilson naona safari zako za ICC sasa zimeiva. Maana jamaa wanasema hawashitaki taasisi bali wanachomoa wewe as wewe.

Cha kujiuliza ni nani mchawi kaifikisha Tanzania ya Nyerere yenye sifa kem kem duniani mahala hapa?
 
Mkuu, kusema ule ukweli kabisa, ushirikiano wa Mabeberu Kwa nchi zetu hizi ni wa Wao Mabeberu wanufaike zaidi

Lakini Kwa nini kusingelikuweko na ushirikiano wa mambo ya Technologies Pekee na mambo ya kubadirishana mambo ya ujuzi Tu"

Maana hayo mengine ndugu yangu ni wizi Wao tu
ni sawa na kuwa na jirani yako msomi ana magari 3, Moja lake, la mkewe na lingine a kupeleka watoto shule, nyumba nzuri, mboga 7, watoto wake wanasoma shule safi za fm academia - then wewe unamnunia, hutaki ushirikiano kisa eti anajidai ni TAJIRI.
 
Kamati ya bunge la Marekani la seneti ya mambo ya nje imeisihi tume ya uchaguzi Tanzania kujirekebisha, kuondoa makosa yaliyofanyika ndani ya miaka 5 iliyopita, kuacha kumshitaki Lissu kwa hoja ya kijinga.

Kamati hiyo inamtuhumu Magufuli kuminya Demokrasia, utawala bora, uhuru wa kujieleza toka ameingia madarakani miaka 5 iliyopita, wamemsihi kuwa sasa ni wakati wa kurekebisha makosa aliyoyafanya kwa miaka 5 iliyopita.

======

OCTOBER 05, 2020

CHAIRMAN RISCH: TANZANIA OFFICIALS MUST CORRECT PAST ERRORS AND HOLD CREDIBLE VOTE

BOISE, Idaho – U.S. Senator Jim Risch, chairman of the Senate Foreign Relations Committee, today issued the following statement regarding the recent suspension of the leading Tanzanian opposition candidate's campaign by electoral officials:

“Suspending the leading opposition candidate's presidential campaign on bogus charges raises serious questions about the independence of Tanzania's electoral commission. The political violence and repression of opposition candidates, restrictions on independent media, lack of autonomy and transparency by electoral officials, and government authorities' interference reflect Tanzania's history of flawed elections and the country's democratic erosion over the past five years.

“Despite profoundly troubling developments throughout the electoral campaigns, Tanzania's October 28 general elections provide an opportunity for President Magufuli and electoral officials to correct past errors and return Tanzania to a positive democratic trajectory by holding free, fair, and credible elections. Otherwise, Tanzania's continued democratic decline stands to undermine its future and will negatively influence democratic progress in the rest of the region.”

Background: On Friday, Tanzania's National Electoral Commission (NEC) suspended leading opposition presidential candidate Tundu Lissu from campaigning for seven days for violating the electoral code of ethics. The NEC accused Mr. Lissu of making seditious comments during one of his rallies in complaints filed by two political parties, including the ruling Chama Cha Mapinduzi party. NEC membership is selected solely by the president of Tanzania.

Chanzo:Chairman Risch: Tanzania Officials Must Correct Past Errors and Hold Credible Vote | United States Senate Committee on Foreign Relations
Talking to deaf ears
 
Ngoja nichague kilaza mmoja hapa kutoka Lumumba nilale nae mbele
 
He was just a mere mbunge hakuwa na maslahi ya urais,risasi zimemfanya ku build career ndio maana kapata jukwaa la kuongea na dunia sasa ana vie for post yenye maslahi na wazungu pia.Wazungu hawamuingizi mtu madarakani bali wanasapoti mtu wanaeweza fanya nae kazi,tutakaomuingiza madarakani ni sisi wapiga kura,ashinde au ashindwe kwa haki tofauti na hapo you will be in trouble
Let's face the music and see who dances better.
 
Kikubwa vyombo vya ulinzi, Nec, na wengine wajitahidi kila mmoja kutenda haki kama kweli kuna hizo kamatakamata za upinzani hazita saidia kitu zaidi ya kuharibu zaidi maana hayo yanayosemwa yataonekana kweli na ndo utakuwa ushahidi wao, imagine jirani kakuhisi unamtesa mtoto na wewe uanze kumfanyia vitimbwi mtoto tayari utakuwa umetengeneza ushahidi mwenyewe hata Lissu Sasa hivi asifanyiwe fitina maana itaonekana kweli Kuna ukandamizaji kikubwa tupendane bila kujali itikikadi siyo yako na hata inauma.
 
Wew siasa za Marekani hauzijui vzr na simfuatiaji au lugha ya kwao inakupa shida kuelewa unategemea taarifa zilizotafsiliwa kwa mlengo wa mtafusili. Marekani kuna carfew, wanapendekeza kura ya posta kwa sabab ya covid 19 jambo ambalo haliko kwenye utamaduni wa upigaji kura wa nchi hiyo. Jambo ambalo liko nje ya utaratibu Katiba yao inasema uamuliwa kwa maridhiano ya pamoja. Hicho ndo kinampa shida Trump sio kukataa matokeo. Hypocrite!!
Ulichoandika hapo ni uchemfu wa hali ya juu.
1. Marekani HAKUNA curfew.
2. Mail in ballot sio kitu kipya Marekani, kipo siku zote. Trump hutumia utaratibu huu kupiga kura miaka yote.
3. Katiba ya Marekani haikatazi mail in ballot wala haosemi kuhudu maridhiano.

Vijana wa Bavicha huwa mnadanganyika sana kwa kujifanya wajuaji.
 
Uchaguzi wa Marekani unaotarajiwa kufanyika November mwaka huu umeingia kasoro nyingi kiasi kwamba Rais Trump amekataa kutoa ahadi ya kukubali matokeo yatakayotangazwa na tume.

Trump amesema kuwa utaratibu wa kupiga kura umepangwa kwa mtindo unaolenga kukandamiza wapiga kura wanaomuunga mkono.

Vilevile kumekuwa na hours kuwa matokeo ya uchaguzi huo yatachelewa kutolewa kwa sababu uhesabuji kura katika baadhi ya majimbo utaendelea kwa siku 4 baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa.
Hatofanikiwa hawezi kumnyasa yoyote kwa kupingwa kwake anachotamani yeye kama rais tume haipangiwi nayeye anatamani ingekuwa anaongoza taifa kama tanzania rais ndio anataka nini kiwe nini kisiwe
 
Uchaguzi wa Marekani unaotarajiwa kufanyika November mwaka huu umeingia kasoro nyingi kiasi kwamba Rais Trump amekataa kutoa ahadi ya kukubali matokeo yatakayotangazwa na tume.

Trump amesema kuwa utaratibu wa kupiga kura umepangwa kwa mtindo unaolenga kukandamiza wapiga kura wanaomuunga mkono.

Vilevile kumekuwa na hours kuwa matokeo ya uchaguzi huo yatachelewa kutolewa kwa sababu uhesabuji kura katika baadhi ya majimbo utaendelea kwa siku 4 baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa.

Kwanza, kuhusu ulalamikaji wa Donald Trump kuhusu upigaji wa kura kwa njia ya posta ni maoni yake binafsi. Inawezekana anatafuta kisingizio kwani kwenye polls yuko nyuma zaidi ya points 10. Utaratibu huo umekuwepo kwa miaka mingi bila ya kulalamikiwa.

Pili, kuhusu Trump kwamba anaweza kukataa kuachia ofisi ni jambo la kupuuza. Ki historia jambo hilo halijawahi kutokea kwenye taifa hilo. Halafu hata ikitokea kwamba atakataa kuachia ofisi bado taifa hilo lina vyombo huru vya kumshughulikia mgombea huyo.

Napenda kumalizia kwa kusema kwamba hata kama kukitokea kasoro za hapa na pale kwenye uchaguzi wa Marekani lakini bado wataweza kuzitatua kwasababu wana vyombo madhubuti na huru. Vyombo madhubuti na huru vya kutatua mambo yao ndio tofauti kubwa kati yao na nchi isiyo ya kidemokrasia.
 
Hivi wale wamarekani weusi wanavyouawanl na mapolisi wao kwa ubaguzi huwa wanatoa matamko gani?
Wasijifanye wanajua demokrasia wakati kwao kuna madudu hawayasemi.
 
Marekani Ni Nani wao wenyewe wameshindwa kuwaonya wanaowauwa waamerika weusi afu wanaipangia Tanzania wapambane kivyao
 
Back
Top Bottom