Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

Marekani yawatahadharisha raia wake wanaotaka kuitembelea Tanzania dhidi ya Ugaidi na uhalifu

Nakuelewa sana mkuu, ila elewa matokeo ya wanachokifanya tafsiri yake ni ugaidi.

Vipi kama kikitokea kikundi kikaanza kuteka viongozi wa serikali kwa mtindo huohuo kwa mfululizo itakuwaje?

Matukio kama kushambuliwa kwa Tundu lisu na yule mfanyabiashara wa Mwanza tuyatafsirije?

Serikali yoyote duniani ikikosana na wananchi wake matokeo yake ni kutengeneza mianya ya kuruhusu makundi ya kigaidi kujijenga na kuingia kwenye nchi husika

Kwa sasa kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa watanzania jambo ambalo linayafanya mataifa ya magharibi yachekelee tu yakijua kwamba siku yakiamua kufanya hii nchi isitawalike ni rahisi sana.

Kama chadema waliweza kupata zaidi ya kura milioni 6 unafiki kundi hilo lote linachukuliaje vitendo wanavyotendewa viongozi wao na baadhi ya wanachama wenzao? Kundi hilo ni watanzania na wapo karibia kila kaya hapa nchini, kuna hawa wastaafu wanatungiwa sheria za kipumbavu, kuna watu wa kanda fulani waliambiwa na kiongozi wa nchi kwamba, ndani ya utawala wake maendeleo kwao watasubiri, wengine walipewa upendeleo kwa kuwa ndio walimuweka madarakani eti!
Kuna kauli nyingi tata ambazo Watanzania wanazo vichwani mwao.

Mambo hayo yote yameleta mgawanyiko mbaya kwenye jamii ya Watanzania huku yakifumbiwa macho alafu leo hii litokee tatizo waanze kutaka wananchi wawe wamoja ilihali wameshawekwa kimatabaka.
Mataifa yaliyoshindana na mataifa ya magharibi yakashinda, kwanza kabisa yalianza kuwaunganisha wananchi wao ndipo yakaanza kupigana vita vya kujikomboa kutoka kwao.

Tunachokiona Tanzania ni tofauti.

Kwanza serikali iliyopo madarakani imefarakana na wananchi kwa kiasi kikubwa hadi kufikia asilimia kubwa ya wananchi kutamani mataifa hayo kuingilia kati
Nilishawahi kusema raisi ni baba wa wote, mtoto mkorofi anapoadhibiwa kupita kiasi ndugu zake watoto wazalendo wanaweza kuwa upande wake na wakamgeuka baba yao.
 
To hell with them, hata wamarekani wote na wazungu wasipokuja, it’s ok, hii warning ni utekelezaji wa mpango huu, hivyo they can just go to hell as long as tuna rafiki wa kweli Mchina, tukimkaribisha Mchina kwa bidii, anatosha
P
Hatuna nguvu ya kuchagua rafiki kati ya hao maana wao wapo kuchukua vilivyopo kwetu..Wachina hawana hurka ya kutalii kama Wamarekani ingawaje idadi yao inaongezeka siku hadi siku.
Wachina pia ni wachumi kwenye matumizi hata hapo Arusha wana hotel zao za bei za kawaida wakati mtalii mmarekani aogopi gharama hata tour guide atapenda kumpeleka Mmarekani kuliko Mchina kwa sababu ya tip nzuri..
 
kuna watu hawatokuelewa mzee, ila umeongea ukweli.
Nilivyoponzeka kwa uwasema US: ''Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza. Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo. Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama. Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.''

1545934890160.png
 
Hivi kwa hali hii bashite likizo atakuwa anaenda wapi??

Europe sidhani,america ndio doh,SA??,

Watakuwa washampiga stop kitambo.
 
Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru nchi yetu tumeichafua wenyewe mbele ya mataifa. Haya mambo yetu ya chuki chuki za kisiasa ya kutekana; kupotezana; kupigana ma risasi hadharani kumetuponza - wacha tuone...
....unawezekana wao ndo wanadhamini show ! Huoni wengine wanaruka dhamana makusudi tu ili watangaze nje kuwa wao ni wafungwa wa kisiasa.
 
Kwani ccm wanawapenda wapinzani? Ndio hayo hayo.
ccm na wapinzani ni watoto wa mama mmoja(tanzania) wasipopendana marekani anapata hasara gani mkuu!

marekani anapaswa ashughulike na mambo yake ya ndani

kila siku tunaambiwa watu wameuana kwa bunduki hapo marekani lakini hakuna hata siku moja walikua na tarifa kabla matukio hayajafanyika

hizi tarifa za ugaidi kwa watanzania wameujuaje

Eti misikiti na ubalozini ndio main target ya magaidi!!, kwanini tusihisi kwamba hizi ni mipango zao!
 
Hizo sifa sasa
Wamezidi nao hao USA
Sisi raia mbona hatuoni hivyo vitu,kwanini walishindwa kutoa hilo tamko enzi za kikwete Makanisa,misikiti na watalii walikuwa wanalipuliwa?
Waseme agenda yao wazi tuwahue.!
Wazee wa fitna hawana sababu ! Wanapiga bomu la sumu wao halafu wanakutwisha lawama wewe na adhabu wanakupangia.
 
Nilivyoponzeka kwa uwasema US: ''Mambo yalianza wakati sasa narudi Dar es Salaam na ndege ya Emirates iliyokuwa inatua usiku. Inaelekea maofisa wa pasi pale uwanjani walikuwa na taarifa zangu mapema na walikuwa wakinisubiri kwa hamu kubwa kwani nilipotoa pasi yangu kwa afisa wa pasi hapo ndipo shughuli za kunishughulikia zilipoaanza. Mimi sikuwa na hili wala lile. Nikawa namuona yule dada aliyekuwa kwenye kile kizimba akikukurika na pasi yangu akiitia katika mashine na kuitoa mara kadhaa. Fikra iliyonijia kwa haraka ilikuwa mashine ni mbovu na harakati zile zilikuwa ni kurekebisha mitambo. Kumbe sivyo wahusika nadhani walikuwa wanahakikisha kuwa mimi ndiyo huyo waliokuwa wakimwinda na kumsubiri na sasa kapatikana, kaingia mwenyewe kwenye mtego na kanasa. Yule afisa wa pasi akanambia nikae pembeni natakiwa kwa mahojiano na watu wa usalama. Hofu haikuwa imeniingia kwa kuwa nilikuwa natambua kuwa harakati dhidi ya ugaidi zilikuwa zimepamba moto na labda nilitakiwa kwa mahojiano mafupi kutaka kujua nyendo zangu. Sikujua wala kutarajia kuwa mshtuko mkubwa ulikuwa unanisubiri.''

View attachment 979144
Pole sana mzee.
 
Eeeh aiseee kumekucha kuna watu huwa wanapasha na kupiga kwata nchi nzima kisa raia wanataka kuandamana sasa ole wenu ugaidi utokee nchi hii

Au ni hao Wamarekani wameamua kupambana na jiwe kwa mbinu chafu ?

Dunia ina mambo hii
 
Mahoteli yatafikisika na kupunguza wafanyakazi,Makampuni ya kusafirisha Watalii yatapaki na kupunguza wafanyakazi,Volunteers hawatakuja kabisa.

Sasa tumshauri Mtukufu raisi na Makonda waongee na BAKWATA ili tupate watalii kutoka Yemen Sudan Syria Iraq Iran pamoja Libya Saudi Arabia na Sultanate of Oman waje kula nyama Pori kwa pilau
Chama cha Maaskofu kisaidie kuomba radhi na iwahakikishie mashoga usalama wao. Kanisa liaunga mkono kwa maslahi yetu.
 
Kwa mara ya kwanza tangu Uhuru nchi yetu tumeichafua wenyewe mbele ya mataifa. Haya mambo yetu ya chuki chuki za kisiasa ya kutekana; kupotezana; kupigana ma risasi hadharani kumetuponza - wacha tuone...
mazoea
 
ccm na wapinzani ni watoto wa mama mmoja(tanzania) wasipopendana marekani anapata hasara gani mkuu!

marekani anapaswa ashughulike na mambo yake ya ndani

kila siku tunaambiwa watu wameuana kwa bunduki hapo marekani lakini hakuna hata siku moja walikua na tarifa kabla matukio hayajafanyika

hizi tarifa za ugaidi kwa watanzania wameujuaje

Eti misikiti na ubalozini ndio main target ya magaidi!!, kwanini tusihisi kwamba hizi ni mipango zao!

Ccm na wapinzani ni watoto wa mama mmoja au nimesoma vibaya ulichoandika? Watoto wa mama mmoja kisha wapinzani wanafanyiwa ukatili wa wazi tena kwa uratibu wa vyombo vya dola? Acha Marekani aje atukumbushe kwamba sisi ni watoto wa mama mmoja maana tumesahau.
 
To hell with them, hata wamarekani wote na wazungu wasipokuja, it’s ok, hii warning ni utekelezaji wa mkakati huu
US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali? - JamiiForums
Hivyo they can just go to hell as long as tuna rafiki wa kweli Mchina, tukimkaribisha Mchina kwa bidii, anatosha
P
Hivi Pascal unaona mchina ni rafiki wa kweli au? Acha kuongea vitu rahisi nakuambia, hata kama unataka post ongea unachokiamini sio unachokifikiri!! Ok number haziongopi!
 
Back
Top Bottom