Marekani yazitisha nchi za Afrika zisinunue mafuta ya Urusi, nchi inayokaidi itashughulikiwa

Marekani yazitisha nchi za Afrika zisinunue mafuta ya Urusi, nchi inayokaidi itashughulikiwa

Msimamo sisi hatufungamani na upande wowote, pia tunatii matakwa ya vikwazo yaliyoidhinishwa na UN Security Council!!
===
Adui wao siyo lazima na kweli kuwa ni adui yetu!!! Nina imani Mama yetu ataupiga mwingi.
Maneno mengi , Tilalila nyingi kama nyinyi hamfungamani na upande wowote kanunueni hayo mafuta ya 🇷🇺🇷🇺 kama nyinyi ni wanaume . mbona mtayatapika 🇺🇸🇺🇸 akiwagundua .
 
Maneno mengi , Tilalila nyingi kama nyinyi hamfungamani na upande wowote kanunueni hayo mafuta ya 🇷🇺🇷🇺 kama nyinyi ni wanaume . mbona mtayatapika 🇺🇸🇺🇸 akiwagundua .
kalagha baho !!
 
Marekani imezitisha nchi za afrika zisinunue kabisa mafuta ya urusi!. Zinaruhusiwa kununua ngano na mbolea lakini ziachane na mafuta maana marekani imeyawekea vikwazo.

Swali: Je kuna nchi ya afrika itakayoweza kushupaza shingo na kununua mafuta ya Urusi? Labda Afrika ya kusini inaweza kumkomalia marekani na kusema haikubali kuingiliwa uhuru wake!

Kitisho kama hicho marekani alikitoa kwa India na China halafu ndo kwanza wakazidisha kununua mafuta na gesi ya urusi maradufu!!

  • Africa can buy Russian grain but risks actions on oil, says US​

    Washington’s ambassador to the UN has said that African nations are free to buy grain from Russia but could face consequences if they trade in US-sanctioned commodities such as Russian oil.
    “Countries can buy Russian agricultural products, including fertiliser and wheat,” Linda Thomas-Greenfield said at a news conference in the Ugandan capital, Kampala, after a meeting with President Yoweri Museveni.
    “We have no sanctions on any agricultural products coming out of Russia,” she added.
    “If a country decides to engage with Russia where there are sanctions then they are breaking those sanctions. We caution countries not to break those sanctions because then if they do they stand the chance of having actions taken against them for breaking those sanctions.” (Source- Aljazeera).

    Sisi hapa Tz sijui kama tunaweza kuwa na msimamo unaoangalia maslahi yetu tu bila kuangalia vitisho vya mabeberu!! Tatizo tunakopa mno, halafu hawakupi mkopo wote, wanakupa kidogo kidogo kwa kadri unavyozidi kuwaramba miguu na kuitikia "hewala bwana!".

Maskini kama wewe una maslahi gani?

Kwa nini unune mafuta yenye vikwazo?
 
Suluhisho ni kuchimba ya kwetu.
Tunaambiwa serikali ni tajiri lakini Cha ajabu wanashindwa kuwekeza kwenye vitu Kama hivi wanasubiri wawekezaji waje.
Hivi kweli serikali inashindwa kusema hapa tunaweka mitambo ya uchimbaji wa mafuta na gesi na tutawauzia wananchi wetu kwa Bei nafuu .Basi kopeni kwa ajili ya haya mambo ya msingi.
Unakopa unaenda kujenga madarasa ya corona
Vuta subra, kama nchi tumeanza mjaribio ya kujenga structures ndani ya bahari kupitia salender bridge. Baada ya hatua hii kukamilika kwa ufanisi sasa tutaanza kujenga tunels deep sea kuchimba mafuta.
 
Ila Kuna waafrika mnatia kichefuchefu Kama wewe jamaa

Halafu mnakufa wengi kwenye bahari mkihangaika kwenda kwa hao mnaowatukana......usisahau marais wa Afrika ambavyo huzungusha vibakuli kwao, nitawaambia ukweli mpaka basi...ha ha ha
Sijawahi kuelewa kwanini hampendi uarabuni japo wale huwa makatili sana.
 
Msimamo sisi hatufungamani na upande wowote, pia tunatii matakwa ya vikwazo yaliyoidhinishwa na UN Security Council!!
===
Adui wao siyo lazima na kweli kuwa ni adui yetu!!! Nina imani Mama yetu ataupiga mwingi.
Mama gani! Hapa angekuwa JPM sawa! Huku kuna Kabudi left winger fresh chini kuna Bashiru Ally mkabaji kuna Polepole wajamaa watupu kwa falsafa za Mwalimu Nyerere wangeenda Asia ila sio kwa Samia.
 
Tuige siasa za ndani za Marekani, ni nzuri mara 1000 kuliko zile za Urusi.
Pamoja na kuonyesha dharau za. wazi hivyo kwa Africa, bado unakuta kuna Mwafrika anaipenda Marekani . siasa za nje za Marekani ni za hovyo sana hasa kwa mataifa masikini kama ya Afrika.
 
Mama gani! Hapa angekuwa JPM sawa! Huku kuna Kabudi left winger fresh chini kuna Bashiru Ally mkabaji kuna Polepole wajamaa watupu kwa falsafa za Mwalimu Nyerere wangeenda Asia ila sio kwa Samia.
Aiseee kabudi alikuwa mtu na nusu
 
Halafu mnakufa wengi kwenye bahari mkihangaika kwenda kwa hao mnaowatukana......usisahau marais wa Afrika ambavyo huzungusha vibakuli kwao, nitawaambia ukweli mpaka basi...ha ha ha
Sijawahi kuelewa kwanini hampendi uarabuni japo wale huwa makatili sana.
Rubbish comment kichefuchefu
 
Ngoja tumtukane tuu mmarekani maana hakuna kitu tutafanya zaidi ya kutii amri🤣😂, nashauri tuongeze matusi na nimejiunga rasmi na warusi weusi wa JF
 
Back
Top Bottom