Marekani yazitisha nchi za Afrika zisinunue mafuta ya Urusi, nchi inayokaidi itashughulikiwa

Watu mnashindwa kuelewa kwamba hivyo vikwazo vimehidhinishwa na UN hivyo kila taifa linawajibika kuvitekeleza
 
Ngoja tuone viongozi wa Africa watakuja na agenda Gani [emoji38][emoji38]
 
Sasa kwa sababu hujui ndio usifanye jitihada zozote za kujitoa huko?

Mzungu anakusaidia kujitoa ila kila siku unamtukana na kumtunishia misuli ambayo yenyewe hauna, hata huyo mwarabu wenu hutegemea sana mzungu kwenye akili na maujanja yote, kazi yetu kuzaliana tu na kulalamika kila siku.
Muundo mbinu gani hapo Tanzania umesimamishwa na mweusi bila uhusika wa ngozi nyeupe tangu uhuru.
 
Wewe ni mtumwa wa wazungu na unastahili kuhurumiwa na kusamehewa bure!! Unawasujudia sana watu weupe!! Sishangai sana kwa kuwa huko kwenu Kenya "masetla" wa kizungu ndo bado wanashamba makubwa na wakenya hufanya kazi kwenye mashamba hayo kwa ujira kiduchu kama watumwa!
 
Ni aibu sana kwa taifa lenye nguvu kama marekani kuwatishia nchi za afrika ili zisinunue mafuta ya Urusi. Kama Marekani ana ubavu huo basi angeuonesha kwa kuyazuia mataifa makubwa kama Uturuki, India na China na menyewe yasinunue mafuta ya urusi!

Jana tu uturuki kakubaliana na Urusi kuendelea kununua mafuta ya urusi na marekani hana ubavu wa kuizuia!!

Putin praised the fact that trade volumes between the two nations grew by 57% last year and doubled in the first five months of 2022. He also noted that Russia supplies Turkey with all types of energy resources, including oil, gas and coal in a stable and predictable manner, “without any interruptions.”
 
Marekani imezoea kuonesha kuwa na nguvu kwa kuyaonea mataifa dhaifu lakini hana ubavu kabisa dhidi ya mataifa makubwa!! Marekani ilijaribu kuizuia Uturuki na India zisinunue makombora ya ulinzi wa anga ya urusi S400 lakini yakamtolea nje akabaki ang'ang'aa macho tu kwa aibu!!
 
Alafu wao wanayanunua
Wapuuzi sana wazungu!! Mpaka leo wananunua nmafuta ya urusi japo wanadai mwishoni mwa mwaka huu wataacha kununua. Lakini Gesi bado wanaililia! Halafu waafrika wanaambia ni marufuku kununua mafuta ya urusi japo wanayahitaji sana! Marekani na wapambe wake ni mawakala wa shetani!!
 
Tukisema Putin anapambana na jamaa hawa ili kuinusuru Dunia dhidi ya udhalimu wao,baadhi Ta JF members hatuelewi kabisa,wanafikiri tuna chuki binafsi dhidi ya Uncle SAM kumbe....

Yaani ugomvi wao wa siku nyingi tangu mwaka 1917 ndio wanataka kulazimisha Dunia yote iwachukie na kuwatenga Warusi iliwadhi malengo ya kisasa ya kutaka kuitawala Dunia kwa mabavu - Warusi na Wachina wakitaka kukomesha ujinga huu,mnaona wabaya ah hawajui wafanyalo!!

Haya mambo ya Ukraine na Taiwan ni gheresha tu za kutaka kutumia mataifa hayo kama battle ground ya kuwatumia watu wengine kupigana vita kwa niaba ya Merikani - lengo hasa ni mbinu za kuziharibu kiuchumi Urusi na China na kuzidhoofisha kijeshi bila ya Amerika kushiriki moja kwa moja kwenye mapigano ya vita.
 
S
Sisi nchi imefungua, tuagize mafuta, tz haiwezi tishwa na Marekani
 

Ndio ukweli haswaa.... hamna chochote zaidi ya ufisadi na kuzaliana na kumtukana mzungu ambaye unamtegemea hadi kwa ARV na condoms.
 
Kwani tukinunua mafuta watatufanya nini ? kwani kununua mafuta ni dhambi ....dawa ni bara zima la afrika kufunga barozi za USA, UK,FRANCE hizo nchi ni hasara kuwa na urafiki nazo
 
Pambafu zake kwa kuwa mbolea na ngano yeye ananunua ndio tununue ,asichonunua nasisi tusinunue .
Yeye ananunua hadi mafuta na nchi zote za NATO zinalilia gesi ya urusi ...sasa anatuambia sisi tusinunue mafuta ya bei nafuu kisa nini ...uchumi wa soko hulia hupo wapi hapo
Kweli nimeamini CCM NA SA100 NI [emoji117][emoji90][emoji90][emoji90] TU
 

China na Urusi wameishtukia hii dhamira ya USA.

Wamegundua kupigana vita ndani ya mipaka yao ni kudhoofisha mataifa yao. Ndio maana Urusi aliamua kwenda Ukraine otherwise vita vingekuja ndani ya mipaka ya Urusi, USA akitumia mamluki, double agents, wasaliti.

China aliamua asimzuie Pelosi na genge lake. Hakuna haja ya kudungua ndege ya viongozi wachache aanze kupiga vita kubwa ndani ya mipaka ya China.

Yeye ameamua kama vita ikitokea tupigane ndani ya Taiwan na huko baharini ambapo South Korea na Japan zitahusika pia. Madhara yake yatakuwa makubwa kwa USA na dunia nzima. Bidhaa, biashara nyingi, meli, ndege nyingi zinapita maeneo hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…