Wakati serikali ya awamu ya sita ikipambana kurudisha imani kwa wawekezaji wa nje na nchi wahisani kuwekeza mitaji yao nchini, adhima hiyo inaweza isifanikiwe kwa kuwa serikali imeshindwa kusimamia utawala wa sheria ulioanishwa kwenye katiba.
Wakichangia mada jana usiku kwenye mtandao wa Twitter kwenye mjadala uliondeshwa na Maria Sarungi, Wakili Fatma Karume na Mshauri wa uchumi Thabit wamesema imani aliyoanza kuijenga Rais Samia Suluhu Hassan kwa wawekezaji wa nje na jumuiya za Kimataifa imepotea kwa kitendo cha kukamatwa Mh. Freeman Mbowe na kuzuia Kongamano la Katiba Mpya.
"Nimezungumza na Diplomat wengi wanafuatilia swala hili na vyombo vingi vya habari vya nje wameandika. Sasa kazi kubwa aliyoanza kuifanya ya kushawishi wawekezaji amejiharibia huko ni sawa na kujifunga goli mwenyewe" asema Thabit.