Maria Sarungi alipewa na nani siri ya Ziara ya Rais Samia Nchini Marekani wiki moja kabla ya kutolewa Taarifa rasmi?

๐Ÿ—ฃ๏ธ๐Ÿ—ฃ๏ธ๐Ÿ—ฃ๏ธ
๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ
 


Hakuna ziara ya Siri Kwa Rais

Wakianza mambo ya kuomba visa Tu watu wa ubalozi wanajua

Pia anaenda na ndege ya Abiria au serikali means kuna maandalizi logistics zote zinashughuliwa na watu mchanganyiko

So ukiangalia huo muingiliano wa watu hapo hakuwezi kuwa na siri
 
Weye mwenyewe kwa uwezo wako wote wa kiakili wadhani ziara ya raisi Samia nchini Marekani ni siri?

Umeuliza suali la kitoto sana labda kama una "beef" na huyo Maria Sarungi.
 
wenyewe wanaohusika na usalama wanatowa leakage kwa sababu za kiusalama.

Usistuke.
Hakuna mtu yoyote wa usalama (wa Tanzania) ambae ata-leak taarifa kama ziara za nje khasa Marekani.

Upo utaratibu ambao huanzia na maombi ya visa ubalozini hadi kuhusisha State Deparment kule kwenyewe.

Baada ya hapo kuna masuala ya clearance na kutayarisha itineraries ambayo hupewa mazee wa Department of State idara ya kulinda viongozi wa nchi za kigeni (foreign VIPs) DSS au diplomatic security services ambao huandaa kila kitu khasa ulinzi, ratiba ya ziara na mengine.
 
Ziara za Rais sio siri hasa anapotaka kwenda nje ya nchi. Kuhusu Maria ni wa kumpuuza maana hajawahi kuwa na jema awamu zote. Akivuka mipaka atashughulikiwa na vyombo vya dola.
 
Hizo zote usemazo ni kawaida za safari. Mimi siziongelei hizo wala sijajibu hizo. nazifahamu kabla hujazaliwa. Tena kuna zingine za VIP, ambazo naamini kwa asilimia mia moja, huzielewi.

Sipo huko wala sikuwa huko nilipojibu. Nipo kwenye leakage za information zilizomshangaza mleta mada.

Sikushangai, wewe itakuwa ni katika wale wanaoitwa kondoo wanachekelea.
 
Swali ni kwa nini Ikulu hawatoi taarifa mpaka Maria Sarungi anatoa?
 
Hizo zote usemazo ni kawaida za safari. Mimi siongelei hizo wala sijibu hizo.

Tena kuna zinhgine za VIP ambazo huzielewi.

Sipo huko wala sikuwa huko nilipojibiu.

Sikushangai, wewe itakuwa ni katika wale wanaoitwa kondoo wanachekelea.
Angalia makazi yangu, I know everything ila hayanihusu lakini penye kurekebisha naingia.
 
Je taarifa rasmi kuhusu safari hii imetoka!? Na kama haijatoka ni kitu gani kimeharibika? Je kuna hatari ya kiusalama namna hiyo kwamba safari ya Samia ikifahamika kwa watanzania kuna tatizo!?

Kitendo cha Maria kufahamu kuhusu taarifa hizi ni kosa kisheria? Je ni jinai? Je watanzania hawana haki ya kujua Samia anakwenda wapi? Hiyo safari anatumia pesa za watanzania sio pesa zake, ni kodi na tozo za watanzania!

Halafu Mkuu ukishakubalia kuwa mtumishi wa umma kuna uhuru fulani personal unaupoteza! Kazi za Samia sio private tena!? Hatuna haja tena ya kumuachia Mkwe wake na Binti wawe wanamsaidia kuendesha nchi kama ni familia yake!

Samia ni mtumishi wa umma na analipwa pesa ambazo kimsingi ni pesa za watanzania! Sasa kwanini muajiri wako asijue sehemu ulipokwenda!?
Kama mtu hakati kufuatiliwa basi abakie na familia yake Kizimkazi uone kama kuna watu wataendelea kumuuliza anafanya nini!?
 
Sawa bibie nadhani tumeelewana.
Nadhani wewe umeelewa, kuwa haziongelewi "itinerary" za safari. Mleta mada kaongea wazi "leak" ya uwepo wa safari. na ndicho nilichojibu mimi.
 
Nachani wewe umeelewa, kuwa haziongelewi "itenerary" za dafari. Mleta mad kaongea wazi "leak" ya uwepo wa safari. na ndicho nilichojibu mimi.
Nami pia nimejibu kwamba hakuna mtu yoyote amevujisha hizo taarifa.

Maria Sarungi ana vyanzo mbalimbali ndani na nje ya TZ hivyo huwezi kusema kuna mtu amevujisha kama moja ya vyanzo hivyo vimempatia taarifa.

Usisahau hata hao waandaji wa mkutano anohudhuria raisi Samia waweza kuwa wametoa hiyo taarifa mapema.

Pia kuna kitu nimegundua, ni weye watumia keyboard au kuna mtu kaazima?

Nachani= Nadhani

dafari= safari

Hata weye waweza kukosea na ukaandika maneno ya ajabu.

Be humble.
 
Hivyo "vyanzo mbali mbali" ndiyo "snitch" katokea humo.


Nini ambacho huelewi hapo?
 


Ni muhimu sana ukaanza na "Ndugu zangu wana ccm"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ