Nakuelewa sana mkuu, ila elewa matokeo ya wanachokifanya tafsiri yake ni ugaidi.
Vipi kama kikitokea kikundi kikaanza kuteka viongozi wa serikali kwa mtindo huohuo kwa mfululizo itakuwaje?
Matukio kama kushambuliwa kwa Tundu lisu na yule mfanyabiashara wa Mwanza tuyatafsirije?
Serikali yoyote duniani ikikosana na wananchi wake matokeo yake ni kutengeneza mianya ya kuruhusu makundi ya kigaidi kujijenga na kuingia kwenye nchi husika
Kwa sasa kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa watanzania jambo ambalo linayafanya mataifa ya magharibi yachekelee tu yakijua kwamba siku yakiamua kufanya hii nchi isitawalike ni rahisi sana.
Kama chadema waliweza kupata zaidi ya kura milioni 6 unafiki kundi hilo lote linachukuliaje vitendo wanavyotendewa viongozi wao na baadhi ya wanachama wenzao? Kundi hilo ni watanzania na wapo karibia kila kaya hapa nchini, kuna hawa wastaafu wanatungiwa sheria za kipumbavu, kuna watu wa kanda fulani waliambiwa na kiongozi wa nchi kwamba, ndani ya utawala wake maendeleo kwao watasubiri, wengine walipewa upendeleo kwa kuwa ndio walimuweka madarakani eti!
Kuna kauli nyingi tata ambazo Watanzania wanazo vichwani mwao.
Mambo hayo yote yameleta mgawanyiko mbaya kwenye jamii ya Watanzania huku yakifumbiwa macho alafu leo hii litokee tatizo waanze kutaka wananchi wawe wamoja ilihali wameshawekwa kimatabaka.
Mataifa yaliyoshindana na mataifa ya magharibi yakashinda, kwanza kabisa yalianza kuwaunganisha wananchi wao ndipo yakaanza kupigana vita vya kujikomboa kutoka kwao.
Tunachokiona Tanzania ni tofauti.
Kwanza serikali iliyopo madarakani imefarakana na wananchi kwa kiasi kikubwa hadi kufikia asilimia kubwa ya wananchi kutamani mataifa hayo kuingilia kati